Baba na mwana ...! Kweli wakati si milele

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,606
696,727
Kuna jambo limenitafakarisha sana...mahusiano ya baba na mtoto...Kwenye Biblia takatifu kuna simulizi nyingi zinazowahusu baba na mwana...hata Mungu mwenye enzi yote yote anamtaja Yesu Kristo kama mwanae mpendwa
Baba kama mzazi ana nafasi kubwa kiroho kwa mtoto kutokana na kizalia DNA ....baba ana uwezo wa kutoa laana na ikashika na pia ana uwezo wa kubariki na mtoto akabarikiwa

Kwenye dhana nzima ya baba na mwana kuna
Baba halisi
Baba halali
Baba wa kufikia
Baba wa hiari
Baba wa kurithi
Ni katika aina zote hizo za ma baba ....inaweza ikatokea tu kiasili kabisa baba akajikuta anampenda sana mmojawapo wa watoto wake wengi alionao...na sometimes sio lazima awe wa kumzaa yeye....yani mtoto wa kufikia anaweza kupendwa zaidi kuliko mtoto halisi

Mtoto mpendwa kwa baba anapogundua kuwa yeye ndio kipenzi cha dingi kuliko wengine...kwa akili za kitoto huanza kuringa na kufanya mambo ya kijinga mengi akiamini kuwa baba hawezi kumfanya kitu ....kuna wakati anaweza hata kuzusha jambo ama kumsingizia mtu kitu kwa baba, na baba bila kutafakari marambili akamchukulia hatua mtu huyo bila kuangalia uhalisia wa tuhuma zenyewe
Mtoto akiona hivyo huota mapembe na kuvimba kichwa...lakini waswahili wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo...na ngoma ikivuma sana hupasuka.....!!!.ni katika kilele cha upendo wa baba kwa mtoto ndio jambo baya sana hutokea na baba akili kuanza kumrudi taratibu
Ewe mtoto ukishaona baba hatoki tena kwenda na wewe popote iwe bar, kwenye harusi ama mialiko yoyote...ukiona baba hakuiti tena chumbani kwake muongee...ukiona baba hakuiti tena akutume hata dukani...tambua tu kuwa sasa baba upendo umepungua na hakupendi tena kama zamani...utajipendekeza na kujifanya umejutia makosa yako lakini wewe sio wake tena....na akimpata mgeni wa kumpa zawadi anaweza kukugawa bure
 
Mzazi mbaguzi wa familia yake ana pancha sehemu ya kichwa chake, eidha kawapata hao watoto kwa bahati mbaya yani matokeo ya alichokua anakifanya hakutegemea yangeleta hayo ama kaona mtoto huyu si lolote
 
Kuna jambo limenitafakarisha sana...mahusiano ya baba na mtoto...Kwenye Biblia takatifu kuna simulizi nyingi zinazowahusu baba na mwana...hata Mungu mwenye enzi yote yote anamtaja Yesu Kristo kama mwanae mpendwa
Baba kama mzazi ana nafasi kubwa kiroho kwa mtoto kutokana na kizalia DNA ....baba ana uwezo wa kutoa laana na ikashika na pia ana uwezo wa kubariki na mtoto akabarikiwa

Kwenye dhana nzima ya baba na mwana kuna
Baba halisi
Baba halali
Baba wa kufikia
Baba wa hiari
Baba wa kurithi
Ni katika aina zote hizo za ma baba ....inaweza ikatokea tu kiasili kabisa baba akajikuta anampenda sana mmojawapo wa watoto wake wengi alionao...na sometimes sio lazima awe wa kumzaa yeye....yani mtoto wa kufikia anaweza kupendwa zaidi kuliko mtoto halisi

Mtoto mpendwa kwa baba anapogundua kuwa yeye ndio kipenzi cha dingi kuliko wengine...kwa akili za kitoto huanza kuringa na kufanya mambo ya kijinga mengi akiamini kuwa baba hawezi kumfanya kitu ....kuna wakati anaweza hata kuzusha jambo ama kumsingizia mtu kitu kwa baba, na baba bila kutafakari marambili akamchulia hatua mtu huyo bila kuangalia uhalisia wa tuhuma zenyewe
Mtoto akiona hivyo huota mapembe na kuvimba kichwa...lakini waswahili wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo...na ngoma ikivuma San hupasuka......ni katika kilele cha upendo wa baba kwa mtoto ndio jambo baya sana hutokea na baba akili kuanza kumrudi taratibu
Ewe mtoto ukishaona baba hatoki tena kwenda na wewe popote iwe bar, kwenye harusi ama mialiko yoyote...ukiona baba hakuiti tena chumbani kwake muongee...ukiona baba hakuiti tena akutume hata dukani...tambua tu kuwa sasa baba upendo umepungua na hakupendi tena kama zamani...utajipendekeza na kujifanya umejutia makosa yako lakini wewe sio wake tena....na akimpata mgeni wa kumpa zawadi anaweza kukugawa bure
Mshana unaona gere?
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom