Baba wa Taifa hakumtendea haki Kikwete, Ndio maana tuko hapa tulipo?

kwa classic management principle zilizotawala enzi zile Mwl alikuwa sawa kabisa.mifumo ya mwanzo ya utawala wa kiraia ime originate kutoka jeshini.Watu wanachangia hii mada wakiwa na hisia za Kikwete kama rais wa nchi sasa,hebu fikirieni askari wa cheo cha chini kule kaboya leo amuandikie malalamiko ya kijeshi Kikwete!

Ata hivyo umenipa Shule Mkuu MM sana tu,namuangalia Obama na Jobs speech

Afadhali umeachana na maswali yako, mimi yalianza kunikera mno kwa sababu, ulikuwa una spin hoja zilezile huku ukipoteza muda na kuonesha kushindwa kusoma ama kuelewa majibu uliyokuwa ukipewa.

Kikwete ni janga la kitaifa, na kwakweli ni vigumu sana kumtetea Mheshimiwa wetu huyu. Mimi nilimuunga mkono alipojitosa kwenye kinyang'anyiro cha uraisi kwa mara ya kwanza mwaka 2005, nilidhani ni mwanajeshi kweli, na mwana TANU aliyeiva... kwamba atatutapatia uogozi uliotukuka, sasa najuta, nilikosea.

Jamani, wa-Tz wenzangu, tusiwe tunazunguka mbuyu, matatizo yetu kwasasa hayatokani na Nyerere kama Nyerere na ujamaa wake. Kuendelea kushikilia hoja hizo ni kuruhusu chuki zinazotokana na ama ukabila, udini, au race supremacy, kutuburuza na mwisho tutakuwa tumepotoka milele. Tutakuwa vipofu na kwa hasara yetu sisi wenyewe na taifa letu. Nyerere hakumwagiza Mwinyi kuuza Loriondo, kutorosha wanyama na dhahabu zetu, wala hakumwagiza mtawala dhalimu BW Mkapa kuuza mashirika ya umma, madini yetu na nyumba za serikali. Haya ni matatizo yetu, tumeyazalisha sisi na Nyerere asingeweza kuyafanya katika uongozi wake.

Tuyapime matatizo yetu kwa context ya wakati wa sasa, viongozi wa sasa, sera tulinazo sasa na siasa hizi mpya. Kama Nyerere aliharibu over 21 years ago, mbona ina hitaji miaka 10 tu kwa kiongozi mzuri na sera nzuri kuleta mapinduzi ya uchumi katika nchi yenye maliasili nyingi kama TZ. Maziwa, bahari na mito peke yake yanatosha ku-sustain uchumi wetu kuwa mzuri kuliko sasa kama ukisimamiwa vizuri. Tangu tumeanza kuchimba gas, madini, ardhi na kubinafsisha mashirika ya umma hatujawahi kuona impact yoyote kwenye ukuaji wa uchumi wetu mpaka sasa. Inflation iko juu, exchange rate inaelekea kwa Mugabe, ufisadi unafikia kiwango cha India, Bangladeshi na Srilanka.

Mwacheni Nyerere apumzike. Tusiruhusu chuki dhidi yake kutawala mioyo na fikra zetu. Mungu katuumba sisi wote na yeye ndiye atatoa hukumu siku ya kiyama.

Heshima kwenu wote mlioshiriki mjadala huu.Hivi mpendwa mwanakijiji 'how old r u?

Kuexpose Identity ya Jakaya Kikwete Kwa Makamanda wake wakati anajua kuwa yule ni junior,na kuwa alichofanya kama kijana ambae anafundishwa kuwa mjamaa anamuona Kiongozi katika style ile ya kimaisha nae anatumia wajibu wake wa kijamaa kupeleka taarifa kwa mkuu wa chama na ambae ndiye Rais wa Nchi.Kisha kiongozi huyo ambae ni Rais anaitoa taarifa hiyo kwa makamanda wake pasipo kuficha utambulisho [Identity] ya mtoa taarifa hakika kwa usalama wa mtoa taarifa ni kitendo kibaya na hatari.

Kupitia hayo na mengineyo ambayo hayajasemwa hapa kwa kuwa wenyewe bado wapo si vyema kuyasema muda ukifika watu pia watajua.Hakika kama binadamu mwingine yoyote ni hakika yalimpa historia ambayo leo watu wanalalamika juu ya utawala wake,lakini kupitia experince ya matukio hayo yamemshape hivi alivyo leo.Yamemtengeneza kuwa mwoga juu ya maamuzi.

