Baba Levo: Natamani nife wa kwanza kabla ya Diamond, akitaka lolote ntamfanyia. Wadau wamfananisha Baba Levo na Gigy Money

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
51,961
41,437
Wasalaam Wana jamvi.

Msanii Baba Levo ameweka wazi kuwa anatamani Mungu amchukue hata leo ili watoto wake walelewe na Diamond.

Baba Levo amesema hayo akieleza hisia zake baada ya Diamond kumlipia ada za watoto wake wawili wanao soma TUSIME SEC.

Baba Levo anasema anatamani Mungu amchukue hata leo kabla hajamchukua Diamond kwani Diamond ni muhimu hapa duniani kuliko yeye .... napia amesema yuko tayari kumfanyia chochote Diamond akimwambia...maana ni mtu muhimu sana kwake.

Hata hivyo wadau wengi wamekuwa wakimuona Baba Levo kama ni mtu aliye na matatizo ya akili hivi karibuni kiasi ambacho utofauti wake na Msanii Gigy Money ni mdogo sana na wengine wamekwenda mbali zaidi kumthadharisha Diamond kuwa makini na watu ya aina ya Gigy na Baba Levo ambao wanaweza kumponza zaidi kwani wamekuwa wakiropoka sana bila kujali wako watu na wana muingiza kwenye gharama sana.

Hata hivyo wadau wamemuomba Diamond kumpatia Baba Levo Daktari wa Magonjwa ya akili.
Wasalaam
 
Nilikua namkubal Sana zaman Siku hiz sijui kawaje, imagine kuwa na Baba kama Baba levo, mxieew, kuna umri mwingine kuwa chawa hata haipendezi, Sijui hana ndugu wa kumshauri , yani umaskin mbaya sana , tusomeshe tu watoto wetu
 
Usimlaumu hana tofauti na wengine wanaompa sifa Magu hadi Magu mwenyewe anashangaa, isipokuwa utofauti wao ni kwamba yeye anampa sifa diamond. Kila mtu anasifia anapopatia msosi. Utasikia waziri anasema tumshukuru Magu kwa mvua kunyesha ...
 
Kama wale Covid 19 wanavyomsifia Kamanda wa Anga hadi leo
Usimlaumu hana tofauti na wengine wanaompa sifa Magu hadi Magu mwenyewe anashangaa, isipokuwa utofauti wao ni kwamba yeye anampa sifa diamond. Kila mtu anasifia anapopatia msosi. Utasikia waziri anasema tumshukuru Magu kwa mvua kunyesha ...
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom