Baba anayetafuta heshima; hujenga heshima ya "ubaba" wake, siyo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba anayetafuta heshima; hujenga heshima ya "ubaba" wake, siyo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Xuma, Nov 11, 2011.

 1. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hii nimeipata katika WANABIDII GOOGLE GROUP nikaona ni vyema niilete huku tushee na kupanuana mawazo kwa wale wasiotembelea hiyo group na kuweza kuchangia pia!  BABA ANAYETAFUTA HESHIMA; HUJENGA HESHIMA YA "UBABA" WAKE, SIYO?

  Kama binadamu; wakati mwingine hujikuta nikicheka peke yangu! Kwa nini nicheke peke yangu? Inawezekana; kwa kuwa binadamu wote ni "wendawazimu" isipokuwa tunatofautiana kiwango cha wendawazimu! Huu ni ukweli wa kifalsafa na kisaikolojia (kama alivyothibitsha Sigmund Freund). Kwa mfano; tazama, mtoto mchanga na au hata baadhi ya watu wazima wanavyoweza "kuonja" makamasi yanayotoka puani mwao au hata kumeza "makohozi" na kuonja "ladha" yake. Au, wakati mwingine mtu mzima anaweza kunusa "choo" chake katika kuhakiki kuwa "mkono' wake ni safi hat baada ya kuusafisha kwa maji na sabubi!

  Huu ndio ule "wendawazimu" usiyoepukika; au fikiria pale mtu mzima anapovua nguo "zote" kisha akajitazama kwenye "kioo" na halafu "akajichesha na au kuchekelea...unaweza kudhani kwamba ni mzima, siyo?!

  Ni sehemu ya "wazimu" wa asili alozaliwa nao binadamu! Nimeanza na "mchokoo" wa kifalsafa katika kujenga hoja ya BABA (MWENYE NYUMBA) ANAPOTAFUTA HESHIMA. Vypvyote viwavyo; baba anayetafuta heshima lazima aonyeshe kwamba ana HESHIMA juu ya kuheshimiwa kwake! Hawezi kupewa heshima kama "hajiheshimu" kwenye "uongozi" wa nyumba, siyo? Hapa naomba tuangalie sifa za heshima za BABA (MWENYE NYUMBA):

  1. Awe BABA (wa ukweli) siyo "shoga"...
  2. Awe na akili ya kuongoza nyumba yake kwa jinsi ya uongozi wa kuielekeza nyumba (mke na watoto) juu ya maisha yenye murua, saada na staha...
  3. Awe jasiri wa kupambana na mazingira yanayotishia "uhai" wa nyumba yake...
  4. Awe na akili na uwezo wa kutatua matatizo ya "nyumba" yake kwa uhuru, haki na usawa kwa kuzingatia utashi wa watu wake (mke na watoto)...
  5. Awe mwanamume mwenye akili na uwezo wa kimaarifa na ustadi wa hali ya juu katika kujenga mustakabali wa "nyumba" na watu wake (mke na watoto)...

  Haiwezekani kwa BABA kupewa heshima kama sifa hizo muhimu hana! Hata BABA huyo akitumia "nguvu" za kipolisi hawezi kupewa heshima kwa kuwa ameonyesha udhaifu kwenye "nyanja" zote na ithibitisho unaonyesha kwamba BABA ameshindwa kujenga heshima, siyo?!

  Angalia kwa BABA (huyu) anayedai heshima...ana sifa hizi zenye kuchusha na kushangaza:

  1. Ni shoga, badala ya kuonyesha "makali" ya ubaba wake anashabikia "ushoga" hata wenzake wanamuona "shoga"...
  2. Nyumba yake inayumba na hali ya watu wa nyumbani kwake (mke na watoto) ni mbaya hata anashindwa kuwatatulia shida na taabu zao...
  3. Ameshindwa kupambana na mfumo wa maisha yanayotishia ustawi wa nyumba yake (kama mke na watoto wake basi wanalelewa na BABA MLEZI)...
  4. Ameishiwa akili na uwezo wa utatuzi wa "nyumba" yake anasubiri muda wake uishe amtaliki mkewe na awatelekeze watoto wake kwa BABA MLEZI...
  5. Amewaachia mke na watoto wahangaike wenyewe katika kujenga mustakabali wa "nyumba".... Huyu ndiye BABA anayehitaji heshima! Ebo...! Heshima gani awezaye kupewa BABA wa aina hii?

  Au kwa kuwa yenye amepewa "ridhaa" kwa kule kuwa na mke na watoto? Haiwezekani kuwa na baba aina hii, siyo? Kama anataka heshima anatakiwa atimize wajibu wake kama BABA WA UKWELI mwenye maarifa, ujuzi na maadili ya kulea "nyumba" yake kwa ujenzi wa watu wake (mke na watoto).

  Hili si fumbo la kifalsafa; isipokuwa ni jinsi BABA anavyotakiwa awe na kwa mfano wake ni sawa na "nchi" au taasisi au jamii ya watu. Mtu anayepewa "dhima" ya kuwaongoza watu lazima awe mwenye akili na uwezo wa kuwaongoza watu hao kutafuta "suluhisho" za matatizo yao kiuchumi, kijamii na kisiasa! Kiongozi (kama BABA) lazima aonyeshe ukomavu katika kudadavua masuala "magumu" yanayohitji utumizi wa "kichwa" makini ili kunyoosha njia ya ujenzi wa mustakabali wa maendeleo endelevu ya watu na miundombinu. KAZI NI KWAKO!

  BABA ASIYEWAJIBIKA NA ASIYEKUWA NA UWEZO WA KUTATUA MATATIZO YA WATU WAKE NI BABA-JINA (HANA MAANA) NA HAFAI! BABA (MJINGA) HAWEZI KUPEWA HESHIMA; HATA AKITUMIA "NGUVU" ZA JESHI NA POLISI...!


  Source: Wana bidii
  http://groups.google.com/group/wanabidii/browse_thread/thread/18066cb4b46aae7d

  BY
  Bakari M Mohamed, BBA[PLM], CPSP[T], MSc (PSCM)
  1.Procurement and Supply Chain Specialist, Consultant, Researcher and Trainer in Procurement Contracts Management
  2. Doctor of Alternative Medicines [DAM] & Natural Healing Therapist
  Department of Procurement and Logistics Management
  Mzumbe University Box 6
  Tel (Office): + 255 23 2604381/3/4
  Mobile : + 255 713 593347
  MZUMBE, Tanzania.
   
 2. Bakari Maligwa

  Bakari Maligwa Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ..Kuwa BABA wa ukweli ni kazi! Lazima "unowe" bongo..uache starehe na sherehe zisizokuwa na msingi ujenge familia yako, siyo? Leo tunamuangalia BABA (ambaye ndio kiongozi wa familia) anashindwa kutatua tatizo sugu la "uchumi wa kaya" hadi kaya yetu inayumba utafikiri ni kaya inayoendeshwa na "mama" peke yake!

  Hata kama; kuna akina mama peke yao (wanaoendesha familia zao na mambo yanaenda vema) kama ilivyo kwa Liberia kwa Mama Hellen Johnson Sirleef (ameweza)..sasa tatizo nini kwa Baba (huyu wa hapa kwetu) au? Sidhani kama tunaweza kusema sana...! Inatia wasiwasi, siyo?
   
Loading...