Mwl. Nyerere alimjua JK kuliko tunavyoweza kufikiria! JK hiyo ndio hulka yake! Kwa taratibu za jeshini hasa kwa wale waliobahatika hata kupitia tu JKT wanaweza kuelewa maana yake ni nini kwa kiendo alichofanya JK kwa wakati ule! Jeshini kwanza kulikuwa hakuna siasa ya kihivyo it was a matter of obeying orders - fullstop! Tena ukiwa mkufunzi umeona jambo ndio sivyo, unashindwa kuripoti kwa Mkuu wa majeshi unaenda moja kwa moja kwa Rais! Duuh... yataka mzoefu kwenye upishi wa majungu na guts za kutosha! Rais aliona kitendo hicho kikamalizwe hukohuko jeshini - he was right! na kwa kuwa hakutaka unafiki aliirudisha barua ya JK kwa mhusika.

That is not an excuse kwa JK kushindwa kiuongozi. Tabia hujengeka tangu utotoni na hayo ndio makuzi yake ndio maana tupo hapa leo!!

Uoni kuwa kulitengenezwa nidhamu ya woga ambayo baada ya kifo chake kila kitu kimekwenda nae.Naona heri ya Kikwete aliyejaribu kumuandikia Mwenyekiti wake Baba wa Taifa,na kutokana na historia hiyo ya watu kumuogopa Mwalimu baada ya kumuheshimu kulikuwa na viongozi copy alipofariki viongozi originar na makucha yao wakajitokeza kwa wingi.

Na kwa kuwa Kikwete alikuwa anawajua na kwa kizazi chake awezi kushinda nao alichofanya kwa sasa ni kutusaidia kuwa huru kifkra hata leo hii tunaweza kuchambua kwa uhuru huu.Tambua kuwa kuna baadhi wana mind sana kuona mko huru hivi na media chungu mbovu.Wanasema ameshindwa kutawala sababu ya kutoa uhuru huu wa kujieleza na uliopitiliza,mpaka wengine wanajaribu kujenga hoja kuwa uhuru bila mipaka ni fujo.

Hawajui kuwa haya yote yanayojili ni Kikwete kutimiza evolution na kutokana na historia na maisha yake kama Mtanzania,ambae pia Mungu kwa namna yake kampa nafasi 2005 kutushape Watanzania kwa kiwango chake,japo na yeye pia kapungukiwa kwa kuwa alipaswa kutenda kwa mujibu wa Matakwa ya Watanzania,sio kwa Matakwa yaleyale ya yaliomsibu huko Monduli na alikopita kama kijana wa Chama cha Mapinduzi.

Umefulia!!!

Mkuu Edson ebu vaa viatu vya huyu jamaa na wewe ndio junior [UJANA] over ambitious kama kada ulietumwa kueneza siasa sio mbinu za kivita kisha unayakuta ya Mkuu yuke unatoa taarifa zako kisha wanakukaanga.To be frank leo hii mnamkubali Zitto,nina hakika Jakaya wakati huo alikuwa ni zaidi ya zitto kwa kuwa kumbuka ulikuwa ni mfumo wa chama kimoja.Matendo ya Zito kufumua uchafu tunaoukubali sasa unatofauti gani na wakati huo kwa itikadi hiyo ya ujamaa na masharti yake ambayo kwa wakati huo huyu kama kijana yalikuwa kichwani kama saa na mkono.

mkuu naamini nyerere hakukurupuka ku'expose ule waraka wa siri! alipima na tabia za mleta waraka ule, inawezekana kabisa nyerere amepokea nyaraka nyingi tu tena nyingi sana kutoka kwa ma'junior mbali mbali lakini haja expose, sijui ni kwanini umemtetea JK hivyo wakti hata huo waraka wenyewe hujausoma umeandikwaje, au nyaraka nyingne nyingi alizowahi kumtumia nyerere.

DSN, kosa kubwa unalolifanya hapa ni kudhania kusiko sahihi. Unadhania wakati wa Kikwete kulikuwa na tofauti kati ya Mwanajeshi wa Taluma na Mwanasiasa Mwanajeshi. Hapa ndipo panapokutatiza. Hata hivyo si tatizo la lazima.

Kabla ya maasi ya 1964 jeshi letu lilikuwa kwa kiasi kikubwa likiwa ni masalio ya jeshi la kitaalum la kikoloni (King's African Rifle ambalo lilibadilishwa baada ya uhuru na kuwa Tanganyika Rifle). Jeshi lile kwa kiasi kikubwa lilikuwa ni non-political. Maasi ya 1964 yakafunua kwa kiasi kikubwa sana udhaifu wa jeshi la namna hiyo ambalo halikutokana na wananchi wenyewe wala halijajikita katika siasa na maisha ya wananchi wake. Na Nyerere aliona hasa baada ya matukio kadhaa ya mapinduzi ambapo majeshi yaliyoachwa na wakoloni yalipoanza kutumia nguvu kuchukua madaraka kwenye nchi.

