Baba anapowatisha wanae...! Je ni kuwataadhalisha au kuwakatisha tamaa ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba anapowatisha wanae...! Je ni kuwataadhalisha au kuwakatisha tamaa !

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by EL MAGNIFICAL, May 1, 2012.

 1. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwanza habari zenu wakuu !

  Nianze moja kwa moja na mjadala, naamini wengi wetu tumeshuhudia sherehe hii ya wafanyakazi, tumeshuhudia jinsi wafanyakazi walivyoonesha kukata tamaa na hali halisi ya nchi inavyokwenda pamoja na yote pia wametuwakilisha vizuri watanzania kwa kauli mbiu isemayo "MSHAHALA KIDOGO, KODI KUBWA, MFUMUKO WA BEI NI PIGO KWA WAFANYAKAZI"

  Pamoja na haya yote mh. Jk alipigilia msumali kwa kusema kuwa amefulahishwa naa hotuba ya ndg. N. mgaya(katibu mkuu tucta) kwa kutambua mfumuko wa bei si tatizo la serikali bali ni ongozeko la bei ktk mafuta (disel) ambapo serikali yetu inategemea sana mafuta ktk shughuli mbali mbali za udhalishaji, lakini hakuishia hapo aliendelea kusema mwezi wa 7 (july) kuna hati hati hali ikawa mbaya zaidi kwa kuwa iran ikiwa kama mdau wa usambazaji wa mafuta duniani "WAKUBWA" wanaweza wakaiwekea vikwazo hivyo ikiwa kama nchi ya pili kwa utoaji wa mafuta duniani, nishati hiyo Upatikanaji wake unaweza kuwa mgumu kidogo na inaweza ikaongezeka bei mara dufu na kufanya mfumuko wa bei nchini kuongezeka zaidi.

  Lakini hakusema pia wana mipango gani madhubuti ya kuzuia jambo hilo ambalo limelalamikiwa sana na wafanyakazi.
  Je kama Rais ndiye aliyesema hivi mbele ya watu wanaotaka mfumuko huu wa bei uishe yeye anasema tujiandae mwezi wa july unafikili anatupa picha gani ! Kukata tamaa au tuchukue jitahada nyingine zozote za kujinusuru !

  Nikutakie kazi njema mh. Rais na serikali yako yote.

  Pia niwatakie maandalizi mema watz wenzangu ktk kuupokea mwezi july.
  Nawasilisha.
   
 2. m

  mama-lokatare Member

  #2
  May 1, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MUNGU amsaidie Rais wetu katika kipindi hiki kigumu.
   
 3. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2012
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Namhurumia sana Mfanyakazi wa nchi hii!
   
Loading...