Baba naye awa Chifu wa Wanyakyusa...Mh?

Hao machifu waliomsimika ni feki! Batukosisye isoni!! Ase!! (Wametutia aibu)
 
JK ndiye Nyakyusa's majestic Chief Mwangupili?

Chief wa Wanyakyusa hauwezi simikwa ukiwa Mbeya Mjini;Wanyakyusa wapo kwa wingi Wilaya mbili tu Mkoani Mbeya nazo ni Kyela na Rungwe na kama unapewa nafasi hiyo kubwa ya kimila unatakiwa uwepo Kyela au Rungwe chini ya amri za "Mafumu"!

Chief Mwangupili huwezi pewa ukiwa Mbeya mjini ambayo ni mbali sana na Nyakyusa land tena eti ukisimikwa kwenye nafasi hiyo na Chief wa wasafwa Mwashenga;hii ni dharau kwetu!

Pia,kwa mila za wanyakyusa,haiwezekani Baba(JK)awe Chief na pia mtoto(Ridhiwan)awe chief wa kabila hilo hilo bila kusubiri kwanza baba yake"aondoke"!Nahisi wamedanganywa!!

Asante kaka kwa kufafanua....mimi nilikereka kuwa hii sio sahihi hata kama sio Mnyakyusa
 
Jamani mbeya ina makabila zaidi ya matano wasafa,wandali,wanyamanyafu etc
Wanyakyusa maeneo yao ni Rungwe na Kyela uko kwingineko wako wachache wanaishi Mbeya mjini,ileje,mbozi etc
Na machief wao maarufu kama Mwakatumbula,Mwakalukwa etc
 
Miaka yote huwa ninawatania watani wangu wanyakyusa kuwa ni jamii iliyochanganyikiwa. sasa naona ni jamii inayoelekea kufa. Mkwere anawezaje kuwa chifu wa wanyakyusa? maana ya uchifu wanaijua? sina kumbukumbu ni linu amesimikwa kuwa chifu wa kabila lake-wakwere
 
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,Mh. Dr. Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na machifu wa Mbeya waliongozwa na Chifu mkuu,chifu Mweshenga mara baada ya kusimikwa uchifu.

Mbeya+-+Machifu.jpg

Machifu wa kinyakyusa wanavaa lubega nyeusi, huyo wa katikati kavaa vazi la kumlinda (lubega) alilotoa kwa shehe yahya. Si mnakumbuka yaliyomkuta kule mwanza mwaka 2005? hapo ni nguvu za giza tupu. kemea hilo katika jina lililokuu kushinda yote!
 
Kinachofanyika katika hilo zoezi ni usanii mtupu na unafiki wa viongozi wa ccm na serikali yake mkoani Mbeya. Hawandio wanaoandaa hayo mazingaombwe.

Wasimikaji wenyewe hawana nasaba na uchief, mzee kama Ambangile wa pale kwenye kijiwe cha Ipyana darajani aliyehusika kumsimika JK au Gracewell Mwakalukwa aliyemsimika Ridhiwani ni walamba viatu wa RC Mbeya na hawana nasaba ya koo za kichifu, wale ni BAPENA, kwa maana ya commoners.

Paramount Chief alikuwa Mwakyembe na mwengine upande wa Rungwe nimemsahau, koo zingine za kichief ni za kina Mwakalukwa na Koroso na hawa wapo warithi wake ambao hawajawahi shiriki hayo matukio ya kitapeli.

JK na familia yake ni malimbukeni, ni watu wenye kupenda sifa ndio maana hudanganywa na kuhadaiwa kila siku.
 
Inaonekana wazee wa kinyakyusa nao ni hamnazo!!! Hata kama ni kujipendekeza basi hii sasa ni too much.

Hawa waliomsimika JK siyo Wanyakyusa, ni Wasafwa. Rizi alisimikwa na Wanyakyusa wa Kyela, ila labda niseme alisimikwa na Wanyakyusa ambao ni CCM, siyo Wanyakyusa wote. Hata hivyo, samaki mmoja akioza wote wameoza!!
 
Wazee wenyewe mbona wanaonekana kama wamelazimishwa kufanya hiyo shughuli. Cheki nyuzo zao.
 
JK ndiye Nyakyusa's majestic Chief Mwangupili?

Chief wa Wanyakyusa hauwezi simikwa ukiwa Mbeya Mjini;Wanyakyusa wapo kwa wingi Wilaya mbili tu Mkoani Mbeya nazo ni Kyela na Rungwe na kama unapewa nafasi hiyo kubwa ya kimila unatakiwa uwepo Kyela au Rungwe chini ya amri za "Mafumu"!

Chief Mwangupili huwezi pewa ukiwa Mbeya mjini ambayo ni mbali sana na Nyakyusa land tena eti ukisimikwa kwenye nafasi hiyo na Chief wa wasafwa Mwashenga;hii ni dharau kwetu!

Pia,kwa mila za wanyakyusa,haiwezekani Baba(JK)awe Chief na pia mtoto(Ridhiwan)awe chief wa kabila hilo hilo bila kusubiri kwanza baba yake"aondoke"!Nahisi wamedanganywa!!
Mbeya mjini na vijijini ni chifu MWANSHINGA yaani himaya ya msafwa . Mbozi mnyiha ... Rungwe na kyela mwangupili nyakyusa
 
Mwanshenga ni Msafwa! Kabila linalodharaulika sana Mbeya! Angalau siku hizi wanajitambua kidogo! U Chief wa Mbeya angeenda Rungwe au Kyela! Sio Hapo Mbeya Mjini!
 
Back
Top Bottom