Nyerere alitambua wakati ule kuwa jeshi letu tulilorithi kutoka kwa mkoloni lilishaanza kuonesha dalili ya majeshi mengine nayo ni kutamani kushika madaraka ya nchi na utoana elements zile zile zikajitokeza baadaye. Hii ndio sababu ya TR kuvunjwa. Kwa miezi kadhaa Tanzania haikuwa na jeshi lake isipokuwa majeshi ya Uingereza kwa muda na baadaye ya Nigeria hadi pale jeshi letu lilipoundwa from scratch.

hapa ni muhimu kuelewa tulipoanza kuliunda jeshi upya tuliliunda kwa makusudi kabisa kuwa ni a politicized military kama lilivyo jeshi la China hivi au Cuba. Hivyo JWTZ lilivyoundwa lilichukua vijana wa TANU na muundo wake ukafungamanishwa kabisa na moja kwa moja na siasa za TANU. Wanajeshi wetu wakajifunza siasa za TANU, malengo ya TANU na hata kuwa na mfumo wa mahusiano ya kisiasa ya jeshi na chama.

ni kutokana na hilo ndio tukaja kuwa na jeshi pia kama tawi kubwa la TANU ambapo kambi na vituo vya jeshi vilikuwa pia ni matawi ya CCM na hili halikuwa kwa jeshi tu bali hadi polisi, na Magereza. Kuelewa hili ndilo litakusaidia kuelewa kilichotokea kwani wakati wa kikwete na tukio hili tunalosimuliwa hakukuwa na tofauti kati ya mwanajeshi taaluma au mwanajeshi mwanasiasa. Kulikuwa na Jeshi la Kisiasa (Politicized Military).

Sasa, kwa muda wote huo tangu 1964 hadi 1992 hivi majeshi yetu yalikuwa part of the political fabric of our society. Hivyo, wanajeshi walikuwa na makamisaa wa kisiasa na walishiriki shughuli za kisiasa kama kawaida na waliwakilishwa kwenye vikao vya chama vya kisiasa kuanzia ngazi za chini kabisa hadi NEC. Mfumo wetu wa kijeshi ulikuwa unafanana sana na ule ulivyo China sasa hivi au hata CUBA na mtu aliweza kumove kwenda upande wowote bila tatizo lolote - mwanasiasa kwenda jeshini au mjeshi kwenda kwenye siasa.

Hili linaeleza nini?
Kwa kifupi ni kwamba:

a. Kikwete japo alikuwa ni afisa wa kisiasa jeshini, bado alikuwa pia ni mwanajeshi kwani hakukuwa na tofauti kati ya mwanasiasa mwanajeshi au mwanajeshi mwanataaluma. Alikuwa ni Afisa wa Jeshi, period. Ndio maana haitwi Luteni Kanali Mstaafu mwanasiasa Jakaya kikwete!

b. Kama mwanajeshi katika jeshi la kisiasa Kikwete alijua utaratibu wa kushughulikia manung'uniko ya pande zote mbili - yawe ya nature ya kisasa kama hili la Sayore au yawe kama ya kijeshi kwani yote mawili yalikuwa yanaweza kushughulikiwa ndani. Kwenye kambi yake pale Monduli kulikuwa na uongozi kamili wa kisiasa.

c. Jeshi lilikuwa kitu kinachoitwa "MKOA WA MAJESHI" kwa maneno mengine katika siasa za Tanzania Jeshi lilikuwa ni mkoa kamili wenye mfumo wa kisiasa kama wa mikoa mingine ya kijiografia. Kikwete alilijua hili. Suala la Sayore kuuza vitunguu na nyanya kwa jeshi lilitakiwa lifuate channel za mkoa wa majeshi. Guess nani alikuwa mwenyekiti wa Chama mkoa wa majeshi?

d. Nyerere alifahamu hiyo division na aliamua kuiacha ifuate mkondo wake kwani ultimately jambo zima kama lingeshindwa kushughulikiwa kimkoa, utaratibu wa rufaa za kichama ungefuatwa na jambo hilo lingeweza kushughulikiwa kichama au kijeshi. Kumbuka kuwa kusingekuwa na tofauti kati ya kushughulikiwa kijeshi au kichama kwani vyote vilikuwa ni pande mbili za kitu kile kile kimoja.

Ukishaelewa kuwa hakukuwa na hii tofauti unayoidhania utaona kwa wazi kosa la Kikwete lilikuwa wapi na kwanini Nyerere alikuwa sahihi kwa asilimia 100 alivyolishughulikia.

Big Up MM! Unajitahidi sana kutuelewesha, lakini it seems DSN hakuelewi wala hataki kuelewa kwani inaonyesha arguments zake zote zimejikita kwa anachokiamini. Ni shughuli nzito kumfafanulia jambo mtu anayesimamia anachokiamini, kuna watu hata ukeshe habadili msimamo wake. Ndio maana nashangaa kwanini bado mtu anang'ang'ania kwenye kutetea JK alijengewa hofu/uoga hadi hii leo. Kama hivyo ndivyo mtu asiyebadilika kutokana na athari za kisaikolojia hafai kuwa kiongozi maana atatupeleka kubaya! Kila mtu anatakiwa kuwa dynamic, JK should have taken the Monduli/Sayore saga as a challenge, challenges are always used as bricks to build our houses. Sio hadithi ya kuonewa au kujengewa hofu hadi hii leo!

habari kutoka kijiweni umeireeeemba ili ionekane ina ukweli fulani! chanzo cha habari yako ni cha kuaminika au kusadikika?

ya kikwete kama kiongozi yanafahamika

hapa la ajabu ni la nyerere,
hebu mjadili nyerere,alichokifanya kilikuwa sawa?

Naamini kabisa Mwl. baada ya kupata ujumbe ule, aliufanyia kazi na kugundua alichokiandika huyu mkuu. Na maamuzi yake yalilalia utafiti wake wa kujua ukweli na ndo maana alirudisha jeshini.

Kumbee! ndo maana enzi za mwalimu wakurwa, walinchoka, waachari, na wanakoo wengi wa Musoma ndio waliokuwa wanapokelewa kwa wingi jeshini...na yeyote aliyekuwa anawagusa walikuwa wanasulubiwa kwa namna moja ama nyingine...huwezi ikawa ni coincidence wakuu wengi wa jeshi enzi zake wote wawe wakura! Tutake tusitake Nyerere alikuwa ni binaadamu ambaye km walivyo wengine alikuwa na mapungufu lukuki..mengine ni very grave na yametujengea msingi wa udhariri wetu na maumivu ya ki-maisha tunayoyapata kila uchao.

Inamaana kama jinsi alivyokimbia Jeshini ndio vivyo hivyo anaendelea
kukimbia majukumu yake kwa Kusafiri kila siku.

Kuexpose Identity ya Jakaya Kikwete Kwa Makamanda wake wakati anajua kuwa yule ni junior,na kuwa alichofanya kama kijana ambae anafundishwa kuwa mjamaa anamuona Kiongozi katika style ile ya kimaisha nae anatumia wajibu wake wa kijamaa kupeleka taarifa kwa mkuu wa chama na ambae ndiye Rais wa Nchi.Kisha kiongozi huyo ambae ni Rais anaitoa taarifa hiyo kwa makamanda wake pasipo kuficha utambulisho [Identity] ya mtoa taarifa hakika kwa usalama wa mtoa taarifa ni kitendo kibaya na hatari.

Kupitia hayo na mengineyo ambayo hayajasemwa hapa kwa kuwa wenyewe bado wapo si vyema kuyasema muda ukifika watu pia watajua.Hakika kama binadamu mwingine yoyote ni hakika yalimpa historia ambayo leo watu wanalalamika juu ya utawala wake,lakini kupitia experince ya matukio hayo yamemshape hivi alivyo leo.Yamemtengeneza kuwa mwoga juu ya maamuzi.

ni kweli. Subconsciously jk ana woga. Ni tukio baya sana

Naamini kabisa Mwl. baada ya kupata ujumbe ule, aliufanyia kazi na kugundua alichokiandika huyu mkuu. Na maamuzi yake yalilalia utafiti wake wa kujua ukweli na ndo maana alirudisha jeshini.

Hivi Mkuu Lincorn azimio la Arusha hapa liko wapi wakati Mwalimu kwenye Kitabu chake cha Ujamaa page No17 anasema "Thes successful implementation of socialist objectives depends very much upon the ledaers,because socialism is a belief in a particular system of living,and it is difficult for leaders to promote its growth if they do not themselves accept it."

The peasants,the wage-earners, the students, the leaders, all of us-to make sure that this sociliast attitude of mind is not lost through the temptations to personal gain (or to the abuse of positions of authority ) which may come our way as individuals,or through the temptation to look on the good of the whole community as of secondary importance to the interests of the our own particular group.

Hiyo ni sauti ya Mwalimu kwenye Kitabu chake cha Ujamaa.Je ndio walivyotenda hata pale ilipobidi.

ni kweli. Subconsciously jk ana woga. Ni tukio baya sana

Vyema Mkuu kwa kuliona kupitia jicho la tatu,wengi hawaioni hiyo wanaangalia mabaya yake ya leo bila kuangalia chanzo cha hayo mabaya chaweza kuwa nini?

Ninachozungumzia hapa kuwa kijana kampa taarifa mkuu,mkuu bila kudisclosures Identity ya mtoa taarifa kawapa Makamanda wake wadeal na taarifa hiyo.Kivumbi cha mchakato mzima,leo mtendwa wa sakata ni Rais,baadhi tunalaumu kuwa amekuwa kimya na matukio kadha wa kadha nyeti,kiasi kuwa tunaona anayaona ya kawaida, lakini atumwangalii nae ndani ya moyo wake kama binadamu anafikra gani?

DSN unaonaje kama Kikwete angeeenda kupatiwa therapy ya kudeal with his unresolved psychological conflicts. Maana nakumbuka walipotupa taarifa zake za daktari walituambia kuwa alichunguzwa hata akili alionekana kuwa yuko fit.. so wewe unataka kutufanya tuanze kumshuku kwamba ana matatizo zaidi kichwani kuliko tunavyofikiria na hasa baada ya kukimbia kujitetea mbele ya wakubwa wake sasa amekuwa na woga fulani hata kama yeye ndio mkubwa mwenyewe.

Unafikiri psychotherapy inaweza kumsaidia kuresolve these deep seated issues?

Everybody is incharge of his destination! How could Nyerere cause unfinished problems to JK until today? Mbona Zakaria Hans Pope ni tajiri mkubwa sasa hivi wakati alikuwa majeruhi mkubwa wa mapinduzi yaliyoshindwa? Mbona na yeye hamlaani NyerereV wait a minute ni tatizo la Nyerere au kichwa cha individual?

Hakuna kumbukumbu bila source, Tafuta source then rudi jamvini tutajaribu kufikiria unachoandika, sio unabwabwaja kama bata tu, bwa! bwa! bwa!

hii ipo humu jamvini. Ni makala moja ndefu na isiyochosha kusoma

Kosa alilofanya Kikwete ni kukiuka hierarchy ya kijeshi. Hakupaswa kumwandikia Mwalimu. Angemwandikia mkuu wa jeshi halafu tatizo hilo lishughulikiwe katika ngazi hiyo. Unless uniambie kuwa jeshi halina taratibu zake kuwawezesha maafisa wa ngazi za chini kutoa malalamiko yao.

Ni kweli mkuu Kazi yoyote au shughuli yoyote ile haindi bila hierarchy (Ngazi), ukiwa junior staff kuna mkuu wa kitengo yeye yupo kwakukusaidia wewe, sasa kama utakwenda kwa Meneja moja kwa moja kuna haja gani ya kuwa na wakuu wa vitengo? alipaswa apeleke barua kwa mkuu wa nidhamu jeshini sio kwa Raisi, yaani amewaruka wote mpaka waziri wa ulinzi kamruka yaani hamuamini... Halafu mleta Hoja anatulazimisha tukubali matendo ya sasa ya JK eti ni kwasababu hiyo! JAMANI WATANZANIA WENZANGU TUMTAFAKARI SANA HUYU JK ANAPENDA SANA KUONEWA HURUMA.

DSN unaonaje kama Kikwete angeeenda kupatiwa therapy ya kudeal with his unresolved psychological conflicts. Maana nakumbuka walipotupa taarifa zake za daktari walituambia kuwa alichunguzwa hata akili alionekana kuwa yuko fit.. so wewe unataka kutufanya tuanze kumshuku kwamba ana matatizo zaidi kichwani kuliko tunavyofikiria na hasa baada ya kukimbia kujitetea mbele ya wakubwa wake sasa amekuwa na woga fulani hata kama yeye ndio mkubwa mwenyewe.

Unafikiri psychotherapy inaweza kumsaidia kuresolve these deep seated issues?

mkuu utapata picha gani ukiambiwa rais wako hazimo sawa? Kwani tulishawahi kuambiwa kuwa mkapa kalewa? Au kapigana na mkewe? Au wewe si mwanakijiji?

Back
Top Bottom