Baba wa ubatizo wa mwanangu ana uhusiano wa kimapenzi na mama wa mwanangu. Navukaje hapa?

supatolu

Senior Member
Aug 7, 2022
137
180
Wakuu, mwaka 2016 nilifunga ndoa ya kiserikali. Ilinilazimu kufanya hivyo kutokana na uhalisia wa mazingira niliyokuwa naishi na mwenzi wangu huyo wakati huo. Mwaka 2019 mwezi Disemba tulifanikiwa kupata mtoto. Na ilipofika Januari 2021 tuliamua kumbatiza mtoto wetu. Kama kawaida ya imani yetu ilibidi mtoto awe na wazazi wa kiroho. (Baba na mama wa ubatizo) ambao kiutaratibu mzuri wawe ni mume na mke. Mke wangu alimpendekeza jamaa mmoja ambaye tunasali nae na ni kiongozi pale kanisani. Nikaafiki na jamaa na mke wake walikubali na kusimamia ubatizo wa katoto ketu.

Ilipofika mwezi machi 2021 nilikuja kugundua kumbe mama mtoto wangu ana mahusiano na baba wa ubatizo wa mtoto wetu. Na uhusiano huu waliuanza zamani kabla hata ya mimi kukutana na huyu binti. Sikulijua hilo hapo awali.

Yaani jamaa ana mke wake, huyu binti alikuwa mchepuko wake kitambo. Hadi mimi naanza mahusiano na binti huyu kumbe wako pamoja na mpaka tunapanga jamaa na mke wake wasimamie ubatizo wa mtoto, kumbe jamaa anamegaga tu mi sijui.

Baada ya kugundua hilo nilikaa takribani miezi mitatu mbele ili nifanye uchunguzi kwa mapana zaidi. Lakini nadhani mwenendo wangu katika kipindi hicho ulimfanya wife ahisi “kuna kitu” hakiko sawa. Kufupisha stori, wife aligundua kuwa nimeshaijua siri yake na “baba wa ubatizo” wa mtoto wetu. Akaondoka kimyakimya akarudi kwao. Akamweleza yote mama yake mzazi.

Mama mkwe alinipigia na kuniomba nimsamehe binti yake na kwamba yeye atamkanya. Kifupi bibie alikiri kosa ila alikuwa hana ujasiri wa kuongea mbele yangu ndio maana akakimbilia kwa mama yake. Nilimpa sharti kuwa awe tayari kuomba msamaha kwa mke wa jamaa maana bila kufanya hivyo ni dhahiri wangeendelea na jamaa. Hakuweza kabisa kufanya hivyo ndio maana namimi nikampotezea jumla mpaka leo.

Pia jamaa nae aliwahi kunipigia na kujifanya ananiulizia hiyo habari na akaniomba tukutane naye eti “tuzungumze kama wanaume”. Sikuwa tayari maana huwa nina hasira sana.

Ishu iko kwa mtoto. Japo ninamhudumia akiwa hukohuko kwa bibi na mama yake ila sijaridhika. Je kisheria naweza fanyaje ili nipate nafasi ya kuwa na mwanangu kwa umri alio nao? Kiukweli aina ya malezi kwa pale kwa mama mkwe sio kabisa.

Pili sasa hivi nina mchumba mwingine na tunatarajia kufunga ndoa mwakani mwezi Juni. Ninahitaji kumhudumia mke wangu mpya ikiwamo bima ya afya n.k. Je nitakuwa sahihi nikisitisha huduma hiyo kwa huyu mama wa mwanangu na kuzihamishia kwa huyu mtarajiwa wangu?
 
Gharama ya kuvunja familia ni kubwa sana. Mungu atusaidie atuepushe mazingira yanayosababisha kuvunjika kwa familia.

Ila pia wanaume mnatongoza wake za watu mnawamega, mkimegewa uchungu wake hamuuwezi. Muosha huoshwa. Kila mmoja ajiheshimu.
 
