Baba anafanya maendeleo ya vitu wakati sisi wanafamilia tunaishi maisha magumu

Jun 5, 2019
43
61
Habari wadau,

Baba ni muda mrefu tangu aoe kwa hiari yake amekuwa akifanya mabadiliko ya maendeleo ya vitu na si kwa sisi wanafamilia.

Watoto hatuli milo ya kueleweka maisha magumu ila kila siku ni ujenzi wa nyumba na matumizi ya kujifaharisha.

Sasa tunadaiwa deni kubwa bila kujua tutalilipaje juu ya matumizi haya.

Tatizo kubwa ni baba kutaka pongezi za lazima kwa majukumu ambayo ni lazima afanye pale nyumbani.

Tumsaidieje baba yangu?
 
Majirani zako unaowaona wana maisha mazuri na maendeleo ni kwa yale unayoyaona kama Nyumba, TV, Gari nk. Sio kwa vile walivyovila maana mla ni mla leo.
Muache baba yako awaletee maendeleo mtamwelewa.siku chache zijazo
 
So ni vyema kuishi nyumba nzuri na hujui hata kula yako ikoje eeeh?.

Ufahari gani huu?
 
Jisaidie mwenyewe , huwezi kumlalamikia mzazi wako kwa maendeleo anayoyafanya huku ukililia chakula wakati una akili ya kutumia JF na kuweka bando ,, maisha yako yatakuwa ya ajabu kuliko unavyofikiri , naombea mzee wako akaze Uzi mpaka utakapopata akili
 
Nimeandika maneno 5 tu. Unaliita povu.

Wewe mshua wako umemshushia misumari hapo umeona fresh au kwavile hayupo humu hawezi kukuuliza kwanini unamtemea povu?
Kwanza si maneno matano rekebisha.
Kingine basi asilazimishe kupongezwa kwa mambo ambayo ni wajibu wake.
 
Habari wadau. Baba ni mda mrefu tangu aoe kwa hiari yake amekua akifanya mabadiliko ya maendeleo ya vitu na si kwa sisi wanafamilia. Watoto hatuli milo ya kueleweka maisha magumu ila kila siku ni ujenzi wa nyumba na matumizi ya kujifaharisha. Sasa tunadaiwa deni kubwa bila kujua tutalilipaje juu ya matumizi haya.
Tatizo kubwa ni baba kutaka pongezi za lazima kwa majukumu ambayo ni lazima afanye pale nyumbani.
Tumsaidieje baba yangu????
Mkuu naona umetembea na "codes"
 
Baba anajua kua hamuwezi kufa na njaa kwasababu kwanza ardhi ya kutosha ya kulima ipo na watoto mtaitumia ipasavyo kuzalisha mahitaji ya nyumbani na hata ziada

Anachokifanya ni hivi, huko unakosema anapeleka rasilimali za familia ili kuleta maendeleo ni kwamba anakutayarishieni nyie watoto wake, wajukuu zake ambao ni watoto wenu nyie, vitukuu na vilembwe urithi wa kudumu
 
Ukiona hivyo ujue huyo ni baba jiwe! Dawa ni kumpuuzia na kwenda kutafuta chakula kwa majirani! ukirudi nyumbani unazuga tu na hicho chakula chake kibovu.
 
Baba anajua kua hamuwezi kufa na njaa kwasababu kwanza ardhi ya kutosha ya kulima ipo na watoto mtaitumia ipasavyo kuzalisha mahitaji ya nyumbani na hata ziada

Anachokifanya ni hivi, huko unakosema anapeleka rasilimali za familia ili kuleta maendeleo ni kwamba anakutayarishieni nyie watoto wake, wajukuu zake ambao ni watoto wenu nyie, vitukuu na vilembwe urithi wa kudumu
Tatizo deni mzee baba. Matumizi haya yoote ni kwa kukopa na kusababisha deni la familia kua juu juu zaidi.
Huoni baadaye vitukuu ambao elimu yao haijaliwi na wanaishi kwa njaa na taabu watashindwa kulipa hilo deni?.
Huoni kua deni likipaa itafika siku vitu vya familia vitapigwa mnada?.
 
Kwahiyo hofu ya watoto ni ya msingi?
 
Habari wadau,

Baba ni muda mrefu tangu aoe kwa hiari yake amekuwa akifanya mabadiliko ya maendeleo ya vitu na si kwa sisi wanafamilia.

Watoto hatuli milo ya kueleweka maisha magumu ila kila siku ni ujenzi wa nyumba na matumizi ya kujifaharisha.

Sasa tunadaiwa deni kubwa bila kujua tutalilipaje juu ya matumizi haya.

Tatizo kubwa ni baba kutaka pongezi za lazima kwa majukumu ambayo ni lazima afanye pale nyumbani.

Tumsaidieje baba yangu?
Mshauri ikiwezekana aoe mke mwingine.
 
Back
Top Bottom