TANZIA Baba Mzazi wa Dkt. Emmanuel Nchimbi afariki dunia

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
9,529
15,816
Habari zilizonifikia usiku wa kuamkia leo ni kwamba Balozi mstaafu na kada mashuhuri wa Chama cha mapinduzi Dr. Emanuel Nchimbi amefiwa naa baba yake mzazi.

Mzee Alphonso Nchimbi amefariki alfajiri ya kuamkia leo katika hospitali ya magonjwa ya moyo ya Jakaya Kikwete Cardiac institute iliyopo jijini Dar es Salaam ambapo alikua akisumbuliwa na matatizo ya moyo.

Mola ampumzishe pema peponi na pole nyingi sana kwa Mh. Dr.Emanauel Nchimbi na familia kwa ujumla.

nchimbi.jpg

----
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Dk Emmanuel Nchimbi amefiwa na baba yake mzazi, John Nchimbi usiku wa kuamkia leo Jumapili Januari 23, 2022 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo baada ya kufika nyumbani kwa marehemu Tabata Relini, John Nchimbi ambaye ni mtoto wa marehemu amesema baba yake amefariki kwa ugonjwa wa moyo uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

“Mzee wetu alikuwa na matatizo ya moyo lakini siku tatu zilizopita hali yake ilibadilika na alichukuliwa kwenda kwenye vipimo hospitali ya TMJ, baada ya kupata vipimo kesho yake hali yake iliendelea kuwa mbaya kwa hiyo tuliamua kumuamishia JKCI kwa ajili ya vipimo zaidi.

“Na katika vipimo walibaini mishipa yake ya upande wa kulia na kushoto inayotoka kwenye moyo imeziba ambayo huwezi kuzibua kwa kutumia waya na ilitakiwa afanyiwe upasuaji mkubwa wa moyo ili kutengeneza njia nyingine na mingine kuibadilisha. Wakiwa kwenye mchakato wa kufanya hivyo ilipofika saa nane usiku wa kuamkia leo baba akafariki,”amesema.

John Nchimbi ambaye ni mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya kiteto amesema baada ya taarifa hiyo maandalizi yanaendelea na Januari 25,2022 wanatarajia kuupumzisha mwili kwenye makaburi ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

“Mzee wetu alikuwa Kamshina wa Jeshi la Polisi, alikuwa kwenye siasa kwa hiyo kutakuwa na miongozo ya kiserikali kwa sababu alilitumikia taifa kwa mara ya mwisho akiwa kama Kamanda wa Polisi wa Mtwara kabla ya kustaafu mwaka 1996,”amesema

Nchimbi amesema baba yake amefariki akiwa na miaka 77 akiacha mjane na watoto saba
 
Pole Sana Brother Emmanuel Nchimbi,Mwenyezi Mungu awe pamoja na nafsi yako
 
Habari zilizonifikia usiku wa kuamkia leo ni kwamba Balozi mstaafu na kada mashuhuri wa Chama cha mapinduzi Dr. Emanuel Nchimbi amefiwa naa baba yake mzazi.

Mzee Alphonso Nchimbi amefariki alfajiri ya kuamkia leo katika hospitali ya magonjwa ya moyo ya Jakaya Kikwete Cardiac institute iliyopo jijini Dar es Salaam ambapo alikua akisumbuliwa na matatizo ya moyo.
Mola ampumzishe pema peponi na pole nyingi sana kwa Mh. Dr.Emanauel Nchimbi na familia kwa ujumla.
Sema balozi wa zamani,
Lini aliandika barua ya kusitafu?
 
Back
Top Bottom