Baba Mchungaji, Mzee wa Upako, Embu anza na hawa.

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,047
2,000
Baba mchungaji, wiki hii umetangaza kiama cha kifo dhidi ya wale wanaochafua jina lako na huduma yako.

Embu kabla ya hao anza na maombi hayo dhidi ya hawa baba;

Embu anza na hawa wanaokatili maisha ya wanadamu wenzao kisa tu wanamtazamo tofauti na yao,

Embu anza na hawa waliowageuza wamachinga leo hii kuwa mafukara kule mwanza, kwa ukatili wa operesheni ya usiku mmoja,

Embu anza na hawa walioamua kuwafanya watanzania hawana midomo wala utashi wa kuongea mawazo yao na hivyo kutaka wawe mabubu daima ilhali wao wakimulikwa na kamera za TV kila uchao,

Embu anza hawa wanaowaweka wenzao sello bila sababu za msingi ilihali wao wakifanyiwa massage kule Mori na Mikocheni na kwingineko,

Embu anza na hawa wanaofunga watu viroba na kuwatumbukiza mto ruvu kwa jina la uhamiaji haramu,

Embu anza uonevu na ukandamizwaji unaolipeleka taifa hili kwenye laana.
 
Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,556
2,000
hao anaowaombea wafe, atakufa yeye atawaacha wazima kabisa. kila utapeli una mwisho wake.
 
Jozi 1

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
6,203
2,000
Baba mchungaji, wiki hii umetangaza kiama cha kifo dhidi ya wale wanaochafua jina lako na huduma yako.

Embu kabla ya hao anza na maombi hayo dhidi ya hawa baba;

Embu anza na hawa wanaokatili maisha ya wanadamu wenzao kisa tu wanamtazamo tofauti na yao,

Embu anza na hawa waliowageuza wamachinga leo hii kuwa mafukara kule mwanza, kwa ukatili wa operesheni ya usiku mmoja,

Embu anza na hawa walioamua kuwafanya watanzania hawana midomo wala utashi wa kuongea mawazo yao na hivyo kutaka wawe mabubu daima ilhali wao wakimulikwa na kamera za TV kila uchao,

Embu anza hawa wanaowaweka wenzao sello bila sababu za msingi ilihali wao wakifanyiwa massage kule Mori na Mikocheni na kwingineko,

Embu anza na hawa wanaofunga watu viroba na kuwatumbukiza mto ruvu kwa jina la uhamiaji haramu,

Embu anza uonevu na ukandamizwaji unaolipeleka taifa hili kwenye laana.
Eti baba mchungaji
Napita tu, ila hiyo kauli yako inahitaji "uhakiki"
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom