Baba wa Taifa akikemea kuhusu Udini/ Dini ndani ya Taifa letu la Tanzania

DENG XIAOPING

JF-Expert Member
Mar 6, 2022
2,398
2,593
- Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni kiongozi aliyepiga vita vikali kuhusu ubaguzi wa kidini au kikabila ndani ya taifa letu la Tanzania.

- Baba wa Taifa alihimiza siku zote za uhai wake pawepo mshikamano wenye umoja baina ya WATANZANIA ndani au nje ya Tanzania pasipo kubaguana kwa misingi yoyote ile iwe ukabila au udini

- Kwa kipindi Cha miaka ya hivi karibuni Taifa letu limekubwa na kasumba moja mbaya Sana kuhusu viongozi wanaoteuliwa.kwa watu[wananchi] kutazama zaidi kuhusu dini zao pasipo kutazama UTANZANIA wao waliokuwanao na sifa zao zilizowafanya wachaguliwe

- Ningependa kushauri kwa WATANZANIA wenzangu kutokutazama zaidi udini wa mtu katika teuzi za viongozi bali kuzama zaidi kuhusu sifa za kiongozi aliyetauliwa au kuchaguliwa.

- Ningependa kushauri pia kwa viongozi kuacha kasumba au kutokuwa na kasumba ya kuchagua watu kwa misingi ya dini zao bali wawachague kutokana na sifa zao zilizobora.

- Migogoro mingi ya kidini duniani uanza taratibu kwa vitu vidogo vidogo na mwisho uwa mikubwa zaidi na yenye madhara.

- Hii ni Tanzania ya watu wote wenye dini na wasio na dini.Wote wanastahili kutumikia serikali [ kuchaguliwa/ kuteuliwa]

Mwisho sikiliza kwa makini maneno ya baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akionya kwa ukali kuhusu udini ndani ya taifa letu la Tanzania. kwenye video fupi hapa chini

- Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa Ni kiongozi aliyepiga vita vikali kuhusu ubaguzi wa kidini au kikabila ndani ya taifa letu la Tanzania.

- Baba wa Taifa alihimiza siku zote za uhai wake pawepo mshikamano wenye umoja baina ya WATANZANIA ndani au nje ya Tanzania pasipo kubaguana kwa misingi yoyote ile iwe ukabila au udini

- Kwa kipindi Cha miaka ya hivi karibuni Taifa letu limekubwa na kasumba moja mbaya Sana kuhusu viongozi wanaoteuliwa.kwa watu[wananchi] kutazama zaidi kuhusu dini zao pasipo kutazama UTANZANIA wao waliokuwanao na sifa zao zilizowafanya wachaguliwe

- Ningependa kushauri kwa WATANZANIA wenzangu kutokutazama zaidi udini wa mtu katika teuzi za viongozi bali kuzama zaidi kuhusu sifa za kiongozi aliyetauliwa au kuchaguliwa.

- Ningependa kushauri pia kwa viongozi kuacha kasumba au kutokuwa na kasumba ya kuchagua watu kwa misingi ya dini zao bali wawachague kutokana na sifa zao zilizobora.

- Migogoro mingi ya kidini duniani uanza taratibu kwa vitu vidogo vidogo na mwisho uwa mikubwa zaidi na yenye madhara.

- Hii ni Tanzania ya watu wote wenye dini na wasio na dini.Wote wanastahili kutumikia serikali [ kuchaguliwa/ kuteuliwa]

Mwisho sikiliza kwa makini maneno ya baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akionya kwa ukali kuhusu udini ndani ya taifa letu la Tanzania. kwenye video fupi hapa chini

View attachment 2252711
Mjamaa...
Tatizo hili si jepesi kama unavyodhania.

Linataka ujuzi ndilo ulizungumze na linapendeza uwasikie wale walioathirika na udini na kujikuta kila mahali wao hawapo.

Hawa ndiyo wanaujua ukweli.
Ingependeza kama hawa wangepewa nafasi ya kulizungumza tatizo hili.

Nyerere hakupata kukumbwa na tatizo la udini katika maisha yake yote.

Mwalimu kapokelewa na Abdul Sykes 1952 na watu wa mwanzo waliokuwa karibu na yeye wote walikuwa Waislam na wanafahamika kwa majina yao wake kwa waume.

Kaishi na Waislam ndani ya nyumba zao.

Hakubaguliwa si kwa kabila yake wale dini yake.

Kaungwa mkono na wana mji wa Dar es Salaam na viongozi wa Waislam kama Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleman Takadir, Mshume Kiyate, Mohamed Jumbe Tambaza, Shariff Abdalah Omar Attas, Iddi Faiz Mafungo, Iddi Tosiri kwa kuwataja wachache.

Majimboni hali ilikuwa ni hii hii kama ilivyokuwa Dar es Salaam.

Lindi aliungwa mkono na Sheikh Mohamed Yusuf Badi na wenzake akina Suleiman Masudi Mnonji.

Tanga aliungwa mkono na Sheikh Abdallah Rashid Sembe na akina Hamisi Heri.

Huko kote Nyerere alishirikishwa katika dua ya kumuombea yeye Mungu na kuomba uhuru.

Nyerere hana historia ya kubaguliwa na Waislam.

Dhifa ya kumuaga safari ya kwanza UNO 1955 ilifanyika katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Nyerere kapata kupambana na tatizo la udini mara tatu.

Mara moja kabla ya uhuru mwaka wa 1958 pale aliposhambuiwa na Shekh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.

Mwaka wa 1963 Nyerere alipambana na Bi. Titi Mohamed katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya TANU.

Mwaka huo huo wa 1963 alipambana na Bilal Rehani Waikela katika mkutano wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) Mwalimu akiwa amealikwa kufunga mkutano huo.

Bahati mbaya haya yote hayako katka historia ya TANU na pengine kama nisingeyaleza yasingefahamika.

Sitaeleza katika hayo matukio matatu nini khasa lilikuwa tatizo kwa kuwa mosi kisa kinatisha na pili nashindwa kueleza kwa ajili ya staha.

Lakini matatizo yote hayo hapo juu nimeyaeleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Mwalimu hawezi kuwa mtu anaefaa kukemea udini kwa kuwa yeye ni sehemu ya historia hii.

Kwa ajili hii yeye hawezi kuwa hakimu wa hili tatizo.
Hili tatizo waachiwe wengine walisemee.

Ndugu yetu Mjamaa aliyefungua uzi huu anasema, ''Tusikilize kwa makini maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akionya kwa ukali kuhusu udini ndani ya taifa letu la Tanzania.''

Swali kubwa ni kuwa ikiwa hali ilikuwa hivi hapakuwa na udini wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika huu udini anaoukemea Mwalimu Nyerere umetokea wapi na nini sababu na chanzo chake?

1654552062777.jpeg

Julius Nyerere na Mshume Kiyate Februari 1964
 
.Sitaeleza katika hayo matukio matatu nini khasa lilikuwa tatizo kwa kuwa mosi kisa kinatisha na pili nashindwa kueleza kwa ajili ya staha.
Mkuu Maalim Mohamed Said asante sana kwa hili neno staha.
Mwalimu hawezi kuwa mtu anaefaa kukemea udini kwa kuwa yeye ni sehemu ya historia hii.
Mtu kuwa sehemu ya historia yoyote, hakumzuii kukemea mabaya ya historia hiyo, ndio maana wakati anaaga alikiri kufanya makosa na kusisitiza kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa.
Kwa ajili hii yeye hawezi kuwa hakimu wa hili tatizo.
Hili tatizo waachiwe wengine walisemee.
Hakuna popote amewahi kusemwa yeye ni hakimu, ila alibaini tatizo la udini, ukanda na Ukabila, sio tuu alikemea bali alifuta uchifu, akazifuta Jumuiya fulani fulani zenye extremity na fundamentalisms na kuunda Bakwata.
Ndugu yetu Mjamaa aliyefungua uzi huu anasema, ''Tusikilize kwa makini maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akionya kwa ukali kuhusu udini ndani ya taifa letu la Tanzania.''
Ni kweli Mwalimu Nyerere alikemea udini kwa kauli na matendo na kuna wadini aliwasweka ndani vipindi virefu.
Swali kubwa ni kuwa ikiwa hali ilikuwa hivi hapakuwa na udini wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika huu udini anaoukemea Mwalimu Nyerere umetokea wapi na nini sababu na chanzo chake?
Hili neno!.
P
 
- Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa Ni kiongozi aliyepiga vita vikali kuhusu ubaguzi wa kidini au kikabila ndani ya taifa letu la Tanzania...
Una historia ya kabla ya Nyerere ni nani walibaguliwa kidini na Mkoloni?

Unaijuwa vita ya majimaji kwanini ilipiganwa na wazalendo na walikuwa kina nani?

Unafahamu historia ya ujio wa Wareno hapa kwetu na walichokikuta na kukifanya?
 
