Baba kanumba amvaa mama kanumba baada ya kuvuruga utaratibu wa mirathi...

jozzb

Member
Jun 30, 2011
87
20
Baba mzazi wa Kanumba anaeishi Shinyanga ambae alishindwa kuja msibani kutokana na kuumwa, amezungumza na kusema kwamba sasa yuko tayari kuja Dar es salaam kushughulikia swala la Mirathi baada ya kudai kwamba mama mzazi wa Kanumba ambae yuko Dar ameanza kuharibu kuhusu ishu ya mirathi.

Amesema "Tutakaa kikao jumamosi kuteua msimamizi wa mirathi, mama ameteua kinyemela bila kunishirikisha.

Hilo swala nimelipinga Nimewasiliana nae kumuuliza kwa nini kafanya hivyo akawa ana jiuma uma tu. Kwa nini umeokota watoto na kuwadanganya danganya kikao cha kusimamia mirathi si tungekaa pamoja? akachukua watoto wangu walioko huko wasichana wawili lakini walipotoka kikaoni wakanipigia simu kwa sababu hawakuridhika"
 
Africans! Huyu si alikanwa na marehemu kabla hajakufa? Mirathi imempataje tena?
 
hili zee nalo bwana...yaani ujanani ulikuwa unakula maandazi ukasahau kuweeka mpunga wa kuja kutanulia akizeeka sasa unaanza kusumbua na mambo ya mirathi....hebu pumzika si unaumwa malaria wewe
 
Kwa nini wakati marehemu yu hai akulilia awe nae poa na kutokwenda uza story maagazetini kupata pesa?

Ana tamaa sana mzee huyu, mie nimechoka na story zake.
 
Watu wanapenda vya bure loh! Hata kama ni baba yake haipendezi kugombea mirathi ya mtoto ambaye akiwa hai hakuwa na time nae..
BTW naona sasa amepona presha,malaria na miguu..
 
Huyu mzee SK katika maisha yake alikua hampi chochote sasa naona amekuja na style nyingine ya kupata vitu vya marehemu. Me naona hizi sheria za mirathi zina mapungufu, haiwezekani mimi katika uhai wangu nisikupe hata senti
halafu nkishakufa uje kugombania mali zangu.
 
Mimi nasema na aje tu kufuatilia hizo mali,
hata kama Kanumba (R.I.P) alikuwa anampa kitu kidogo hawezi kukipata tena,
na kwa tabia zetu akina mama atajiona kana kwamba huyo mtoto alizaa mwenyewe.

Njoo tu kaka utaambulia chochote.
 
Mimi nimelea watoto pekee yangu
lakini siweze kamwe kuwazuia kumtunza father wao,

hata wanawake wenzangu msiwe na roho mbaya,
kila kitu tutakiacha duniani hatutaondoka navyo.

Huyu mzee SK katika maisha yake alikua hampi chochote sasa naona amekuja na style nyingine ya kupata vitu vya marehemu. Me naona hizi sheria za mirathi zina mapungufu, haiwezekani mimi katika uhai wangu nisikupe hata senti
halafu nkishakufa uje kugombania mali zangu.
 
Ninyi mnatafuta laana nyingine..... Baba bi baba hata kama aliact kama dume la nyani... sometimes akinamama nao wanachangia kuwaharibu sana watoto...watch out!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom