Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza: Hivi CHADEMA wamejitoa au wametolewa?

Alvin A.

JF-Expert Member
Oct 14, 2016
2,868
3,624
Ameandika Baba AskofuKalikawe Lwakalinda Bagonza

#TUJIULIZE ZAIDI

1. Hivi Chadema wamejitoa au wametolewa?

2. Hivi Chadema wamesusa au Wamesuswa?
3. Hivi Chadema Wameacha au Wameachwa?

Wasomaji msinihukumu bila kunisikiliza. Maswali haya ni ya msingi kwangu.

- Media haiko na wapinzani
-Msajiri hayuko na wapinzani
-Mahakama haiko na wapinzani
-Vyombo vya dola haviko na wapinzani
-Viongozi wa dini hawako na wapinzani
-Asasi za kiraia haziko na wapinzani
-Bunge haliko na wapinzani
-Tume ya uchaguzi haiko na wapinzani
-Wazee mashuhuri hawako na wapinzani
-Wana taaluma hawako na wapinzani
-Wasimamizi wa chaguzi hawako na wapinzani
-Walinzi wa amani hawako na wapinzani
-Waajiri hawako na wapinzani
-Mashirika yasiyo ya kiserikali hayako na wapinzani
-Wapinzani hawako na wapinzani.
-Hata mimi siko nao, naandika kujipendekeza kwao!

Hii inaitwa unyanyapaa (stigmatization). Kwa hiyo walichokifanya, kwa maoni yangu:
Hawakujitoa, wametolewa
Hawakususa, wamesuswa
Hawakuacha, wameachwa

Kimya cha makundi yote hapo, tafsiri yake ni kuwasusa, kuwaacha, kuwatoa katika mchakato wa kidemokrasia, na kupuuza madai yao. Walio wengi, wanaona ni salama ama kukaa kimya au kuwalaumu na kuwakejeli.
Watu, kundi au mtu aliye katika hali hii ya kuachwa, ni hatari kwa jamii, ni hatari kwa nafsi yake mwenyewe na mara nyingi hujikinai.

Baba wa Taifa aliwahi kusema, "Amani ni tunda la haki. Palipo na amani kuna haki na palipo na haki kuna amani. Tanzania tuna amani lakini haina maana kuwa haki inatendeka. Kinachotokea ni kuwa, watu wana matumaini kuwa haki itatendeka siku moja. Watu hawa siku wakikata tamaa kuwa haipo, yatatokea maafa makubwa sana. Viongozi wana jukumu la kuhakikisha matumaini ya watu kupata haki hayapotei".

Dumisha Uhuru na Umoja,
Wake kwa waume na watoto,

Mungu Ibariki Tanzania.

75264855_1578359772305508_5669511672880955392_n.jpg
 
Walitangaza kuwa wamejitoa au wewe ndio mmewatoa
Sisi tunasikiliza hoja yao kuwa wamejitoa.

State agent
 
Sioni tatizo kwa CDM kujitoa, ilibidi CCM waje na tamko kwamba wapinzani wameamua kumuunga mkono Jiwe, na mpinzani wako akikukimbia maana yake amekuogopa unatakiwa usherehekee ushindi, lakini imekuwa kinyume CCM wanalalamika na kumlaumu Mbowe, Kwanini?
 
Back
Top Bottom