Baba mkatiri, Mtoto huwa kama Baba, Baba Mstaraabu, Mtoto hufuata.

Mahweso

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
1,098
1,501
Kitu anacho kifanya Mkuu ni kuwaondolea Watanzania uwoga,
Watanzania wamesha shuhudia watu kupigwa Risasi na Polisi sio zaidi ya mara moja,
Watanzania Mabomu ya Machozi imekuwa kawaida kwao,
Watanzania kuwekwa Ndani na Polisi ni kawaida siku hizi,

Sasa Mkuu ujue baada ya muda fulani hawa Watu huwa na Ununda, yaani kuzoea manyanyaso na kujitoa thamani wenyewe na kujiona hawana umuhimu wa kuishi, sasa ikifikia hatua hiyo Mkuu ujue Vurugu au Vita ya ndani huwa iko jirani sana.

Kwa majibu yanayotoka kwa viongozi na matendo yake, sijui kama Watanzania wa hali ya Chini wataendelea kujiona wana thamani ya kujiita Watanzania na kujiona wana haki ya kuishi,

Siwezi kuyarudia yaliyosemwa, kila Mtanzania anayajua.
Chungeni sana kauli zenu Viongozi, Polisi Watanzania wanawaheshimu, sio kwamba wanawaogopa, chungeni sana Nguvu mnazotumia bila sababu, au kwa kutumwa na Watawala.

Asanteni,
Mungu ibariki tanzania
 
Back
Top Bottom