Baba anafanya maendeleo ya vitu wakati sisi wanafamilia tunaishi maisha magumu

Habari wadau,

Baba ni muda mrefu tangu aoe kwa hiari yake amekuwa akifanya mabadiliko ya maendeleo ya vitu na si kwa sisi wanafamilia.

Watoto hatuli milo ya kueleweka maisha magumu ila kila siku ni ujenzi wa nyumba na matumizi ya kujifaharisha.

Sasa tunadaiwa deni kubwa bila kujua tutalilipaje juu ya matumizi haya.

Tatizo kubwa ni baba kutaka pongezi za lazima kwa majukumu ambayo ni lazima afanye pale nyumbani.

Tumsaidieje baba yangu?
hapo mama inabidi acheze na kufunga hat trick bila hivyo dakika 90 itakuwa bila.
 
Jisaidie mwenyewe , huwezi kumlalamikia mzazi wako kwa maendeleo anayoyafanya huku ukililia chakula wakati una akili ya kutumia JF na kuweka bando ,, maisha yako yatakuwa ya ajabu kuliko unavyofikiri , naombea mzee wako akaze Uzi mpaka utakapopata akili

Mkuu wewe utakuwa ni lumumba fc, bisha, siyo kwa uelewa huu wa mada
 
Baba anajua kua hamuwezi kufa na njaa kwasababu kwanza ardhi ya kutosha ya kulima ipo na watoto mtaitumia ipasavyo kuzalisha mahitaji ya nyumbani na hata ziada

Anachokifanya ni hivi, huko unakosema anapeleka rasilimali za familia ili kuleta maendeleo ni kwamba anakutayarishieni nyie watoto wake, wajukuu zake ambao ni watoto wenu nyie, vitukuu na vilembwe urithi wa kudumu
Hii ni roho mbaya tu
Yani wewe uishi kama mateka ili vitukuu usivovujua vije kula bata?
 
Mwishowe mpaka baba amalize hizo nyumba mtakuwa mmekufa kwa udumavu. Muombeeni baba yenu.
Ashauriki. Alisema familia aliipata yeye mwenyewe bila ya kusaidiwa. Kuhusu utendaji wake, kasema tusijusumbue maana hata malaika wanamkubali na ataweza siku kupewa chance ya kuongoza malaika .
 
Halafu huyu baba ana nyumba zake mbili moja ipo kijijini alipotoka nyingine hii ya hapa mjini anapoishi. Hizi nyumba anazipendelea sana yaani kila siku anaziboresha, imagine ile nyumba ya kijijini hata wapenzi wa mpira hakuna lkn amefunga dstv!?
Amepeleka na banda la sport pesa
 
Habari wadau,

Baba ni muda mrefu tangu aoe kwa hiari yake amekuwa akifanya mabadiliko ya maendeleo ya vitu na si kwa sisi wanafamilia.

Watoto hatuli milo ya kueleweka maisha magumu ila kila siku ni ujenzi wa nyumba na matumizi ya kujifaharisha.

Sasa tunadaiwa deni kubwa bila kujua tutalilipaje juu ya matumizi haya.

Tatizo kubwa ni baba kutaka pongezi za lazima kwa majukumu ambayo ni lazima afanye pale nyumbani.

Tumsaidieje baba yangu?
Nafanya mambo ya msingi kwanza baadaye mtaishi kama wafalme wanangu ,,,,lakini mkiona vipi kufeni tuu
 
Halafu huyu baba ana nyumba zake mbili moja ipo kijijini alipotoka nyingine hii ya hapa mjini anapoishi. Hizi nyumba anazipendelea sana yaani kila siku anaziboresha, imagine ile nyumba ya kijijini hata wapenzi wa mpira hakuna lkn amefunga dstv!?
 
Umizwa kichwa uone namna gani siku moja utajitegemea.

Si bora hata mnakula,,,,mi ningekulaza njaa siku mbili ujielewe.

Work up!!
 
Back
Top Bottom