Baba HIV+, Mama HIV+: Je, Mtoto anaweza kuzaliwa salama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba HIV+, Mama HIV+: Je, Mtoto anaweza kuzaliwa salama?

Discussion in 'JF Doctor' started by Darwin, Sep 19, 2008.

 1. D

  Darwin JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Juzi kuna gazeti moja nimesoma kwamba watu wenye hiv huko Nigeria wanalazimishwa kuoana ili ongezeko la ukimwi lipungue.

  Kwanza ni jambo lakushangaza na kusikitisha kwamba watu wanalazimishwa kuoana, ila najiuliza je hao watu wana uwezo wa kuzaa watoto ambao hawana HIV?
   
 2. M

  Mama JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Mtoto anaweza kuzaliwa bila kuwa na virus iwapo mama mwathirika atawahi kliniki. Huko atapewa dawa zinazozuia maambukizo toka kwa mama kwenda kwa mtoto hasa wakati wa kujifungua.

  Baada ya mtoto kuzaliwa salama, inabidi mama achague either kumnyonyesha maziwa yake tu bila kumpa kitu kingine chochote hata maji ya kunywa hadi mtoto atakapo timiza umri wa miezi sita, au asimnyonyeshe kabisaaa.
   
 3. K

  Kungurumweupe JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 317
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Kwanza ni vizuri ieleweke kwamba, hakuna direct contact kati ya damu ya mama na ya mtoto kwa kipindi chote mtoto awapo tumboni mwa mama yake. Hii inaondoa uwezekano wa mtoto kupata maambukizi akiwa tumboni mwa mama yake au kabla ya kuzaliwa!

  Mtoto aweza kuambukizwa tu wakati wa kuzaliwa au baada ya kuzaliwa ikiwa hapatachukuliwa hatua za tahazari za kuzuia hilo!

  Ieleweke kuwa ngozi ya mtoto huwa ni very delicate wakati ule wa kuzaliwa kiasi cha kuruhusu uwezekano wa kupata michubuko kwa urahisi endapo kutakuwa na msuguano kati ya hii ngozi na kuta za njia ya uzazi!

  Kama njia ya uzazi haitapata vilainishi vya kutosha na ikawa ni ndogo kiasi cha kuchanika na hatimaye kutoa damu, na kama ngozi ya mtoto itakuwa na michubuko wakati wa kuzaliwa, basi mtoto anaweza kuambukizwa hiv wakati huu wa kuzaliwa!

  Kama mtoto atazaliwa bila maambukizi, basi anaweza kuambukizwa na maziwa ya mama yake kama tu huyu mtoto atakuwa na michubuko kwenye utumbo wake au kwenye njia yake ya chakula wakati wa kipindi kile cha kunyonya!

  Ili mtoto asiambukizwe kutokana na maziwa ya mama yake basi inabidi either anyonye maziwa ya mama yake pekee kwa muda wote wa utoto wake (muda wa kunyonya) na asipewe kitu kingine, au kama hilo haliwezekani basi atumie maziwa ya ng'ombe au artificial pekee na kamwe asichanganye na maziwa ya mama! Hii ni kwa sababu maziwa ya ng'ombe au yale artificial huwa yana kemikali ambazo zina nguvu kali inayoweza kusababisha michubuko kwenye utumbo laini wa mtoto! Hivo mtoto akipewa haya maziwa yenye kemikali yatakayosababisha michubuko kwenye utumbo wake laini halafu akanyonya maziwa ya mama yake mwenye hiv, basi kuna uwezekano wa mtoto huyu kupata maambukizi kwa kuwa utumbo wake tayari utakuwa na michubuko iliyosababishwa na maziwa haya yenye kemikali!

  Hivo basi, kama mtoto amezaliwa na wazazi wenye hiv, na ili mtoto wao asipate maambukizi ya hiv basi inabidi mama yake afanye au achague kitu kimoja tu kati ya hivi viwili vifuatavo:

  1. Mama amnyonyeshe mtoto wake mwenyewe kwa muda wote wa kunyonyesha bila kumpa kitu kingine au kumchanganyia maziwa yoyote yale, yawe ya ng'ombe au artificial!

  2. Kama hilo la kwanza hapo juu haliwezekani, basi mtoto apewe maziwa ya ng'ombe au yale ya artificial pekee bila kuchanganya na yale ya mama yake kwa muda wote wa utoto wake (kipindi cha kunyonya)!
   
 4. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ...Mnh!!! Vipi tena mazee??? Uko sawa kweli upstairs!!???
   
 5. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Tatizo juu ya matatizo !!!!!!!
   
 6. Willy

  Willy Member

  #6
  Sep 20, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 78
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Dear
  Lets be careful here what kungurumweupe said above is not totally true. Mtoto akiwa kwenye tumbo la uzazi anaweza kuambukizwa virusi vya ukimwi. Hii inategemea the stage of the mother disease, degree of immunodeficiency as indicated by levels of CD4 na mambo mengine. Ingawa the biggest proportion of children get infected during delivery. As an HIV expert I enjoy following up what is written in JF, but tusiende mbali sana tukadangaya umma, hasa kwenye jambo kama maambukuzi ya HIV.
  Asante Willy
   
 7. kkiwango

  kkiwango Senior Member

  #7
  Sep 20, 2008
  Joined: Aug 27, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Uko sahihi Willy.Lakini pia kama mama akipata therapy mapema basi anaweza mkinga mtoto asipate HIV wakati bado yuko tumboni.
   
  Last edited: Sep 20, 2008
 8. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2008
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asanteni sana wana JF mliotoa mafunzo haya katika topic hii. Sometimes mimi huwa naulizwa maswali yanayohusika na ugonjwa wa ukimwi nabaki kubabaisha jibu bila kuwa na solid facts.
  Kuna wakati mwana mama mmoja aliniuliza....Je kama ukifanya mapenzi na mwanaume mwenye ukimwi ambaye ni "Carrier" wakati wote wawili mkiwa mmelewa....utaambukizwa ugonjwa huu?
  Mimi nikamwambia Ndio ataambukizwa.
  Je wana JF....mnasemaje katika swali hili?
   
 9. D

  Darwin JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Si wanasema kwamba manii ya mwanaume yanabeba sana virusi vingi? sasa huyo mtoto siatakua keshambuakizwa tayari hata kabla yakua mkubwa tumboni?

  Au kinachoingia kwenye yai la kike ni zile mbegu tu sperm cell bila ule umajimaji unaobeba virusi vingi?

  Haya madokta kazi kwenu.
   
 10. K

  Kungurumweupe JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 317
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Dear Willy,

  Please don't mislead people!

  What I said is totally true, though you can add some other facts!

  Question: What you mean by your statement that my explanation is not totally true?! Can you please clarify so that we don't confuse people?!
   
 11. D

  Darwin JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kungurumweupe bado kuna hili swali hapa

   
 12. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2008
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Darwin, ni kweli kinachoungana ni ile mbegu yenyewe sperm na ovum, ambazo hazina virusi- kwa hiyo kitoto (ki-zygote) kinachotokea kiko free of virus. Maambukizi yanaweza kutokea kuanzia wakati wa ujauzito (sio kama mchangiaji mmoja aliyesema haiwezekani kuambukizwa kwa sababu damu hazigusani)- kuna conditions kibao ambazo zinaharibu intergrity ya placenta kwa hiyo vijidudu vingi, HIV, malaria, n.k vinaweza kuingia upande wa mtoto, ingawa ni kweli maambukizi mengi yanatokea wakati wa kujifungua.
  Kuna njia nyingi sasa za kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto; sasa hivi 'nji' zilizoendelea ni kama hawana tena tatizo hilo lakini kwetu TZ bado tunajikongoja.
  Tutafika, taratibu!
   
Loading...