Baba Ambaka Binti Yake Mara 360 Atupwa Jela Miaka 14,400 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba Ambaka Binti Yake Mara 360 Atupwa Jela Miaka 14,400

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Sep 27, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Monday, September 27, 2010 2:43 AM
  Baba wa nchini Philippines ambaye alimbaka binti yake mwenye umri wa miaka 13 karibia kila siku kwa muda wa mwaka mmoja, amehukumiwa kwenda jela miaka 14,400. Mahakama ya nchini Philippines imemhukumu kwenda jela miaka 14,400 baba aliyembaka binti yake mwenye umri wa miaka 13 mara 360 ndani ya mwaka mmoja.

  Baba huyo awali alihukumiwa adhabu ya kifo mwaka 2006 kwa makosa hayo ya ubakaji ambayo aliyafanya wakati mama wa mtoto huyo alipokuwa nje ya nchi kikazi.

  Ikitoa hukumu ya kesi hiyo ijumaa iliyopita, mahakama ya rufaa ya mjini Manila ilitengua adhabu ya kifo aliyohukumiwa baba huyo na badala yake ilimhukumu kwenda jela miaka 40 kwa kila kosa moja la ubakaji alilofanya baba huyo.

  Kwa makosa yake 360 ya ubakaji yaliyokuwa yakimkabili baba huyo alijikuta akihukumiwa kwenda jela jumla ya miaka 14,400.

  Binti aliyebakwa na baba yake ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 22, aliiambia mahakama kuwa baba yake alianza kumbaka mwezi januari mwaka 2001 baada ya mama yake kusafiri kwenda Hong Kong kufanya kazi za ndani na kumuacha yeye pamoja na ndugu zake wawili pamoja na baba yao kwenye kitongoji cha Los Banos, kusini mwa Manila.

  Mkasa huo wa ubakaji uligundulika mwaka mmoja baadae baada ya binti huyo kwenda kuwatembelea ndugu wa mama yake na kugoma kurudi kwa baba yake.

  Huku akilia binti huyo aliwaelezea ndugu wa mama yake jinsi baba yake alivyokuwa akimbaka karibia kila siku. Mama yake alirudi toka Hong Kong na kumfungulia kesi mahakamani mumewe.

  Mahakama ilitupilia mbali utetezi wa baba huyo kuwa alizushiwa kesi hiyo na mkewe ili aweze kuwachukua watoto akaolewe na mwanaume mwingine nje ya nchi.

  Haijajulikana kama baba huyo atakata rufaa hukumu hiyo ya kwenda jela miaka 14,400.

  chanzo: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
 2. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hizi tamaa nyingine jamani! binti yako kabisa?:confused2::confused2:
   
 3. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hii ni laana!! lol!
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Sep 27, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kweli dunia haiishi maajabu!
   
 5. Smiles

  Smiles JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 1,231
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  This is madness, wangenyonga tu kha....:mad2::mad2::mad2::mad2:
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  Mi baba mingine laana tupu.
  Dawa ya mibaba kama hiyo ni kuirga na kuipa hamu za kuingiliwa uwanja mdogo
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Laana hiyo, mbona hawajampiga risasi kabisa? Hafai huyu.
   
 8. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Wangeongeza na kazi ngumu s%*"@!zi taipu zake...!:mad2::mad2:
   
Loading...