DSN
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 2,837
- 1,674
Kama taarifa hii ni kweli wakati JK akiwa Mwanafunzi wa elimu ya siasa chuoni Monduli,alipowasilisha taarifa yake kwa Baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere,na kisha Baba wa Taifa kuukabidhi waraka huo kwa wakuu wa kijeshi wa JK ukiwa kama ulivyo pasipo kuficha jina au utambulisho wa mtoa taarifa.Hakika tendo hilo halikuwa sawa hata kidogo na ndio chanzo na tatizo la sura ya utawala huu tulionao sasa,ambao uliacha kovu moyoni mwa mhusika ambae kwa hakika kwa kuwa alichokiwakilisha kilikuwa ni kweli kulingana na siasa za ujamaa [Comrade System] na kujikuta anaingia matatizoni na kumuacha akishindwa kujua msimamo wa Itikadi ambayo ametumwa kuisambaza na kuitetea.
Namheshimu sana Baba wa Taifa mpaka hapo alipotufikisha,lakini nae pia anayo yake ambayo yamechangia pia kutufikisha hapa tulipo leo hii.Kitendo cha Mwalimu kutoa taarifa hile ya JK kwa Wakuu wa Jeshi ikiwa na jina la Mhusika au mleta taarifa kilikuwa ni UCHONGANISHI, japo kwa upande wake pia hatujui kama alikujua kama Mkuu wa Majeshi uenda angeipeleka kama ilivyo eneo tajwa na mtoa taarifa [Ukizingatia upeo wa Elimu wa Wakuu wa Jeshi wa zama hizo].
Kikwete kama kijana mdogo ambae aliitaji kuongozwa kupitia wakubwa wake ukizingatia unyeti wa kazi yake,lakini the Court break become the court breaker. Hatimae songombingo hilo la wakuu wake na songombingo la wanafunzi wenzie wa kitaaluma wa kada ya kijeshi ambayo yeye alisimama katika kada ya siasa, vilimshape na kumuweka katika hali tata sana kisaikolojia.Na hata dhamira yake kusimama kama Rais wa Nchi hii siku moja kwa kusudio la kujenga kile ambacho alikiona na kuamini toka ujana wake akifikilia kuwa angeweza, lakini kumbe sivyo kulingana na mfumo [system].Lakini kwa kuwa mambo yale yale ya the Court Break become the Court Breaker pamoja na kuibuka kwa Azimio la Zanzibar, yale ya kule chuo yalikuwa yamekwisha sambaa sehemu kubwa ya Nchi yetu na idala nyingi za Serikali.
Tufike sehemu tukili kuwa tunahitaji watu jasiri ambao kwanza hawakuwepo kwenye zama za kumjua huyu alikuwa nani,watakao wasulubu hata rafiki zao endapo wametenda ndivyo sivyo,lakini kwa style ya Jakaya Kikwete kila akikumbuka aliko toka na njia alizopita na mafairi yanayopita mikononi mwake yakiwa na taarifa kadha wa kadha juu ya wale wale aina ya viongozi waliokuwa chini ya Mwalimu ambao kwake ni senior toka akiwa kijana anakosa nini cha kufanya.
Kwangu mimi yeye nilipenda kuona kuwa anakuwa Free Mind Man,alipofika yeye hadhi yake kama Rais hana wa kuwajibika kwake bali kusimamia kile ambacho anakiamini pasipo kuhesabu yaliyopita huko nyuma.Kwa kuwa yaliyotokea kwake MUNGU ALIKUWA NA SABABU NAE NDIO MAANA AKAWA RAIS ILI MUNGU AFIKISHE UJUMBE KWA WALE WOTE WALIOMTENDEA YALIYOPITA, AKIWA NA DHAMIRA YA KWELI KWA MUJIBU WA ITIKADI YA WAKATI HUO.
Lakini nae kageuka kuyafungia macho hayo na hakika nae woga huo ataulipia kwa style ya namna yake.Atuthibitishie kuwa Mwalimu hakumtendea haki.Nasi tutapata cha kujifunza na watu kutambua haya tuliyonayo ni matokeo ya historia ya yale yaliyotokea kwake pia asisahau kutuandikia kitabu haswa sisi vijana wa kizazi kipya ambao tutajifunza kupitia kitabu hicho.
NINA MUHESHIMU BABA WA TAIFA MWALIMU JK NYERERE, LAKINI KWA HILI MWALIMU HAKUMTENDEA HAKI HATA KIDOGO?
Nawasilisha