kamati
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 240
- 109
Habari ndugu zangu mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28 nimeajiliwa hapa kwa mda wa mwaka mmoja na nilibahatika kuoa miezi minne iliyopita kiukweli kipato changu ni kidogo sana changamoto inayonikuta ktk ndoa ni kuwa baba mkwe anamlazimisha mke wangu asaidie kwao kwa kuomba sukari nguo za wadogo zake na hata pesa ya kulimia kitu ambacho mke wangu hana kazi. Na mpaka juzi baba mkwe aliomba 60000 ya kulimia nikajipiga piga nikamtumia 30000 baba kajibu sasa hii pesa gani kaanza kulaumu sana mpaka ikafika hatua naona ndoa yangu inaanza kupata wakati mgumu mke wangu kutwa kanuna kwa kunilaumu sitaki kusaidia wazazi wake