TANZIA Baba Askofu Jimbo Katoliki Tanga, Anthony Banzi afariki dunia akipatiwa matibabu Hospitali ya Muhimbili

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
5,520
2,091
Kwa Masikitiko makubwa napenda kuwataarifu kuwa Askofu wa Kanisa Katoliki Tanga Anthony Banzi afariki Dunia alfajiri ya leo Muhimbili National Hospital. RIP Askofu Banzi.

Pumzika kwa Amani Baba Askofu Anthony Banzi

Raha ya milele umpe eeh BWANA Na mwanga wa milele umuangazie

Marehemu apate rehema kwa Mungu apumzike kwa Aman.

Amina

Banzi.jpg


Pia soma > Askofu Mhashamu Anthony Banzi: Tuwaheshimu marehemu, tusiwafunge kwenye viroba

Taazia.jpg

HISTORIA YA ASK. ANTHONY BANZI KWA UFUPI:
_____________________________________
Imenakiriwa na Kuhaririwa na Mwl. J. A. Sabuni
________________________________

Anthony Banzi (amezaliwa Mangoja, Parokia ya Tawa, Morogoro 28 Oktoba 1946) ni askofu Mkatoliki nchini Tanzania.

Aliwekwa wakfu na Kardinali Polycarp Pengo mwaka 1994. Tangu mwaka huo, ni askofu wa Jimbo la Tanga.

MAISHA YAKE:

Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Lukenga. Mwaka 1960 alijiunga na Seminari ndogo ya Mt. Peter, Bagamoyo na baadaye Seminari ndogo ya Mt. Charles huko Itaga kuanzia mwaka 1965 hadi 1967.

Mwaka 1968-1969 alijiunga na Seminari Kuu ya Kibosho kwa masomo ya Falsafa na baadaye Seminari kuu ya Kipalapala kwa masomo ya Teolojia kuanzia mwaka 1970 hadi 1973.

Alipewa daraja takatifu ya upadre tarehe 29 Julai 1973.

Alifanya kazi kama paroko msaidizi katika parokia za Mlali, Msongozi, Mtombozi, Matombo na kama Paroko katika Parokia ya Maskati.

Mwaka 1976 alifanya kazi kama mhasibu mkuu wa Seminari kuu ya Ntungamo, Bukoba.

Miaka 1976 - 1981 alikwenda Austria (Ulaya) kwa masomo zaidi, ambapo alitunikiwa shahada ya udaktari (Ph.D).

Kuanzia mwaka 1981 hadi 1982 alikuwa Chaplain wa Hospitali ya Turiani na pia paroko wa parokia ya Mandera.

Miaka 1981 - 1985 alikuwa Mhasibu mkuu wa Jimbo Katoliki la Morogoro.

Miaka 1985 - 1987 alikuwa Chaplain wa Sekondari ya Bigwa, Morogoro.

Miaka 1988 - 1991 alikuwa Gombera wa Seminari kuu ya Ntungamo.

Mwaka 1992 Padre Anthony Banzi aliteuliwa kuwa Gombera wa Seminari kuu ya Kibosho, Moshi, ambapo alifanya kazi mapaka alipoteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo katoliki la Tanga tarehe 24 Juni 1994 na kuwekwa wakfu tarehe 15 Septemba 1994.
 
Kwa Masikitiko makubwa napenda kuwataarifu kuwa Askofu wa Kanisa Katoliki Tanga Anthony Banzi afariki Dunia alfajiri ya leo Muhimbili National Hospital. RIP Askofu Banzi.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele Umwangazie, Pumzika kwa Amani, Amina.
 
Back
Top Bottom