IsayaMwita
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 1,127
- 140
Hebu wewe Kikwete umemsahau rafiki yako mwalimu Nyerere, kipenzi chako, mshauri wako wa karibu hata Mizengo Pinda anajua, Ulipenda kumuuliza ushauri pale ulipotatizika, haukusita kumsikiliza siku zote
Unakumbuka pale Chimwaga alipokwambia usubiri umwachie Mkapa, na wewe ukaonyesha moyo wa upendo kwa kipenzi chako kuwa wewe ni msikivu japo ulikuwa kipenzi cha watanzania na tulikuhitaji uiongoze nchi kwa siku zile(1995).
Baba kikwete sasa naona umeanza kusahau usia wa rafiki yako mwalimu , yeye alikuwa anawasikiliza wananchi siku zote wanataka nini, na kweli alijitahidi pale alipoweza kuwaridhisha, sisi watanzania tumekuambia kuwa wakamate mafisadi wote wewe unawatetea, kibaya zaidi wewe uliyetuambia mafisadi watashughulikiwa sasa tunaona siku zinakwenda, hakuna linaloendelea.
Mzee Kikwete tuambie kule kwa baba wa taifa (Butiama)mlifuata nini ? Mbona hamukutekeleza hata moja yale mliyokusudia ? Lile la Zanzibari mmelifanya liwe kitendawili, wenye kukitegua ni ninyi wenyewe.
Kikwete wewe wajua uchumi wetu unavyoporomoka kila kukicha, maisha ya watanzania yakiendelea kuwa mabaya nani wa kuwaokoa na moto huu, ninyi ni mashaidi kuwa watanzania ni wavumilivu, ama ni kwa kuwa wewe na jamaa zako mna neema za kutosha ?
Nilidhani watasubutu, watawasaliti na kuwazodoa hao nasaba wao. Lakini mambo yamezidi unga, kila wakiruka wanakanyaga humo humo, mtawezaje kuizamisha boti mliyoipanda ninyi wewe ? Akili zenu sasa zinawaza 2010 ni jinsi gani mtashinda kwa kishindo, Mungu awahurumie sana. Najua mnatufanya mtakavyo kwa sasa ila wakati utawahukumu tu.
Mwalimu Nyerere Uko wapi baba hawa wanao wakubwa wametusaliti, watanzania tunakukumbuka,uko wapi baba ? baba wewe ulitupenda sote, haukuwa na ubaguzi kilichokuwepo ulitugawia kwa uwiano sawa, baba njoo uone hata huyu mwanao uliyempenda sana(Kikwete) naye kaziba masikio, kila kukicha anatuambia maisha bora kwa kila mtanzania.
Baba wamekuja hapo Butiama, tukadhani wamekuja kukuomba msamaha kwa haya wanayotufanyia, kumbe wamekuja kukudharirisha na ndiyo maana wale wenye akili kama vile Mzee Mwinyi, Sumaye Mwanao Mkapa na wengine wengi hawakudiriki kusogea hapo ulipo lala baba.
Baba kilio chetu tunakielekeza kwako baba, usikie hapo ulipolala, wewe ndiye uliyetuchagulia watu hawa, watokee hata kwenye njonzi, waambie watutumikie vema ili tusije tukachukua uta na mishale yetu tukaanza kuwawinda kama nyani msituni,waambie wewe haukuwa hivyo, na kama ungekuwa hivyo basi vyote wanavyouza kwa sasa wasingevipata hivi leo ?
Baba tunajua haukuwa malaika hata wewe ulikosea lakini ulikubali kukosolewa, mwalimu ulijaa mioyoni mwa watanzania, tulipokosea wewe ulitukosoa,baba upendo wako ulikuwa kama mshumaa, Afrika kusini wanajua, Msumbiji wanajua, baba !! baba !! Mwalimu uko wapi baba ?
mwana wa Mwita nimesema.[/B]