Baba wa Demokrasia Tanzania, Ali Hassan Mwinyi na Cabinet Meeting iliyochukua Dakika 3 - Machi 1990

alijitahid sana kubalance kebinet yake sana ukizingatia ni upande hole mwengine
 
He later explained that the reason was to fight corruption, which was rampant in all ministries and because of the lack of accountabilty.

See a phrase in purple; how come you find an entire cabinet is corrupt then you re-appoint a large proportion of those who were in the previous cabinet?
 
Asante sana kwa kumbukumbu nzuri. Nalikumbuka sana hili gazeti, bahati mbaya sikutunza nakala yangu. Wakati huo nilikuwa mwalimu pale Moshi mjini na nilikuwa na desturi ya kununua magazeti pale posta.
Hiyo cabinet mpya ilidumu hadi October 1990 ulipofanyika uchaguzi mkuu mwingine, enzi hizo kura ya urais bado ilikuwa ya 'Ndiyo' au 'Hapana'. Mbunge wa Moshi mjini wakati huo Brig Gen Muhiddin Kimario alishindwa na kijana mdogo wa chuo cha Mzumbe kwa msaada mkubwa wa mtandao ulioitwa wakati ule MUWATA (Muungano wa Wanavyuo Tanzania, hii ndio ilikuwa serikali ya wanafunzi kwenye vyuo vyote nchini). Kijana huyo John Peter Mwanga alidumu kwenye ubunge kwa muhula mmoja tu, akasombwa na kimbunga cha NCCR ya Mrema 1995.
Baada ya uchaguzi wa 1990 Dr John Samuel Malecela aliteuliwa kuwa waziri mkuu lakini changamoto za rushwa ziliendelea, au naweza kusema zilizidi, hasa katika sekta ya ardhi na maliasili. Mtakumbuka kipindi hicho ndipo ilipotokea ile kashfa ya Loliondo ambayo marehemu Stan Katabaro aliiripoti sana kwenye gazeti lake la Mfanyakazi. Baadaye watu wakapiga hela kwenye mkutano wa masuala ya Mazingira kule Brazil, Mfanyakazi likaripoti, Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Ahmed Hassan Diria (marehemu) akakanusha kesho yake, lakini siku iliyofuata Mfanyakazi likaweka front page nakala za barua na baadhi ya hati za malipo zilizotumika, ukimya ukatawala!

Kwa ujumla tumetoka mbali sana kuhusu haya mambo ya rushwa. Yapo mengi ya kujifunza kutoka kwenye historia hiyo ambayo yakitumiwa vizuri tutasonga mbele kimafanikio.
Mkuu, nimefarijika na analysis/maoni yako...hakika utu uzima dawa. Ubarikiwe popote ulipo mkuu! umenikumbusha gazeti la mfanyakazi na Mzalendo bila kusahau majira. Katika sekta ya habari, nchi hii imetoka mbali sana...
Kwenye sakata la Loliondo, aliyekuwa mkurugenzi wa hifadhi alikuwa muhidin Ndolanga, mwenyekiti wa zamani wa FAT (Football association of Tanzania) na alikuwa na ukaribu na mzee Mwinyi. baada ya lile sakata, ndolanga alitolewa kwenye nafasi hiyo lakini hakushitakiwa wala kuchukuliwa hatua.
 
Mwinyi aliyafanya haya kwa shinikizo la JK Nyerere.. Ambae alikua mkosoaji mkuu wa serikali yake
Alifanya kwa pressure ya vitu vingi! Wakati ule chama kilikuwa cham hakina unafiki wala kulikuwa hakuna pesa z kupiga kwenye chama ni mapenzi dhati ya chama chao!! Sio sasa wapiga deal wamejaa chamani!! Pressure vyombo vya usalama na JKN mwenyewe pia!!
 
Kama kuna mtu ana zile nakala za Loliondo gate aje azilete hapa kwa faida ya kizazi cha sasa waelewe wapi tumetoka! RiP Stan Katabalo yule Mzee Mungu amrehemu! Alipambana vita akiwa pekeyake na kalamu yake! Wakampofoa abanaaa!! Watu wabaya sanaaa.....Marehemu Mgumia na Kina Ndolanga!!!
Mkuu, nimefarijika na analysis/maoni yako...hakika utu uzima dawa. Ubarikiwe popote ulipo mkuu! umenikumbusha gazeti la mfanyakazi na Mzalendo bila kusahau majira. Katika sekta ya habari, nchi hii imetoka mbali sana...
Kwenye sakata la Loliondo, aliyekuwa mkurugenzi wa hifadhi alikuwa muhidin Ndolanga, mwenyekiti wa zamani wa FAT (Football association of Tanzania) na alikuwa na ukaribu na mzee Mwinyi. baada ya lile sakata, ndolanga alitolewa kwenye nafasi hiyo lakini hakushitakiwa wala kuchukuliwa hatua.
 
Kama kuna mtu ana zile nakala za Loliondo gate aje azilete hapa kwa faida ya kizazi cha sasa waelewe wapi tumetoka! RiP Stan Katabalo yule Mzee Mungu amrehemu! Alipambana vita akiwa pekeyake na kalamu yake! Wakampofoa abanaaa!! Watu wabaya sanaaa.....Marehemu Mgumia na Kina Ndolanga!!!
Daah! Mwenyezi Mungu amrehemu stan Katabalo...alikuwa mwandishi shupavu asiyeteteleka na kwa kipindi akiliandikia gazeti la Uchunguzi la Mfanyakazi miaka ya 1992/93. Aliandika kuhusu kashfa ya Loliondo (Loliondo Gate) na ilipelekea kuwindwa hadi kifo chake! kuna makala zake zilianzishwa na wadau humu JF, nime-attach link hapo chini
Loliondo: The disturbing connection and secrets
Stan Katabalo: Tunauhitaji mzimu wako wa habari za Uchunguzi!
 
Mzee Ben na JK wote walipitia Foreign affairs kabla ya kuwa maraisi. Huoni kama hiyo ingemsaigia Mkuu wa sasa kupata exposure, kama na yeye angepitia huko??

Ile Confidence ya kuhutubia mikutaano ya kimataifa, ku negotiate mikopo ya nje etc.
 
Back
Top Bottom