Baba Askofu Mwamakula: Kutenganisha dini na siasa haiwezekani Fatuma Karume alipaswa kujieleza kabla ya kutolewa uwakili wake Bara

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Ameandika Baba AskofuEmmaus Bandekile Mwamakula

Mheshimiwa Fatma Karume (pichani) kama kweli umeondolewa kuwa miongoni mwa Mawakili katika Mahakama Kuu Tanzania Bara pasipo kupata nafasi ya kuhojiwa, kuhojiwa, kushitakiwa, kuonywa, kusikiliza na kusikilizwa, basi hayo yatakuwa ni matatizo makubwa katika mfumo wa Mahakama zetu au matatizo katika tafsiri ya kile tunachookiita uhuru wa kuhoji, kuhojiwa, kujieleza, kujitetea, kusikilizwa na kutoa maoni. Mungu mwenyewe aliasisi kanuni hii pale katika Bustani ya Edeni ambapo pamoja na makosa yao, lakini Mungu aliwapa Adam, Hawa, na "Nyoka" nafasi ya kuhoji, kuhojiwa, kutoa maoni, kujitetea na kusikilizwa. Kanuni hii ambayo kila mwanadamu huzaliwa nayo huitwa "Natural Justice."

Tunawaomba sana Mahakimu na Majaji katika Mahakama zetu waheshimu sana na kuilinda kwa gharama zote kanuni hii ya "natural justice". Wao ndio pekee ambao Mungu amekasimisha kwao mamlaka ya kutoa haki katika jamii kwa njia ya kuitunza, kuienzi na kuihifadhi kanuni hii.

Ninakuombea ili Mungu akupe utulivu, uvumilivu, na hekima katika kutafakari ni kwa namna gani utaweza kupata haki yako ya kuhoji, kuhojiwa, kusikilizwa, na hata kujitetea (natural justice).

Ninaamini tukio hili la kwako litaleta changamoto yenye kujenga katika mfumo wa Mahakama zetu kupitia tafakuri za kisheria na mantiki (logic) zitakazofanywa na wanasheria na wadau wote wa sheria, haki na katika nchi hii.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani

1569475028084.jpeg
 
Hili ni suala la kisheria pengine ingekuwa kuwa busara zaidi kwetu sisi mbumbumbu kuelewa zaidi kama tutaeleweshwa usajili,kanuni,taratibu zinazohusiana na usajili, mwenendo pamoja na kusimamishwa uwakili n.k.
 
Back
Top Bottom