Bab Tale: Wasanii wa WCB kutembea na wanawake waliowazidi umri wanamuenzi mtume SAW

Status
Not open for further replies.
Kumbe wanawake wanaotuzidi umri wana kitu flani amazing sana inavyoonekana, nitajaribu niwaletee report
 
Meneja wa kundi laWCB babu tale amedai kuwa wao hawa manage hisia za wasanii wao bali kazi zao, na ameongezea pia wasanii hao kutembea na wanawake waliowazidi umri ni bahati na wanamuenzi mtume Muhamad kwa kuwa naye alitembea na Khadija aliyekuwa amemzidi umri





Hao wala hawaamalizi mwaka watagawana mbawa wait and see

Mimi hata unilipe pesa siwezi kusikiliza mziki wao wa vibao kata
 
Kwasababu mtume alimuoa bi Khadija ambaye alimzidi umri,
Ila hawa madogo hawajaoa wanazini tu,
Si bora yeye alioa sasa hawa wanazini na kutafta kiki ikiwa sijui na masharti ya kalumanzila. Wameji jengea imani potofu waoe ili iwe halali kabisa. Kwani bi Khadija alimzidi mtume miaka mingapi
 
Hawana lolote kujishaua tu, wanataka umaarufu kwa hao maarufu, mbona hawaji chukua mabibi wa uswazi wasio na umaarufu.
 
Loh sasa walitembea tu bila kufunga ndoa ama walifunga na ndoa kabisa.?
 
Tale umekosea sana kutoa mfano wa ujumla kuhusisha matendo ya wasanii na Mtume Muhammad (saw) kwa kuwa yeye hakumhusisha mke wake kama wanavyofanya wasanii wake, bali kwa ajili ua Uislamu tu. Mtume hakuzini, hakutaka umaarufu kwa ajili ya kuonekana (Shirk ya ria). Mtake radhi Mwenyezi Mungu na waislamu kuepusha athari ya maneno yake kwa vijana wetu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom