Baba tulikupenda lakini Mungu alikupenda zaidi

CharmingLady

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
18,250
12,868
Ni miaka kumi na mitano (15) imepita tangu baba yetu mpendwa ututoke duniani. ilikuwa siku ya majonzi,huzuni na siku niliyopatwa uchungu ambao sijawahi upata tena. Tunakukumbuka kwa busara,hekima na upendo tulioupata toka kwako. lakini ulizimika kama mshumaa wakati wa upepo.
unakumbukwa sana na mama yetu mpendwa, watoto, wajukuu, ndugu jamaa na marafiki.
BWANA ALITOA, BWANA ALITWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE!!!!!!
 
Ooh!b charminglady pole sana wangu! Mwenyezi Mungu azidi kuwapa hekima na uvumilivu kila mnapo mkumbuka baba yetu kipenzi.

Kila jema na lenye kheri lisikuponyoke na endeleeni kuya enzi yale mema baba kipenzi aliyo yaacha.
 
asante sana Mohamedi Mtoi, daima twamkumbuka kwa upendo wake uliotuunganisha wanae mpaka sasa tuna upendo baina yetu!
 
Last edited by a moderator:
wakati unakumbuka kifo cha baba,CL kumbukeni yale mema yote aliyokutendeeni,mafunzo aliyokupeni,njia aliyokuonyesheni,upendo wake viwe dira kwako na kwa nduguzo wote.
RIP baba.
 
pole shosti charminglady kwa sad memory,bwana alitoa na akatwaa jina lake lihimidiwe!
 
Last edited by a moderator:
Pole shosti angu.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa.
Jina lake Lihimidiwe.
 
wakati unakumbuka kifo cha baba,CL kumbukeni yale mema yote aliyokutendeeni,mafunzo aliyokupeni,njia aliyokuonyesheni,upendo wake viwe dira kwako na kwa nduguzo wote.
RIP baba.

asante Bishanga, tunajitahidi kuyaenzi yote mema alotuachia!
 
to loose a parent ni tough moment kwa kila mtu...since my dad passed away ni exactly miaka 15 kama ilivyo kwako charminglady,i was still so as my bros n sis, we had no where to run.
Lakini ashukuriwe Mungu wa mbinguni aliyesimama kuwa baba tangu wakati huo hata sasa...
Urithi pekee aliouacha baba yetu kwetu ni elimu kiduchu ambayo ilikuwa chachu ya elimu nyingi niliyonayo hata sasa...
Mtakumbukwa daima mababa wote mliotangulia mbele za haki...tupo pamoja charminglady.
 
Ni miaka kumi na mitano (15) imepita tangu baba yetu mpendwa ututoke duniani. ilikuwa siku ya majonzi,huzuni na siku niliyopatwa uchungu ambao sijawahi upata tena. Tunakukumbuka kwa busara,hekima na upendo tulioupata toka kwako. lakini ulizimika kama mshumaa wakati wa upepo.
unakumbukwa sana na mama yetu mpendwa, watoto, wajukuu, ndugu jamaa na marafiki.
BWANA ALITOA, BWANA ALITWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE!!!!!!

Pole CL. . .RIP baba yetu. . .
 
Inawauma kwa sababu kuna vitu vizuri alivyokua akiwanfanyia,iwe ushauri,makanyo,iwe kuwapa direction na mambo mengiine mengi,cha msingi ni kuyafuata na kuyaenzi aliyoya'impart kwenye maisha yenu.....
R.I.P DAD.......Pole sana mamaa charminglady
 
Last edited by a moderator:
Ni miaka kumi na mitano (15) imepita tangu baba yetu mpendwa ututoke duniani. ilikuwa siku ya majonzi,huzuni na siku niliyopatwa uchungu ambao sijawahi upata tena. Tunakukumbuka kwa busara,hekima na upendo tulioupata toka kwako. lakini ulizimika kama mshumaa wakati wa upepo.
unakumbukwa sana na mama yetu mpendwa, watoto, wajukuu, ndugu jamaa na marafiki.
BWANA ALITOA, BWANA ALITWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE!!!!!!

Mungu azidi kuwalinda,kuwatunza,kuwajali,kuwabariki na Pengo lizibwe na Muumba wa dunia hii....

Mzidi kubarikiwa katika makapu yenu ya unga,mbarikiwe kwenye mifuko yenu itunzayo hela,vyupa mafuta yenu visikauke..

Upendo utawale ndani ya nyumba yako na wengine pia.
Shemeji.
 
Pole sana mkuu. Muenzi kwa kutenda mema yote aliyokufundisha na kujitunza na kuwaheshimu watu wote. mia
 
asanteni wadau wote, pamoja na kumkumbuka pia ni changamoto kwetu sote tulio hai je tumejiandaaje?
 
Back
Top Bottom