Wakuu, mwaka 2016 nilifunga ndoa ya kiserikali. Ilinilazimu kufanya hivyo kutokana na uhalisia wa mazingira niliyokuwa naishi na mwenzi wangu huyo wakati huo. Mwaka 2019 mwezi Disemba tulifanikiwa kupata mtoto. Na ilipofika Januari 2021 tuliamua kumbatiza mtoto wetu. Kama kawaida ya imani yetu ilibidi mtoto awe na wazazi wa kiroho. (Baba na mama wa ubatizo)
Kitu cha kwanza na cha muhimu zaidi ni uhakika wa kwamba huyo mtoto ni mwanao. Unaweza kuta huyo mtoto mwenyewe ni wa huyo jamaa "baba wa ubatizo". Ningekuwa katika nafasi yako ningefanya utaratibu wa kupima DNA kisheria, na kwa sababu mama wa mtoto amekiri uchepukaji, haitakua ngumu sana kupata kibali cha mahakama/barua ya social wellfare itakayowezesha upimaji wa DNA.

Kuhusiana na suala la pili, inabidi ufuatilie talaka rasmi mahakamani uachane kisheria na huyo mama mtoto wako, maana mlirasimisha unganiko lenu kisheria mahakamani, hivyo lazima pia unganiko hilo litenguliwe mahakamani kisheria kabla huja move on na kuoa mwanamke mwingine. Pole kwa yote mkuu.
 
Wakuu, mwaka 2016 nilifunga ndoa ya kiserikali. Ilinilazimu kufanya hivyo kutokana na uhalisia wa mazingira niliyokuwa naishi na mwenzi wangu huyo wakati huo. Mwaka 2019 mwezi Disemba tulifanikiwa kupata mtoto. Na ilipofika Januari 2021 tuliamua kumbatiza mtoto wetu. Kama kawaida ya imani yetu ilibidi mtoto awe na wazazi wa kiroho. (Baba na mama wa ubatizo)
Ww ndyo mwanaume hata mm nishasema eti nimehakikisha kabisa wife anachepuka halafu eti unaambiwa msamehe hyo sikubaliani ni kumuacha moja kwa moja umefanya jambo zuri sana hawana akili hawa sijui wapoje yaan wanawake akili zao dah

Cha kukushauri huyo mtoto mkapime DNA isije ikawa mtoto wa huyo jamaa wanawake wajinga sana
 
Gharama ya kuvunja familia ni kubwa sana.
Mungu atusaidie atuepushe mazingira yanayosababisha kuvunjika kwa familia.

Ila pia wanaume mnatongoza wake za watu mnawanega, mkimegewa uchungu wake hamuuwezi. Muosha huoshwa. Kila mmoja ajiheshimu.
Msitishane, hakuna gharama yakuvunja familia, ni kuamua tu. Gharama kubwa ni kuvumilia maumivu ambayo mwisho wa siku utalazimika kufanya maamuzi magumu/ya ajabu. Ndoa siyo kifungo.
 
Aisee pole sana na Hongera kufanya maamuzi ya Kiume...!!

Ushaurii ambao utakusaidia sana tafuta mwanamke mwingine anzisheni maishaa ilaa mwanao muachea aendelee kulelewa na mwanae so long mama yake yupo tayari kumlea kuliko kumleta alelewe na huyo mwanamke ambae utamuoa anaweza nyanyasika zaidi.
 
Wakuu, mwaka 2016 nilifunga ndoa ya kiserikali. Ilinilazimu kufanya hivyo kutokana na uhalisia wa mazingira niliyokuwa naishi na mwenzi wangu huyo wakati huo. Mwaka 2019 mwezi Disemba tulifanikiwa kupata mtoto. Na ilipofika Januari 2021 tuliamua
Pamoja na madhira yote bado unataka kuingia kwenye ndoa ya pili!!!??? Kweli sikio la kufa....kwani ukiishi mwenyewe utakufa? Endelea na upumbavu wako.
 
Back
Top Bottom