BAba na Mwana- Mahusiano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BAba na Mwana- Mahusiano

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MwanajamiiOne, Aug 25, 2009.

 1. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #1
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Habari ndugu
  Mimi huwa si mpenzi wa Udakus but kichwa cha habari kilinishawishi ...................... Hivi ni wapi tunapoelekea watanzania wenzangu?  Siyo siri tena, akiangua kilio nyumbani kwa mama yake mkubwa katika Mtaa wa Miningani Kondoa mkoani hapa, mbele ya Mwandishi wa Uwazi, Binti huyo alieleza kuwa, Baba yake mzazi ambaye ni Mpiga debe katika Stendi ya Mabasi yaendayo mikoani Mjini Dodoma, amekuwa akimlazimisha kuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu toka mama yake afariki hadi pale alipomkubalia na kujikuta akiambulia mimba ambayo hata hivyo mtoto alifariki mara baada ya mimba kuharibika.

  Akieleza mkasa mzima ulivyoanza, Msichana huyo alisema, alilazimika kusoma huko Kondoa, japo yeye ni Mzaliwa wa Chamwino Manispaa ya Dodoma, baada ya wazazi wake kutengana na baadaye kwa bahati mbaya mama yake alifariki dunia kwa kile alichodai kuwa ni Ugonjwa wa UKIMWI, hivyo kujikuta akipata malezi ya baba peke yake.

  Huku akimwaga machozi, Binti huyo alisema baada ya kumaliza Elimu ya Msingi, mwaka 2008 alichaguliwa kujiunga na Shule moja ya Wasichana iliyoko Iringa, ndipo Baba yake Mzazi alipomuahidi kumsomesha ambapo alimpatia mahitaji yote ya shule na kufanikiwa kuanza Kidato cha Kwanza mwaka huo.

  Alisema wakati wa likizo, Baba yake alikuwa akimlipia nauli ya kwenda Iringa na kurudi Dodoma na hata likizo ilipomalizika, alifanya vivyo hivyo, lakini mwishoni mwa mwaka huo mwezi wa kumi na moja, alipata taarifa kutoka kwa baba huyo kuwa Mama yake alikuwa amefariki dunia huko nyumbani kwao Kondoa na aliweza kufika na kumzika Mama yake.

  Kwa masikitiko alisema, baada ya kufunga shule mwezi wa kumi na mbili alirejea Chamwino, Dodoma kwa Baba yake Mzazi na akawa akilala chumba na kitanda kimoja na mzazi wake huyo kwa kisingizio kuwa, hakuwa na namna nyingine kwani aliishi kwa ukata.

  Akasema. Ilikuwa Desemba 12, mwaka jana, Baba yake alirudi usiku wa saa nne na kumlazimisha kufanya ngono na alipojaribu kumkatalia, mzazi wake huyo alimwambia endapo angekataa, angemuua, jambo lililomfanya aingiwe na hofu hivyo kubaki na mshangao mkubwa akiwa haamini kile alichokuwa akifafanyiwa na mzazi wake huyo.

  Maskini wa Mungu, Binti huyo anasema alikuwa katika siku za hatari (siku zake) kushika mimba, kwa hiyo baba yake alipogusa tu (kufanya naye mapenzi) akajua tayari amenasa mimba.

  Msichana huyo alisema baada ya kitendo hicho, alikwenda Kondoa kumalizia msiba wa mama yake na aliogopa kurejea kwa baba yake na kulazimika kurudi tena shuleni lakini baada ya kufika huko shuleni huwa kuna kawaida ya wanafunzi kufanyiwa vipimo kujua kama wapo wenye ujauzito lakini cha ajabu vipimo havikuonesha kama alikuwa na ujauzito.

