Baba nifundishe kuukabili uhalisia.. Nisiukimbie ukweli

minded tips

Senior Member
Apr 29, 2018
169
500
Professor Kabudi kanywaje dawa isiyothibitishwa,?
Poleni watanzania... Poleni sana wananchi wanyonge wa mwili imara wa roho na thabiti wa ufahamu
Dawa ya Corona iliyofuatwa haraka haraka kwa ndege maalum ya mkuu wa nchi haiwezi kutumika hadi baada ya utafiti utakaochukua takriban siku 180.. Hii sio dawa ya maabara ni dawa ya asili.. Tuwe watulivu tutajulishana aina ya kipimo kitakachotumika kuthibitishwa ubora wake na kama haina side effects.. Hapa TBS na TMDA (TFDA) pengine hazirahusika...

Prof Kabudi anatuchanganya.. Tena sana.. Kwanini sasa asingeagiza kiasi kidogo kwanza kwa ajili ya sampling na kuthibitishwa ndio tutume lidege letu kuleta mzigo wa kutosha?

Nadhani muda utasema lakini naona kuna jambo si la kawaida sana hapa.. Kuna mkanganyiko mkubwa kwenye hili.. Kimamlaka na maamuzi.. Kuna hofu ya wazi pengine hiyo dawa ina madhara makubwa kiafya ama la haina uwezo wa kutibu Corona

Ni muhimu pia kujikumbusha alichosema Waziri wa afya huko inakotoka dawa.. Yeye alisema ile dawa ni kwa ajili ya kinga na si kwa ajili ya tiba kwa waliokwisha ambukizwa.. Ila ndio hivyo tena tumeshaulipia mzigo ambao hatutautumia hadi siku 180 zipite.

Baba nifundishe kuukabili uhalisia nisiukimbie ukweli.. Wahenga walituasa: kwa mwoga kulienda kicheko kwa shujaa kulienda kilio.

Hofu ni adui number moja kwenye kuukimbia ukweli.. Lakini hofu ni silaha number moja kwenye kuukabili uhalisia... Hofu na mashaka huleta mbinu na tahadhari. Ujasiri huleta majigambo na kutojali

Tusitoane hofu katikati ya hatari kubwa.. Tusifiche uhalisia kwa kufutika uvundo kibindoni.. Tuambiane ukweli.. Tutaokoa maisha mengi

Tukiwatoa watu hofu huku sisi tumefichama tunatengeneza tatizo kubwa zaidi.. Wananchi wanakuwa sio makini tena na tahadhari inakuwa ndogo.

Tumepigwa tena kwenye dawa isiyothibitishwa na ambayo hatutaweza kuitumia kwa miezi sita

Mungu wabariki waja wako.. Na watesi wa wana wako... Wabariki pia

Jr
ndugu umeandika kitu kizuri kweli ila kwanini bado unaweka uoga uoga?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

lamalu

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
478
500
Kazi yako ww ni kupotosha watu dhidi ya hatua ambazo serekali inachukua
ukibandika andiko lolote la kupotosha hapo utanikuta nitakujibu. Hii staili yako ya kuponda kwa lengo la kutafuta attention punguza bro hujui kitu ww!!!
Ww ni mkurupukaji hakuna asiyekujua humu unajipenyeza kwenye kila habari inayo trend lazima ubandike upupu
Tiba mbadala zote mchakato wake ni tofauti..serekali haiwezi kuingia kichwa kichwa inachukua hizo tiba mbadala kwa ajili ya public consumption ya wananchi wake kabla ya ku test
Proff Kabudi kaonyesha uzalendo wa hali ya juu kitendo cha yy kunywa dawa kabla ya mtz yy ameonyesha imani kwenye dawa.....
pili hata kama dawa itakuwa na madhara basi ianze kumdhuru yy kabla ya mtanzania yyte yule
kuna misukule mingi isiyojielewa unaikamata humu na upupu wako,.......
eti unazungumza gharama ya kurusha ndege!!!?
kuna gharama ipi dhidi ya uhai wa watz.....
nyie ndio vimbelembele mnapiga kelele raisi afanyi kazi!!??
jitihada zinafanyika za wazi unapiga kelele eti gharama ya ndege!!?punguza GILIBA punguza upotoshaji wenye akili wameona wameelewa.
Na wenye akili pia wamekuona una akili gani!! Hahahaha yaani junior hapa nimemwambia kuna GT anasema eti pro alikunywa ile sample ili kama ina madhara afe yeye kwanza, kacheka kaniomba niimfanyie mpango ajiunge jf kwan na yeye pia atakuwa ni GT

