Baba Mzazi Wa Mwanamuziki Diamond Aibuka-Soma Mambo Mazito Aliyosema Hapo Chini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba Mzazi Wa Mwanamuziki Diamond Aibuka-Soma Mambo Mazito Aliyosema Hapo Chini

Discussion in 'Celebrities Forum' started by nngu007, Jul 12, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG]  BABA mzazi wa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond', (pichani) Abdul Juma ameibuka ambapo mbali na tukio hilo pia amenena mambo mazito kuhusu mwanaye huyo huku akimsukumia tuhuma nzito mama mtu, Amani linaanika kila kitu.

  ASAKWA PANDE ZOTE ZA DAR
  Awali lilitangulia zoezi la kumsaka baba Diamond katika pande zote za Jiji la Dar es Salaam ili kumsikia alichonacho moyoni kuhusu mafanikio ya mwanaye huku taarifa za mahali anapoishi zikipotoshwa na watoa habari wetu.
  Wapo waliosema mzee huyo anaishi Kibamba, wengine Mbagala, pia wapo waliodai anakaa Manzese au Magomeni, jijini Dar es Salaam.
  Timu ya mapaparazi wa Amani ilizama kazini kikamilifu ikiapa kumnasa mzazi huyo popote alipo na hatimaye Julai 2, 2012 saa saba mchana ilifanikiwa kupabamba nyumbani kwake, Magomeni Kagera, jijini Dar es Salaam lakini mwenyewe hakuwepo.
  Ziliachwa salamu za utambulisho kwa jirani mmoja ili atakaporudi mzee huyo amtaarifu kuwa mapaparazi watarudi siku nyingine.
  Julai 7, 2012 saa tano asubuhi mapaparazi wetu walitinga nyumbani hapo na kumkuta mzee huyo akisema alipata salamu na alikuwa akisubiri ujio huo, hivyo akawa amejiibua mwenyewe.

  AANZA KWA KUANIKA HISTORIA KWA UFUPI
  Baada ya salamu na utambulisho, mzee huyo alianza kwa kukiri kwamba kweli yeye ni baba mzazi wa Nasibu (Diamond) na kuweka wazi kwamba aliachana na mama mzazi wa msanii huyo miaka 9 iliyopita.
  "Ni kweli mimi ndiye Abdul Juma, ni baba mzazi wa Nasibu au Diamond. Eee, mimi niliachana na mama Nasibu miaka tisa iliyopita, tena siku tunatengana niliondoka nyumbani saa tisa usiku, maana nilikuwa naishi kwao (ukweni).


  AMGEUKIA DIAMOND
  Kinyume na matarajio ya kuzungumzia mafanikio ya mwanaye kwa sasa, baada ya kuwekwa katikati na waandishi wetu, mzee Abdul ‘aliangusha' kilio cha lawama kwa Diamond kuhusu matendo anayomfanyia kila kukicha.
  Mzee huyo anayeonekana ‘kisharobaro' alisema mafanikio makubwa aliyonayo mwanaye yasimfanye ashindwe kumthamini yeye kama baba na mapenzi yake kuyaelekeza kwa mama yake tu.
  "Kuhusu Diamond, labda nimwambie huyu mtoto kuwa, amepata mafanikio ndiyo, lakini mafanikio hayo yasimfanye ashindwe kunithamini mimi kama baba yake na kupeleka mapenzi yote kwa mama yake tu," alisema.


  NI KWANINI?
  "Nasema hivyo kwa sababu, zamani kabla jina lake halijawa kubwa, mawasiliano yetu yalikuwa mazuri sana, lakini nikaja kushangaa baada ya kuwa staa, akakata mawasiliano na mimi baba yake, aliangalie hilo."
  Akaongeza: "Sisemi kwa sababu nataka awe ananiletea hizo fedha zake, la hasha! Ila mimi kama baba yake ajue kuniheshimu.
  "Diamond nampigia simu hapokei, namtumia meseji hajibu, maana yake nini? Naumizwa sana na kitendo cha kutopokea simu yangu kila ninapompigia kumjulia hali. Na hali hii ameanza mara baada ya kupata mafanikio.


  JARIBIO LAIVU Katika kuthibitisha hilo, paparazi wetu alimtaka mzee huyo kumwendea hewani mwanaye ili kujiridhisha kama kweli ‘hapokeagi' simu yake, simu ikapigwa, ikaita wee mpaka ikakatika.
  Baba Diamond: "Si umeona, si nilikwambia ukawa huamini."


  MARA YA MWISHO KUMUONA DIAMOND
  Mzee huyo aliendelea kutiririka kuwa, mara ya mwisho Diamond kufika nyumbani kwake ilikuwa mwezi wa tatu (Machi) mwaka huu baada ya hapo mawasiliano yakakatika.
  "Diamond alikuja nyumbani kwangu mwezi wa tatu ikiwa ni mfungo wa tatu katika dini yetu ya Kiislam, akanipa fedha. Baada ya hapo hatujaonana tena wala hanijulii hali," alilalama mzee wa watu.


