Baba tafuta muda uwe unakaa na mtoto/watoto wako

6321

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
649
1,116
Mawasalimu kwa jina la JMT.

Nalishuhudia hili jambo. Kumbuka ewe baba umri unaenda itafika kipindi hauna nguvu za kufanya kazi, utakuwa umestaafu na utakuta haukujenga ukaribu na wanao. Watoto ni faraja ya uzeeni kaa nae vizuri.

Tunajua Majukumu ya baba ni kutafuta riziki ya familia lakin kwenye swala la kutafuta angalau kila siku ukae na watoto wako upige nao story n jambo la manufaa kwa baadae. Wanawake/wake zenu wanachukua point nyingi sana kwa watoto, mama anachukua pesa kwa baba anamkidhi mahitaji ya watoto, hawa watoto kwenye ukuaji wao wanaamin mama ndio kila kitu kuhusu Wao.

Mbaya zaid Mama akiwa anatatua mahitaji ya watoto hawez kutatua hiv hivi, kuna maneno atayaongea tu ambayo maneno hayo yatamfanya baba aonekane sio kitu, lakin kwa uhalisia sio kweli.

Nb. Hawa wanawake wanapandikiza chuki sana kwa watoto juu ya baba yao, Ishi nao vizuri. Kuna tofauti ya kudekeza na kuishi nao vizuri watoto.

Mwandiko sio maridadi ila ujumbe ufike kwa wanaume wote.
 
Mawasalimu kwa jina la JMT.

Nalishuhudia hili jambo. Kumbuka ewe baba umri unaenda itafika kipindi hauna nguvu za kufanya kazi, utakuwa umestaafu na utakuta haukujenga ukaribu na wanao. Watoto ni faraja ya uzeeni kaa nae vizuri.
Ridhiki=riziki/rizk
 
Ninachofahamu ni kwamba kuna matunzo na malezi; akina baba wengi wanaamini kuwa waki provide material thing inatosha kuwa wamekuwa wamefanya malezi which is not true, unaeza ukaprovide kila kitu lkn kama hupati wasaa wa kuonesha na kufanya malezi juu ya watoto ni bure kwa maana ya kumaintain ioe bonds kama mzazi.

Ukaribu wa mtoto na mama ni thru malezi wala si vinginevyo, mfano mtoto anakuwa na true sense of feeling kwa vile mama anavyompa maziwa, chakula, kubembeleza mtoto kutoka katika bad bad to good mood, katika hvy tunachoshindwa biologically ni kuwanyonyesha watoti lkn vyote tunaweza ikiwa tutadhamiria kufanya hvy!

Ni jukumu letu wababa kushiriki pia kwenye malezi than matunzo ambayo tunadhani kwa kufanya hvyo inatosha.
 
Kutafuta fadhila ya mwanao huo ni utumwa na kujipendekeza

Mwanaume hajaumbwa hivo hizo ni tabia za kimama

We mpe misingi Bora na malezi stahiki yanayofaa inatosha, akupende asikupende hiyo haijalishi na Kama ni mwanao wa damu maji yatafata MKONDO wake
 
Nilitaka kuchangia hivi hivi, umenisemea.
 
Back
Top Bottom