Mr. Masasi
Member
- May 12, 2011
- 53
- 4
Nahitaji msada wenu jamani, mimi ni mmoja kati ya watoto sita tuliozaliwa na baba yetu pamoja na mama yetu wakiwa ndani ya ndoa. Lakini walitengana mara baada ya baba yangu kuwa na nyumba ndogo ambako alifanikiwa kuzaa watoto watatu, mara tu baada ya mama yngu kuligundua hilo aliamua kuondoka kwenye mji wake na kwenda kuolewa na yeye na kufanikiwa kuzaa watoto wawili, baadae mume wake na mama ambaye ni baba yngu wa kambo alifariki. Alipofarik mama aliamua kurudi kwenye mji wake ambao aliukimbia, yaani nyumban kwetu. Kwa bahati mbaya sisi watoto wake wote sita hatukubahatika kupelekwa shule na baba yetu pamoja na kwamba baba alikuwa mtumishi na kuna mali ambayo ingetosha kutusomesha, lakin watoto ambao baba alizaa nje ya ndoa wote amewasomesha. Sasa kwa sasa mara bada ya mama kurudi kwenye mji wake akawa amepiga marufuku ile mali yote kutumika kuhudumia familia ndogo ya baba ambapo bado anaish na huyo mke wake mdogo. Baba bada ya kuzuiwa kuchukua mali kutoka kwetu maisha yamemgonga hana uwezo tena wa kuhudumia tena familia hyo, amekimbilia mahakan na amefungua kesi akidai anataka kugawa mali kwa wanae. Sasa kisheria hapo inakuaje mana wazazi wote hakuna aliyefariki, mama hataki ile mali igawanywe, tukiwa tunampa suport sisi wanae wanne, wakike watatu na wakiume ni mimi tu, kiukweli baba mi simkubal, harafu baba anapewa suport na watoto wawil wakiume kwan nao wanataka mali igawanywe na wanamfeel dingi. Je kisheria twaweza itaka mahakama tupige kura mana ss tuko wengi najua tutawashinda tu. Na sheria inasemaje ili kumlinda mwanamke yani mama yetu. Nipeni ushauri mana mi ndo msemaji mkuu pale mahakamani harafu ndo kama wakili harafu elimu ya sheria sina . Natanguliza shukran kwa wanasheria wote