minded tips
JF-Expert Member
- Apr 29, 2018
- 475
- 847
ndugu umeandika kitu kizuri kweli ila kwanini bado unaweka uoga uoga?Professor Kabudi kanywaje dawa isiyothibitishwa,?
Poleni watanzania... Poleni sana wananchi wanyonge wa mwili imara wa roho na thabiti wa ufahamu
Dawa ya Corona iliyofuatwa haraka haraka kwa ndege maalum ya mkuu wa nchi haiwezi kutumika hadi baada ya utafiti utakaochukua takriban siku 180.. Hii sio dawa ya maabara ni dawa ya asili.. Tuwe watulivu tutajulishana aina ya kipimo kitakachotumika kuthibitishwa ubora wake na kama haina side effects.. Hapa TBS na TMDA (TFDA) pengine hazirahusika...
Prof Kabudi anatuchanganya.. Tena sana.. Kwanini sasa asingeagiza kiasi kidogo kwanza kwa ajili ya sampling na kuthibitishwa ndio tutume lidege letu kuleta mzigo wa kutosha?
Nadhani muda utasema lakini naona kuna jambo si la kawaida sana hapa.. Kuna mkanganyiko mkubwa kwenye hili.. Kimamlaka na maamuzi.. Kuna hofu ya wazi pengine hiyo dawa ina madhara makubwa kiafya ama la haina uwezo wa kutibu Corona
Ni muhimu pia kujikumbusha alichosema Waziri wa afya huko inakotoka dawa.. Yeye alisema ile dawa ni kwa ajili ya kinga na si kwa ajili ya tiba kwa waliokwisha ambukizwa.. Ila ndio hivyo tena tumeshaulipia mzigo ambao hatutautumia hadi siku 180 zipite.
Baba nifundishe kuukabili uhalisia nisiukimbie ukweli.. Wahenga walituasa: kwa mwoga kulienda kicheko kwa shujaa kulienda kilio.
Hofu ni adui number moja kwenye kuukimbia ukweli.. Lakini hofu ni silaha number moja kwenye kuukabili uhalisia... Hofu na mashaka huleta mbinu na tahadhari. Ujasiri huleta majigambo na kutojali
Tusitoane hofu katikati ya hatari kubwa.. Tusifiche uhalisia kwa kufutika uvundo kibindoni.. Tuambiane ukweli.. Tutaokoa maisha mengi
Tukiwatoa watu hofu huku sisi tumefichama tunatengeneza tatizo kubwa zaidi.. Wananchi wanakuwa sio makini tena na tahadhari inakuwa ndogo.
Tumepigwa tena kwenye dawa isiyothibitishwa na ambayo hatutaweza kuitumia kwa miezi sita
Mungu wabariki waja wako.. Na watesi wa wana wako... Wabariki pia
Jr
Sent using Jamii Forums mobile app