Mjamaa...
Tatizo hili si jepesi kama unavyodhania.

Linataka ujuzi ndilo ulizungumze na linapendeza uwasikie wale walioathirika na udini na kujikuta kila mahali wao hawapo...
Unashangaza sana unaposema Nyerere hafai kuzungumzia udini, na wewe hapa unaleta "segregation" tayari, na mtu hawezi kuondoa tatizo kama bado analiendeleza bila kujielewa kama unavyofanya hapa licha ya ujuaji ulionao.

Nyie watu huwa siwaelewi na haya madai yenu ya udini, mnalalamika kila wakati kama vile hili taifa limekuwa likiongozwa na wakristu miaka yote, kumbe hata nyie mmeshapewa nafasi ya kuongoza na hakuna la maana mlilofanya kuondoa hiyo hali.

Matokeo yake mme develop inferiority complex kwenye vichwa vyenu, siku hizi mnateteana hata kama viongozi wa dini yenu wanafanya madudu mnakimbilia kusema wanalaumiwa kwasababu ya dini yao. Mnatumiwa na wenzenu bila nyie kujijua.

Huu ujinga unaongozwa na Zitto Kabwe, na msaidizi wake Fatma Karume nae anaropoka tu siku hizi, wala siwaoni mkiwakemea, wote mpo kimya mnawaangalia tu wenzenu katika imani.

Wanatetea matumbo yao kwa kujikinga kwenye mwamvuli wa dini yenu, naona hawa jamaa wanataka kuwafunga watu midomo wasikemee udhaifu wa serikali iliyopo madarakani, huu ni ujinga wa hali ya juu kabisa.

Hatuwezi kuacha rasilimali za taifa letu kuchezewa halafu tusihoji kisa mkiulizwa mtasema mnaulizwa kwa sababu ya dini ya viongozi waliopo!.msidumaze wengine akili kwa sababu nyie mmekubali kudumaza akili zenu kwa haya madai yenu ya kila siku.

Nakuona kila siku unakuja na utetezi wako kwamba Nyerere alipofika Dsm alipokewa na waislamu, kwani ajabu ni ipi hapo? waislamu sio sehemu ya jamii ya watanzania? au nyie waislamu mnajiona special sana zaidi ya wengine hivyo kuhitaji special treatment?

Wacha hizi hoja zako za kitoto, Tanzania ni taifa la watu wenye dini na wasio na dini, wote tunachangamana huko barabarani kila siku kwenye shughuli zetu, na hakuna ajabu yoyote ya watu wa dini tofauti kukutana kwenye harakati zao, labda uwe na lako la siri.
 
Una historia ya kabla ya Nyerere ni nani walibaguliwa kidini na Mkoloni?

Unaijuwa vita ya majimaji kwanini ilipiganwa na wazalendo na walikuwa kina nani?

Unafahamu historia ya ujio wa Wareno hapa kwetu na walichokikuta na kukifanya?
Jambo la muhimu ni kuwa mada yangu imejikita zaidi juu ya kauli ya Mwalimu kukemea kuhusu udini na hiyo ili kuwa baada ya kupata Uhuru kuhusu kabla ya uhuru mwalimu hukuwa na mamlaka yoyote wakati huo
 
Unashangaza sana unaposema Nyerere hafai kuzungumzia udini, na wewe hapa unaleta "segregation" tayari, na mtu hawezi kuondoa tatizo kama bado analiendeleza bila kujielewa kama unavyofanya hapa licha ya ujuaji ulionao.

Nyie watu huwa siwaelewi na haya madai yenu ya udini, mnalalamika kila wakati kama vile hili taifa limekuwa likiongozwa na wakristu miaka yote, kumbe hata nyie mmeshapewa nafasi ya kuongoza na hakuna la maana mlilofanya kuondoa hiyo hali.

Matokeo yake mme develop inferiority complex kwenye vichwa vyenu, siku hizi mnateteana hata kama viongozi wa dini yenu wanafanya madudu mnakimbilia kusema wanalaumiwa kwasababu ya dini yao. Mnatumiwa na wenzenu bila nyie kujijua.

Huu ujinga unaongozwa na Zitto Kabwe, na siwaoni mkimkemea, wote mpo kimya mnamuangalia tu; anatetea tumbo lake kwa kujikinga kwenye mwamvuli wa dini yenu, huyu jamaa anataka kuwafunga watu midomo wasikemee mabaya yanayolikumba taifa, huu ni ujinga wa hali ya juu kabisa.

Hatuwezi kuacha rasilimali za taifa letu kuchezewa halafu tusihoji kisa mkiulizwa mtasema mnaulizwa kwa sababu ya dini ya viongozi waliopo!.msidumaze wengine akili kwa sababu nyie mmekubali kudumaza akili zenu kwa haya madai yenu ya kila siku.

Nakuona kila siku unakuja na utetezi wako kwamba Nyerere alipofika Dsm alipokewa na waislamu, kwani ajabu ni ipi hapo? waislamu sio sehemu ya jamii ya watanzania? au nyie waislamu mnajiona special sana zaidi ya wengine?

Wacha hizi hoja zako za kitoto, Tanzania ni taifa la watu wenye dini na wasio na dini, wote tunachangamana huko barabarani kila siku kwenye shughuli zetu, na hakuna ajabu yoyote ya watu wa dini tofauti kukutana kwenye harakati zao, labda uwe na lako la siri.
Maelezo mazuri 👍
 
- Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni kiongozi aliyepiga vita vikali kuhusu ubaguzi wa kidini au kikabila ndani ya taifa letu la Tanzania.

- Baba wa Taifa alihimiza siku zote za uhai wake pawepo mshikamano wenye umoja baina ya WATANZANIA ndani au nje ya Tanzania pasipo kubaguana kwa misingi yoyote ile iwe ukabila au udini

- Kwa kipindi Cha miaka ya hivi karibuni Taifa letu limekubwa na kasumba moja mbaya Sana kuhusu viongozi wanaoteuliwa.kwa watu[wananchi] kutazama zaidi kuhusu dini zao pasipo kutazama UTANZANIA wao waliokuwanao na sifa zao zilizowafanya wachaguliwe

- Ningependa kushauri kwa WATANZANIA wenzangu kutokutazama zaidi udini wa mtu katika teuzi za viongozi bali kuzama zaidi kuhusu sifa za kiongozi aliyetauliwa au kuchaguliwa.

- Ningependa kushauri pia kwa viongozi kuacha kasumba au kutokuwa na kasumba ya kuchagua watu kwa misingi ya dini zao bali wawachague kutokana na sifa zao zilizobora.

- Migogoro mingi ya kidini duniani uanza taratibu kwa vitu vidogo vidogo na mwisho uwa mikubwa zaidi na yenye madhara.

- Hii ni Tanzania ya watu wote wenye dini na wasio na dini.Wote wanastahili kutumikia serikali [ kuchaguliwa/ kuteuliwa]

Mwisho sikiliza kwa makini maneno ya baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akionya kwa ukali kuhusu udini ndani ya taifa letu la Tanzania. kwenye video fupi hapa chini

View attachment 2252711
Anza na Zanzibar kwanza, hakuna Waziri Mkristo hata wa dawa
 
Mkuu Maalim Mohamed Said asante sana kwa hili neno staha.

Mtu kuwa sehemu ya historia yoyote, hakumzuii kukemea mabaya ya historia hiyo, ndio maana wakati anaaga alikiri kufanya makosa na kusisitiza kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa.

Hakuna popote amewahi kusemwa yeye ni hakimu, ila alibaini tatizo la udini, ukanda na Ukabila, sio tuu alikemea bali alifuta uchifu, akazifuta Jumuiya fulani fulani zenye extremity na fundamentalisms na kuunda Bakwata.

Ni kweli Mwalimu Nyerere alikemea udini kwa kauli na matendo na kuna wadini aliwasweka ndani vipindi virefu.

Hili neno!.
P
N
Anhaa, ni vyema umelifahamu hilo, kuwa Mwalimu hakuwa na mamlaka "yoyote", unawafahamu waliokuwa na mamlaka kisiasa kabla ya uhuru? Soma; Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa
Ndugu mbona unirudisha kabla ya Uhuru wakati andiko langu limejikita kumzungumzia mwalimu baada ya Uhuru na kauli zake za kupiga Vita udini Mimi hayo ya kabla ya Uhuru hayana nafasi Sana Ila baada ya Uhuru ndio Jambo la msingi kwa kuwa Sasa hatuishi kabla ya Uhuru bali tunaishi baada ya uhuru
 
Anza na Zanzibar kwanza, hakuna Waziri Mkristo hata wa dawa
Kama wameteuliwa kwa misingi ya kidini si Jambo la busara Ila Kama wateuliwa kutokana na sifa zao zilizo Safi/ bora basi hakuna shida hata Kama ni waislamu kwa kuwa ni wazinzibar Basi wanahaki kuteuliwa
 
Back
Top Bottom