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nyamizi

Platinum Member
Feb 19, 2009
1,657
2,000
Demokrasia ni pamoja na kukubali kukosolewa...
ww ni mfupi kwa akili hilo limethibitika.....
mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu..!!
sehemu yyte nitakoyokuta umepotosha nitakutandika......
tek that to your wallet...stpd man
Imebidi nicheke tu,unatumia nguvu kubwa sana kuexpose Incompetence yako ktk kujenga hoja!
 

Graph

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
2,751
2,000
Leo angalau umeongea la maana, kumbe ukiacha mambo ya uchawi una akili 😂.
Huyu jiwe kajaa ego sana ndicho kinachomsumbua, anajiona smart dunia nzima, kwa hiyo hasikilizi chochote anaamini anachoamini ndicho sahihi na hakuna wa kumwambia chochote. Hiyo ndiyo shida yake tu
 

Salange

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
683
1,000
Umewaza kama mimi. Iweje tutumie gharama kuuubwa kiasi kile (mafuta yaliyotumika, posho za wasafiri na cabin crew na posho zao, gharama za chakula na malazi) kwenda kufuata chupa mbili zenye ujazo wa 500mls@. Yaani tukashindwa hata kupiga simu tu kuwaambia "wazee, tunaomba mtuwekee kwenye buti ya meli/ndege ya mizigo hizo chupa mbili pesa tunatuma mpesa na ya kutolea." Ama hata angetumwa mfanya usafi tu wa wizarani akimbie faster.

Aliyesema maajabu ya dunia yako 7 pekee, apimwe akili.
Yaani chupa mbili tu, tuuu! Nashindwa kuamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Salange

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
683
1,000
Hiyo ya kwenye maboksi si ya Wamadagascar waishio nchini ikiwa imetolewa na ndugu zao walioko Madagascar? Au sikumwelewa vizuri Kabudi. Yetu ni chupa mbili tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
140,698
2,000
Leo angalau umeongea la maana, kumbe ukiacha mambo ya uchawi una akili .
Huyu jiwe kajaa ego sana ndicho kinachomsumbua, anajiona smart dunia nzima, kwa hiyo hasikilizi chochote anaamini anachoamini ndicho sahihi na hakuna wa kumwambia chochote. Hiyo ndiyo shida yake tu
Leo angalau umeongea la maana, kumbe ukiacha mambo ya uchawi una akili .... JF raha sana kuna mmoja hapo kasema naandika pumba tupu
Anyway....!!! Thanks dude for a compliment

Jr
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
140,698
2,000
Misukule kama hii ndio inakupa bidii ya kuposti ujinga.....
nishakujua ww ni wa kupuuza ......
" When wise man are silent ignorance multiplier"
When wise man are silent.. wise MAN ARE.. shikamoo kilugha.. Kama huwezi lugha za watu usiforce kuweza ama kujitia mjuzi

Jr
 

The Happiness

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
5,467
2,000
Mkemia mkuu wa serikali anasema Dkt. Fidelice Makumiko amesema : ''Dawa hizi ni msaada, na hawawezi kukataa kitu ambacho wamepewa...dawa hii tumeipokea kama msaada na sio kwa ajili ya kugawa kwa wananchi ... dawa hii tumeipokea kama zawadi kwa ajili ya kufanya utafiti wakatuonyesha kuwa ni salama na haina madhara kwa wananchi wao'' View attachment 1445485 View attachment 1445487

Jr
Prof kanywa sample ya utafiti
Wananchi wao ni wananchi wetu..?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom