Baba ashikiliwa kwa tuhuma za kumkanyaga mtoto wake kwa gari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba ashikiliwa kwa tuhuma za kumkanyaga mtoto wake kwa gari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Apr 13, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  MKAZI wa Makumbusho, Gharibu Ayubu (35) anashikiliwa kituo cha polisi Kinondoni jijini hapa kwa kumkanyaga kichwani kwa gari lake hadi kufa, mtoto wake, Ayubu Gharibu aliyekuwa na mwaka mmoja na miezi mitano wakati alipokuwa akirudi nyuma ili kutoka katika nyumba yake wakati akitaka kuelekea Sinza.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elius Kalinga aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 2.00 asubuhi katika nyumba ya Gharibu iliyopo barabara ya New Bagamoyo eneo la Makumbusho katika Wilaya ya Kinondoni.

  Kalinga alisema tukio hilo lilitokea baada ya mtoto huyo kutaka kwenda na baba yake asubuhi hiyo, lakini baba yake akamkabidhi kwa makewe ambaye alirudi naye ndani, lakini baada ya muda mtoto huyo alitoka tena nje na kulifuata gari hilo bila mama yake kujua.

  Alisema mtoto huyo alipolifikia gari hilo aina ya Toyota Folona alikwenda kusimama nyuma yake na Gharibu alipokuwa akirudi nyuma ili aweze kupata mwelekeo wa kutoka katika nyumba yake kuelekea Sinza ghafla akamkanyaga mtoto huyo kichwani na kumsababishia kifo kwa kuwa aliumia sana kichwani.

  Kamanda Kalinga alisema Gharibu anashikiliwa na jeshi lake na atafikishwa mahakamani huku uchunguzi wa kesi yake ukiendelea kufanyika.

  Katika tukio jingine, Kamanda Kalinga alisema maiti ya mwanaume aliyefahamika kwa jina la Yusuph Mwinchande (36) ilikutwa ikiwa kandokando ya makaburi huku pembeni kukiwa na bomba la sindano linalosadikiwa kuwa na dawa za kulevya.

  Kalinga alisema maiti hiyo ilikutwa juzi saa 9.00 jioni na chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika, uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

  Katika tukio jingine, Mkazi wa Handeni Tanga, Shola Mwangomo (37) alifariki dunia akiwa ndani ya basi la Kampuni ya Sai Baba akitokea nchini Msumbiji pamoja na rafiki yake, Obed Mwakihaba (37) ambaye ni mkazi wa Kihonda Morogoro.

  Kamanda wa polisi Mkoa wa Temeke, David Sime alisema Obed alitoa taarifa juu ya kifo hicho baada ya kufika jijini Dar es Salaam ambapo alisema yeye na rafiki yake huyo ambaye sasa ni marehemu walitoka nchini Msumbiji katika kitongoji cha Montepwesi kijiji cha Nanupo, Aprili 9 saa 11.00 alfajiri lakini walipofika Somanga katika daraja la Mkapa rafiki yake akafariki dunia.

  Hata hivyo Kamanda Sime alisema kuwa Obedi alidai kuwa rafiki yake huyo kabla hajafariki alikuwa akiumwa malaria. Maiti imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Temeke kwa uchunguzi.
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=19163
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,396
  Likes Received: 22,273
  Trophy Points: 280
  Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu.
   
 3. B

  Bibi Kizee JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  inasitikitisha! mhh mwili wote umeishiwa nguvu jamani! mungu awape faraja wafiwa
   
 4. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  So sad............
   
 5. senator

  senator JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Inauma sanaa nimeisikia jana hii naona wakina kibonde waliongezea sijui..eti jamaa aliondoka pasipo kujua kama amegonga mpaka alipotoka nje mkewe ndo akakuta mtoto kafariki nje...
  All in All inauma kweli..RIP mtoto Ayubu Gharibu
   
 6. b

  bwanashamba Senior Member

  #6
  Apr 13, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  du poleni sana ndugu zangu
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hii ndio maana kuna neno linaitwa AJALI.
  Wengi sana wamekutana na kadhia hii.
  Poleni sana wafiwa. Lilikuwa haliepukiki.
   
 8. b

  bwanashamba Senior Member

  #8
  Apr 13, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  du inauma sana lakini ila mengi watazungumza lakini ni ajali tu kama ajli
  zingine
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Hii inauma!
   
 10. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #10
  Apr 15, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,606
  Likes Received: 3,906
  Trophy Points: 280
  Duh! poleni wafiwa , pole baba wa mtoto,

  wanasheria hapa mfiwa si atashinda kesi au inakuwaje?

  dah! imenihuzunisha sana
   
Loading...