Baba Mzazi wa Mhe. Tundu Antipas Lissu Mughwai afariki dunia jioni ya leo

Ninasikitika kuwatangazia ndugu zangu wa JamiiForums kuwa muda mfupi uliopita baba mzazi wa mheshimiwa Tundu Antipas Lissu Mughwai na Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai amefariki dunia muda mfupi uliopita. Marehemu Augostino Lissu Mughwai (84) amefariki katika hospitali ya taifa ya muhimbili alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu. Mungu amlaze mahala pema peponi, Amina.

Rest in peace.
 
poleni sana ndugu zangu. Tunashakuru Mungu kutuzalia wapiganaji Antipas, Christina na Vicent ; ndio ninnao wajua. Mahambe itakuwa na majonzi makubwa. Mungu amlaze mahali pema peponi mzee wetu.
 
...pole sana Lisu...Mwenyezi Mungu akujaaliye moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba...
 
Natumia wasaha huu kutoa pole kwa makamanda wetu wa msiba wa mzazi wao, kazi ya MUNGU haina makosa. RIP Mr. A Lissu
 
Hakika wote sisi ni wake yeye . mwenyezi Mungu na kwake ndiyo marejeo yetu.....Mungu akupe moyo wa subira na uvumilivu wewe mheshimiwa na jamii yote iliyoguswa...
 
Pole sana Mh. T. Lissu na wafiwa wote. RIP marehemu mzee wetu uliyetuzalia JEMBE LA UKWELI!
 
Back
Top Bottom