Baba ateketeza familia yake mamba korikie Moshi.....


Sokomoko

Sokomoko

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2008
Messages
1,918
Likes
24
Points
135
Sokomoko

Sokomoko

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2008
1,918 24 135
Maafa makubwa yamekikumba kijiji cha Mamba Kokirie wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro baada ya mtu mmoja kumuua mama yake mzazi na watoto wake wawili kwa kuwakata na kuwachinja kwa panga.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea juzi usiku katika kijiji hicho likiacha vilio na simamanzi baada mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Meckimelan Mamkwe (45) aliamua kukatisha uhali wa familia yake.

Mashuhuda wa tukio hilo waliozungumza wamesema mtekelezaji wa mauaji hayo alifika nyumbani anakoishi na mama yake huyo aliyetajwa kwa jina la Christina Ronald (65) na kukuta akila chakula cha jioni akiwa na wajukuu zake wawili.

Ghafla alianza kumshambulia mama yake mzazi kwa kumtata na panga na baada ya kuona amefariki alianza kuwakatakata kwa panga watoto wake wawili waiotambuliwa kwa majina ya Emmanuel Meckimelan (12) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Kokirie na mdogo wake Ezekiel Meckimelan (8) anayesoma darasa la pili kwenye shule hiyo.

Baada ya kusababisha mauaji hayo, kijana huyo alilala ndani ya nyumba hiyo pamoja miili ya marehemu hao asijue nini cha kufanya hadi jana asubuhi ambapo ndugu na majirani walifika katika nyumba hiyo na kubaini mauaji hayo. Wananchi wenye hasira kali walianza kumshambulia kwa silaha mbalimbali Meckimelan na kumuua kwa kumchoma moto.

Miili ya marehemu hao wote wanne ilichukuliwa na polisi jana na kupelekwea Hospitali ya Kilema Marangu ambako hadi sasa imehifahdiwa ikisubiri uchunguzi kabla ya mazishi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko,amethibitisha tukio hilo lakini hakuwa tayari kuelezea kwa undani zaidi kwa kile alichodai hakuwa na taarifa kamili za tukio hilo na ameahidi kutoa taarifa baadaye.

Source: RFA.
http://www.wavuti.com/habari.html#ixzz15kVUxFSR
 

Forum statistics

Threads 1,237,487
Members 475,533
Posts 29,290,450