Pascal Ndege
JF-Expert Member
- Nov 24, 2012
- 2,977
- 1,897
Yesu Kristo alijinyenyekeza akatii mpaka mauti. Ndio somo la kila siku ambalo tunajifunza katika biblia. Yesu Kristo hakuwa na hatia alipobebeshwa msalaba na wale wayahudi. Nadhani kwa hili la kupinga kustaafishwa mimi sipo upande wa Baba askofu. Kwasababu kwa hili la tuhumu tu linatosha kabisa kuishi maisha ya kitakatifu.
Tumekuwa wagumu sana duniani. Maisha ya kiroho yamekuwa kama ya kisiasa. Watu wanachukulia Uchungaji ni sawa na madaraka ya kijamii. Si hapo tu hata ile saba mara sabini ni kama haipo. Wachungaji hawasamehani wala hawasamehi na wala hawaionei haya biblia.
Hata ile sala baba yetu watu wanasali kama wimbo wa taarabu. Ugomvi huu haugusi tu maisha ya waanglikana pekee bali wakristo na waamini wote kwa ujumla. Hasa pale tunapokuja kutathimini ukristo wetu na matayalisho yetu ya hapa duniani ya kurudi mbinguni kwa baba yetu juu mbinguni.
Nimeumia na kusikitika maana Mavuno ni mengi na wavunaji wamesahau kuvuna na kuanza kupanda magugu kwenye shamba la bwana.