Baba Mwenye Uhusiano wa Kimapenzi na Binti Yake Atupwa Jela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba Mwenye Uhusiano wa Kimapenzi na Binti Yake Atupwa Jela

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Aug 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]Baba na binti yake ambao walikuwa kwenye penzi zito kwa kipindi cha miaka mitatu, wametupwa jela baada ya kupatikana na hatia ya kuingia kwenye uhusiano kinyume na maadili ya jamii.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Andrew Butler mwenye umri wa miaka 47 ambaye alikuwa akila uroda na binti yake Nicola Yates mwenye umri wa miaka 26, amehukumiwa kwenda jela miezi 10.

  Mahakama ya mjini Birmingham ilimuona Andrew na binti yake Nicola wote wana hatia ya kuingia kwenye uhusiano huo haramu uliodumu kwa miaka mitatu wakiishi pamoja kama mtu na hawara yake.

  Andrew aliachana na mama yake Nicola mwaka 1992 wakati huo Nicola akiwa na umri wa miaka sita.

  Alipokuwa na umri wa miaka 20 Nicola alianza kumtafuta baba yake kwa kutumia mtandao wa rekodi za familia nchini Uingereza unaoitwa Genes Reunited.

  Baada ya kufanikiwa kumpata baba yake, Nicola alikuwa karibu zaidi na baba yake na haukupita muda mrefu ukaribu huo uligeuka uhusiano haramu wa kimapenzi kati ya baba na binti yake.

  Hii ilikuwa ni mara ya pili wawili hawa kufikishwa mahakamani kwa kosa kama hili.

  Mara ya kwanza walinaswa wakiwa na uhusiano huu haramu miaka minne iliyopita ambapo Andrew alihukumiwa kwenda jela miezi minne wakati Nicola alihukumiwa kufanya kazi ngumu za kuitumikia jamii kwa jumla ya miezi 18.

  Lakini mwaka 2008 baba huyo na binti yake waliuamsha tena moto wa mapenzi na kuanza kuishi pamoja.

  Nicola alijaribu kufanya uhusiano huu uwe wa siri akijaribu kufanya kila awezalo ili familia yake isijue kinachoendelea.

  Lakini dada yake siku moja aligundua picha za ngono alizopiga Nicola na baba yake zilizokuwa kwenye simu na ndipo alipomuonyesha mama yao ambaye alihamaki kwa kusema "Huyu alikuwa mume wangu wa zamani".

  Akitoa hukumu, jaji wa kesi hiyo alisema "Najua kuwa mko kwenye uhusiano uliojaa mapenzi ya kweli, lakini uhusiano huu ni kinyume na maadili ya jamii".

  "Ni uhusiano usiokubalika mbele ya jamii kwa sababu ambazo zinaeleweka", aliongeza jaji huyo.

  Wakati Andrew akihukumiwa kwenda jela miezi 10, Nicola alihukumiwa kwenda jela wiki 26 lakini kifungo hicho kilibadilishwa na kuwa kifungo cha nje cha miaka miwili.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,139
  Trophy Points: 280
  Miezi kumi mbona michache?
  Huko anaenda kulimbikiza libido, akitoka anakuja na ari zaidi nguvu zaidi na kasi zaidi
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,077
  Likes Received: 6,540
  Trophy Points: 280
  Tena nasikia kuwa huyo faza ni dr. kwa taaluma. nilijua wenzetu wameelimika kumbe ni uozo mtupu.
   
 4. COMPLICATOR2011

  COMPLICATOR2011 JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Sioni kosa hapo, angekuwa ni mama na kijana wake sawa lkn kwa baba na binti yake huenda hata hamzai, cha msingi wakapime DNA kwanza wasikurupuke kuwatupa mahakamani.
   
 5. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kama ndoa ya jinsia moja wameruhusu na hiyo kitu waruhusu basi, wenyewe si wana akili sana!
   
 6. k

  kaeso JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hawa jamaa wana laana kwa kweli. Sasa wanamfunga miezi kumi ili iweje si bora wangemuachia tu..
   
 7. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni ajabu kweli hawa watu weupe, kama waliweza kuruhusu wanaume kwa wanaume kuoana, ili ndo wanaona ni kinyume na maadili?

  KWELI MAJUU HAMNAZO.
   
 8. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,119
  Trophy Points: 280
  Kwani walipima DNA wakathibitisha kuwa huyo binti huyo ni baba yake? je kama mama alim'bambika huyo jamaa? jamaa nae akaamua ajilie mazao yake?? haya yaishe tu maana naona mambo mengine hata shetani anayaogopa
   
 9. K

  Karry JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  duh huu sasa ndio mwisho wa dunia'
   
 10. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,756
  Trophy Points: 280
  Hapa t-zii wapo wanaobaka watoto wa wake zao, yaani mama kaja na katoto dingi anakula kuku na yai!! Af kuna ambao wapo kwenye malavidavi ya nguvu baba na mwanae wa kumtotoa af kuna wale wanawarubuni watoto zao na kuwatishia kuwauwa shenzi hiv skuhz kinadadapoa wapo tele kisa cha kumtaka mwanao haswa kinakuwa nini? Kaka c kiherehere cha kiumeni?!!!!
   
 11. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  47 kwa 26
  wote wa akili timamu !!
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Mar 19, 2014
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280

  you mean Tanzania hayapo haya?? wapo wengi tu
   
 13. I

  IBM2014 JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2014
  Joined: Mar 2, 2014
  Messages: 937
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kichefuchefu
   
 14. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2014
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,723
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  Njombe kuna mmoja kazaa na binti yake na wanaishi pamoja. yaani dulia ilipofikia. ukisoma katika Bible Mambo ya nyakati sura 18 imekataza haya mambo na ni laana mbele za Mwenyezi Mungu
   
 15. d

  dope bwoi Member

  #15
  Mar 19, 2014
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 97
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Mimi mwenyewe nime experience hiyo nlikua na demu wangu secondary wakati yuko form2 mi niko form4 nakuja kustuka kwamba dingi yake anamega baada ya kwenda mitaa ya kwao ndo mshikaji flani akanistua uyo demu anatembea na dingi yake tokea yuko std 6 kwakweli nilipagawa ila sikua na jinsi niliamua kumuacha kistaarabu bila yeye kujua nimetambua hilo ila demu shuleni alikua poor sana alikua anashika nafasi za mwisho nikaja kugundua ali athirika kisaikolojia...dingi yake ni mmachame na ni luteni kanali..anaishi mtoni mtongani-madafu
   
Loading...