Baba mbaroni kwa kumchinja mwanawe

Nasisitiza tena, kabla ya kufunga ndoa msiishie kupima UKIMWI tu hebu muwapime na wanaume akili maana haya matukio yamezidi sasa!
 
MTOTO Bahati Mlelwa (3) amenusurika kifo baada ya baba yake mzazi kumjeruhi shingoni kwa kisu na kuutelekeza mwili wake kichakani.

Baba huyo, Halfan Mlelwa(28) mkazi wa kijiji cha Mnyagala katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga amethibitisha unyama huu na kusema mtuhumiwa anahusishwa pia na mauaji mengine ya kutumia mapanga maeneo mengine.

Alisema tukio hilo lilifanywa juzi saa 11:00 jioni kijiji cha Mnyagala wilaya ya Tanganyika. Ambapo baba huyo alimtelekeza akijua ameua. Akisimulia alisema mtuhumiwa aliachana na mke wake akiwa na ujauzito wa mtoto Bahati.

‘’Jioni ya siku hiyo ya tukio mtuhumiwa alifika kwa mke wake wa zamani ambaye hakuwepo akamchukua mtoto Bahati na kutokomea naye kichakani jirani na nyumba aliyokuwa akiishi mtoto huyo na mama yake akamuue,”alieleza.

Mtuhumiwa akiwa na mwanawe kichakani alichomoa kisu kibindoni akaanza kumchinja na kuondoka akiamini amemchinja na kumuua.

Inadaiwa mama wa mtoto huyo aliporejea nyumbani hakumwona mwanaye hivyo akaanza kumtafuta na kumkuta akiwa amezimia huku mwili mzima ukiwa umetapakaa damu.

Kamanda Kuzaga alisema opereshini ya jeshi la polisi inayoendelea wilayani humo dhidi ya watuhumiwa wa mauaji na uhalifu mwingine ilifanikisha kumnasa mtuhumiwa huyo haraka.

Alisema haijafahamika chanzo cha baba huyo kumfanyia unyama huo mwanaye ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi iliyopo mjini Mpanda kwa matibabu.

CHANZO: HABARILEO

Analeta swaga za Ibrahim kwa isaka sioooo
 
Huyu ni wa kunyongwa tu akapumzike kaburini vinginevyo atasababisha maafa zaidi katika jamii
 
Hii habari haijajitosheleza. Walijuaje kama ni baba wa mtoto ndio kahusika?! Kama hajakiri,nani alimuona kichakani akimchinja?!

Sent from my Infinix X650B using Tapatalk
Kisheria upo sahihi. Mahakama ndio itaamua
 
Hakuna sababu ya kuua na Kama ipo unaanzaje kumuua mtoto mdogo ambaye hata kujitetea hawezi,kupigana na wewe hawezi ?
Kama ni mwanaume wa shoka akatafute wanaume wa saiz yake wamuonyeshe kazi.Kuna kulogwa pia lakini uchawi unaweza kuhusika maana kwa mtu wa kawaida sio rahisi kufanya hlo tukio na jingine pia mzee huenda ana tatizo la akili.
 
Hii habari haijajitosheleza. Walijuaje kama ni baba wa mtoto ndio kahusika?! Kama hajakiri,nani alimuona kichakani akimchinja?!

Sent from my Infinix X650B using Tapatalk
Chanzo cha habari, Habari Leo
 
Hii habari haijajitosheleza. Walijuaje kama ni baba wa mtoto ndio kahusika?! Kama hajakiri,nani alimuona kichakani akimchinja?!

Sent from my Infinix X650B using Tapatalk
Hivi mkuu unaielewa kashogi wanayolishwa wauwaji wa aina hiyo wakiwa mikononi mwa polisi?

Kwanza huungamishwa ukweli wote pasina shaka penda asipende, kisha hizo danadana zake ndiyo huenda kuzifanyia mahakamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom