TANZIA Baba Mzazi wa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo Mzee Urban Costa Ndunguru amefariki Dunia

TEAM 666

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
4,330
8,421
Baba Mzazi wa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo @jokatemwegelo , Mzee Urban Costa Ndunguru amefariki Dunia Alfajiri ya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa (ICU) kwa muda sasa baada ya kupata kiharusi (stroke).

DC Jokate ametuthibitishia taarifa hizo na kusema taratibu za mazishi bado zinaendelea nyumbani kwa Marehemu.


Update

Mwili wa Baba Mzazi wa DC wa Kisarawe Jokate Mwegelo Mzee Urban Costa Ndunguru unatarajiwa kuagwa Jumatatu December 21,2020 katika Kanisa la St Peters DSM, kisha kusafirishwa Jumatatu hiyohiyo kwenda Mbinga Mkoani Ruvuma.


Mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumanne December 22, 2020, katika kijiji cha Tanga, Mbinga. Mzee Ndunguru amefariki Alfajiri leo Hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa (ICU) kwa muda baada ya kupata Kiharusi (Stroke)

#RIPMzeeNdunguru







Chanzo Cha habari-Millardayo
 
millardayo-___CI-CdNZAG9s___-.jpg
 
Back
Top Bottom