  SMS YA MWISHO KUIJIBU
  Alisema Aprili, mwaka huu, Diamond alipotwaa tuzo tatu za Kili Music Awards 2012, yeye alimtumia ujumbe mfupi wa maneno akimpa hongera naye akajibu asante baba. Lakini baada ya hapo ikawa imetoka.
  "Baada ya kufanikiwa kutwaa tuzo za Kili, mwaka huu nilimpigia simu mwanangu ili nimpongeze, hakupokea, nikamtumia SMS ndipo akajibu, ‘asante baba', mchezo ukaishia hapo.
  "Namshukuru sana dada yake, Mwajuma Abdul (Queen Darleen) yeye ndiyo yupo karibu sana na mimi kwani mara kwa mara anakuja kunitembelea na wakati mwingine hunikumbuka kwa fedha, hata pale aliposhinda tuzo ya Wimbo Bora wa Dancehall alifika nyumbani kunionesha tuzo yake, binafsi nilijisikia furaha," alisema mzee Abdul ambaye kwa sasa hana mke.


  HAJUI ANAPOISHI MWANAYE
  Mbali na msanii huyo kutopokea simu ya baba yake kila anapompigia, vile vile mzee huyo alidai hajamuonesha wapi anapoishi.
  "Huyu mtoto hajawahi kunionesha anapoishi, sijui anafikiri nikiwa karibu naye nitakuwa namuomba fedha. Mimi sina njaa ‘kihivyo' na wala sitaki fedha zake, ila ninachotaka salamu tu, nasikiasikia anaishi Mwenge (usahihi ni Sinza Mori) lakini hataki kunionesha.
  "Ninachojua yote haya yana mwisho kwani nyota aliyonayo sasa kuna siku itazima. Simuombei mabaya lakini inaniuma sana kunifanyia hivyo."


  DIAMOND APIGIWA SIMU MARA KUMI NA MBILI
  Baada ya kupata matamshi hayo ya baba mzazi wa Diamond, mwandishi wetu siku ya Jumanne alifanya jitihada za kumpata msanii huyo ili ajibu ‘mashitaka' hayo lakini licha ya kupigiwa simu mara kumi na mbili hakupokea.
  Mbali na kupigiwa simu, paparazi wetu alimtumia ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake ya mkononi, lakini pia hakujibu kitu. Juhudi za kumsaka zinaendelea.


  Source: GPL
   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  mbona sioni jambo zito hapo
   
 3. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Dingi hana lolote anataka mkwanja tuu.
   
 4. B

  Babuu Rogger JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 80
  Baba ni baba hata ukiwa unamiliki Millioni Mia, Diamond arudi nyuma ana bahati sana baba yake yupo hai.
   
 5. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  jambo zito lipo mkuu,huu ni mwanzo tu wa hii tamthilia na itauza sana magazeti..watu wako kwenye biashara.
   
 6. B

  Babuu Rogger JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 80
  Usiseme hivyo ndugu yangu.
   
 7. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,671
  Trophy Points: 280
  Take 92%
   
 8. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu na pia ukitaka kujua umuhimu wa kitu ni pale utakapokikosa. Huyu baba akifa katika mahusiano mabaya namna hii na Diamond kuna uwezekano mkubwa wa nyota yake kupotea kabisa . Aelewe pasipo huyu baba asingekuwepo duniani leo na hiyo inatosha kuwa na THOUSANDS OF ASANTE NA HESHIMA KWA BABA
   
 9. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45

  Unataka nisemaje?
   
 10. s

  sawabho JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Weeee, kutopokea simu ya Baba mzazi sio jambo zito, je kama anaumwa anataka akwambie neno la mwisho !!!!
   
 11. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,520
  Likes Received: 10,437
  Trophy Points: 280
  ya kanumba (r.i.p) ya hamia kwa Almasi na atauza sana magazeti ya shigongo.!
   
 12. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,493
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280

  ...


  Mzee anafana na mwanae kichwa!!  .........
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Kutakuwa na aidha baba wa kambo au baba wa kufikia
   
 14. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,630
  Likes Received: 1,386
  Trophy Points: 280
  Hao waandishi nao yanawahusu nini?
   
 15. sikafunje.N

  sikafunje.N Member

  #15
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Like father like son ... 'masharobaro'
   
 16. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #16
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,286
  Likes Received: 808
  Trophy Points: 280
  Du hapa mama atafutwe aseme ukweli huenda Diamond keshampata Baba mwingine mbona naona mdomo hawafanani?
  Hata hivyo bado inaniuma kwani inaonyesha hata km aliimlea hata kumjali hataki, watoto wa kiswahili atadai Baba yake ana Harrier, Scania au yuko YUROP
   
 17. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 283
  Trophy Points: 160
  inakuaje baba anapotelekeza family pamoja na watoto,mama apate shida peke yake kulea watoto peke yake,ccha ajabu watoto wakikua na kuwa na pesa,baba ndio anajileta? visa kama diamond,kanumba etc vinatukuta wengi,mu uwa sielewi baba wengine inakuaje atelekeza familia harafu mkifanikiwa baadaye ndio anajileta
   
 18. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hebu mwambie huyo,mzazi ni mzazi tu,no matter what!
   
 19. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna kitu nimepata hapa,kumbe QUEEN DARLEEN na DIAMOND ni ndugu!,hii inathibitisha ule msemo wa wengi kwamba watoto wa kiume hupenda kuwa karibu na mama zao na watoto wa kike kama QUEEN DARLEEN kamwe hawawatupi baba zao.
   
 20. s

  shosti JF-Expert Member

  #20
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  si kila baba ni baba wengine wana majina yao
   
Loading...