  MIEZI MIWILI BAADAYE Binti huyo alianza kujisikia vibaya lakini aliogopa kuwaambia walimu na kubaki na hali hiyo mpaka aliporudi nyumbani mwaka huu likizo ya mwezi wa sita na kwenda kwa mama yake mkubwa aishie Area A, mjini hapa na kumwelezea mwanzo hadi mwisho wa mkasa huo, ndipo alipompeleka katika Hospitali ya Matovolwa na kugundulika kuwa alikuwa na ujauzito wa miezi sita. Akasema, alijaribu kumueleza baba yake lakini mzazi huyo alimtisha kwa kumwambia asimtaje yeye bali amsingizie mtu mwingine, jambo ambalo alimkatalia na kumwambia kuwa amemweleza mama yake mkubwa.
  WIKI MBILI BAADAYE Alisema, alipigiwa simu na mama yake mkubwa wa Kondoa akijulishwa kuwa taarifa za kulala na baba yake Mzazi kwa wanafamilia wote na zaidi akilaumiwa kuwa mama yake alikufa kwa UKIMWI ambao aliukwaa kutoka kwa baba huyo. Akasema, hali hiyo imekuwa ikimsumbua kwakuwa hata yeye anajua jinsi mama yake mzazi alivyofariki kwa mateso makuu.

  SIKU ZA HIVI KARIBUNI Msichana huyo anasema kwa sasa anasumbuliwa na kupanda kwa presha iliyopelekea yeye kulazwa siku sita katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwasababu ya mawazo, hali iliyosababisha mimba yake ya mtoto wa kiume kuchoropoka.

  Binti huyo alisema baada ya kuruhusiwa alirudi kwa mama yake mkubwa wa Area A Dodoma lakini alianza kusumbuliwa na miguu kuwaka moto hadi kufikia hatua ya kuiloweka kwenye maji ya baridi na kushindwa kutembea.

  Baada ya Mama yake Mkubwa kuona hali hiyo, ilimbidi amuarifu dada yake aliyeko Kondoa na kumpeleka huko na ndipo alipo sasa akiendelea na matibabu hivyo kushindwa kurejea shuleni kuendelea na masomo.

  Kwa mujibu wa mama yake mkubwa wa Kondoa, alimchukua binti huyo baada ya kusikia matatizo yaliyompata na kusema kuwa, wakati wa uhai wa marehemu mama yake walihangaika kimatibabu mpaka walipompeleka Hospitali ya Wilaya ya Kondoa na kugundulika kuwa aliambukizwa Virusi Vya UKIMWI na kwa kuwa walimchelewesha, walishindwa kupata matibabu sahihi hivyo kupoteza uhai. Anasema, alimwita binti huyo na kumweleza kuwa, kwakuwa alifanya ngono na baba yake, ni vizuri wakahakikishe juu ya Afya yake.

  Tarehe 14, mwezi huu, wawili hao walikwenda katika Hospitali ya Wilaya ya Kondoa na kuchukua vipimo vya HIV na kutakiwa kurudi tena kupima mwezi ujao ili kuhakikisha mara ya pili.

  Source: http://www.globalpublisherstz.com/2009/08/25/baba_kanibaka_kanipa_mimba_na_ukimwi.html
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  uvumi tu huu!
  practically IMPOSSIBLE
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii ipo sijui kama ni udaku lakini ngoja nikuwekee PC yake.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Huyu ndo binti mwenyewe aliyekumbwa na mkasa​
   
 5. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwani wewe haujawahi kusikia baba anakula kuku na mayai yake,au unachoona wewe akiwezekani hapo nini.
   
 6. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2009
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,501
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Fidel80;
  Unanifurahisha sana, kwenye minuso kama hii hukosi kuchangia au ku-provide details.

  Ile thread ya leo inayohusu marupurupu ya vigogo kuwa juu umeshaiona? vp huko nako umeshachangia au bado?
   
 7. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #7
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hata mie ninatamani sana iwe uvuni maana kama ni kweli basi tumekwisha uko wapi utu wetu?


  Kuna sehemu binti anasema aliporudi likizo alikuwa analala chuba kimoja na kitanda kimoja na baba yake jamani- ninachouliza hapa je hisia za kibinadamu (baba kama mwanaume) si zinakuwa controlled na akili ya mtu au?
   
 8. w

  wakumbuli Senior Member

  #8
  Aug 25, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  E bwana ee wewe uko juu,sasa sijui unataka tuchangie nin i na mtoto ameshafariki dunia,au huyo dingi ndio anakutisha,Mbona huelezei hali yake na mwenendo wake kwa sasa ili tutatue tatizo kamilisha upekuzi
   
 9. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #9
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mtoto gani unasema amefariki? aliyefariki ni hicho kiumbe kilichokuwa kinatarajiwa. Ninachokuomba uchangie ni wapi tunaelekea iwapo tumefikia hatua ya kuwa wanyama kiasi hiki?- kwanza kutembea na binti yako wa kumzaa na pili kumwuua kwa ugonjwa hatari wa UKIMWI- kwangu its too much kwa kweli
   
 10. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  guys,
  huu ni uvumi tu.believe me or not.
  hivyvo vyanzo vyenu vya habari ''ni utata mtupu''
   
 11. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,649
  Likes Received: 1,473
  Trophy Points: 280
  Mi naomba Mungu tu huyo binti awe HAJAAMBUKIZWA kwa muujiza wowote ule. from there on tunaweza kujadili lakini kama hali ni hii....oops mbona najisikia kulia jamani this is too much!
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  kaizer kaka yangu................. hii ndio dunia ya sasa. Ila Geoff ametuambia ni uzushi huu si kweli lets hope kuwa si kweli maana ninasikia kufa.

  Hivi JF hatuwezi kuwa na utaratibu wa kufuatilia mambo kama haya?yaani kuwe na jopo la wanasheria wanaoweza kufuatilia na kuhakikisha haki inatendeka kwa wanaoonewa? Kwa sababu ninaamini kabisa huyu akishapimwa itaishia hapo hapo na kama (Mungu pitisha mbali) amepatikana na ugonjwa ndo bahatii mbaya na mtuhumiwa ataendelea kupeta na kama hakukutwa nao basi ni closed- case.
   
 13. b

  bnhai JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Mie sijaona kwanini uitwe uvumi? Inawezekana ni kweli imetokea. Ila nasikitika sijaona hata sehem moja vyombo vya dola vikihusishwa.
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hehehe Mkuu Makanyaga nipo mzee kama kawa hakuna kulaza damu.
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Aug 25, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hehehehe MJ1 kuongea rahisi lakini vitendo ndo F unakijua kipindi cha Heka heka cha Clouds FM kinarushwa na Gea Habib anafatilia mikasa kama hii mitaani huko na kurusha radioni sasa kuna msamalia alijitokeza na kuguswa na tukio mojawapo akataka kulifanyia kazi mbona wale watangazaji wakawa wanamyeyusha na mwishowe kula kona kabisa. Sasa sijui kwa walikuwa wanaogopa kutoa ushirikiano.
   
 16. Koiya

  Koiya Member

  #16
  Aug 25, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Achana nae huyo asichokijua au anachopinga nini dunia ya sasa usijue mambo hayo haya basi huyajui hujawai hata kusikia usitutanie wewe au yalikufika unaona so kwa sababu vitendo hivyo vya kikatili dunia hii wanaona kama fashion yani hii ni laana
   
 17. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  chanzo cha habari nakionaga hakinaga ishu zinazoeleweka kabisa, mengi ni ya uongo/uzushi, kama hii ni kweli bac mungu a2nusuru.
   
 18. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #18
  Aug 25, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hii kama ni kweli ni ubakaji si mahusiano. Nashangaa pia mwandishi haoneshi kama hiyo kesi imefikishwa polisi au la, na kama bado ni kwanini?
   
 19. GP

  GP JF-Expert Member

  #19
  Aug 25, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  chanzo ni cha kidaku, uzushi mtupu.
   
 20. M

  Msindima JF-Expert Member

  #20
  Aug 25, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Geoff, vyovyote tu ilivyo iwe kweli au uvumi ni sawa tu lakini elewa kuwa hivi vitu vipo kwenye jamii zetu,wako wabab pasipo aibu hudiriki kufanya vitendo hivi na watoto wao tena wa kuwazaa.

  Cha muhimu ni kujadili kwamba tunakoelekea ni wapi? maana kama hii story ni kweli kwa hakika inatisha sana na inaumiza sana unajaribu kufikiri huyo baba akili yake ni nzuri au ina hitilafu?
   
Loading...