Baba Mzazi wa Mhe. Tundu Antipas Lissu Mughwai afariki dunia jioni ya leo

R.I.P Mzee wetu mpendwa Mungu wa amani akurehemu, akumbuke mema yako hapa duniani akupe pumziko la milele, kamanda Tundu Lisu na wanafamilia tupo pamoja ktk kipindi hiki kigumu, neno moja tu kumbuka kwetu ni kilio mbinguni ni furaha kwa baba yetu kumaliza utumishi wake hapa duniani.
 
Raha ya milele umpe eee bwana na mwanga wa milele umwangazie apumzike kwa aman,amina
 
R.I.P mzee Lissu,poleni sana wafiwa naamini Mwenyezi Mungu atawapa nguvu ktk kipindi hiki kigumu cha msiba....bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe/libarikiwe.
 
Sipati picha kama Tundu yuko ivi baba yake alikuwaje?
Naongelea michango yake bungeni na historia yake kama mwanaharakati mpaka akafikia kufungwa
RIP mzee wetu
 
Poleni wafiwa wote. Marehemu alale mahala stahiki. Amina. Tupo pamoja Kamanda Tundu Lissu na familia nzima!
 
Pole sana Kamanda na Familia yote, Tunakuombe upite salam ktk kipindi hiki kigumu!!
 
Ninasikitika kuwatangazia ndugu zangu wa JamiiForums kuwa muda mfupi uliopita baba mzazi wa mheshimiwa Tundu Antipas Lissu Mughwai na Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai amefariki dunia muda mfupi uliopita. Marehemu Augostino Lissu Mughwai (84) amefariki katika hospitali ya taifa ya muhimbili alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu. Mungu amlaze mahala pema peponi, Amina.
mkuu kama unaweza kutueleza msiba au mazishi watafanyia wapi ili watakao pata muda waungane na mhe. Tundu kwenye kipindi hiki kigumu
 
Mungu ampumzishe pema peponi..hakika tunamshukuru kwa kazi yake njema aliyoifanya ya kumlea kamanda wetu hata amefika alipo sasa.

Bwana amrehemu.
 
pole sana mh lissu ,familia yote ya marehemu na makamanda wote kwa msiba huu wa mzee wetu!
 
Ninasikitika kuwatangazia ndugu zangu wa JamiiForums kuwa muda mfupi uliopita baba mzazi wa mheshimiwa Tundu Antipas Lissu Mughwai na Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai amefariki dunia muda mfupi uliopita. Marehemu Augostino Lissu Mughwai (84) amefariki katika hospitali ya taifa ya muhimbili alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu. Mungu amlaze mahala pema peponi, Amina.

RIP Mzee Augostino Lissu Mughwai na MUNGU awatie nguvu wanafamilia wote katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
 
Back
Top Bottom