Baadhi yetu wanatamani taifa lianguke, likumbwe na magonjwa na maafa ili tu Serikali ilaumiwe

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
4,329
2,000
Hivi karibuni kumekuwa na watu wenye fikra hasi kuelekea maendeleo ya kitaifa.

1. Ajali ya treni Bahi. Kuna Watanzania wenzetu wanaikuza habari na kukataa kuwa ni vifo vitatu tu, wanasema namba imefichwa. Wanatamani maafa yangekuwa makubwa sana sababu tu serikali imepeleka nguvu nyingi kwenye miundo mbinu ya reli.

2. Mwanzoni hospitali nzuri ya kisasa ya Mloganzila nayo ilitangazwa kama hospitali hatari ukipelekwa huponi. Kipindi ambacho ilibidi watanzania tujivunie kwa kuwa na hospitali nzuri.

3. Uvunjaji rekodi wa mapato ya TRA, kama taifa ilibidi tushangilie mafanikio na kuongeza juhudi kwani mapato yakiwa makubwa taifa litaweza kwenda mbele kwa kasi lakini kuna Watanzania wenzetu hili nalo hawalifurahii.

Umewaza itakuwaje reli ya SGR ikisombwa na mafuriko? Au kwa bahati mbaya ndege yetu moja ikapata ajali? Je, tutasikitika kama taifa ama wapo watakaoshangilia?

Baadhi yetu wanatamani taifa lianguke, likumbwe na magonjwa na maafa ili tu serikali ilaumiwe. Kama taifa tufanye nini tutoke hapa maana hali inavyozidi kuna hati hati ya adui wa taifa kupata support na kuweza kuyumbisha taifa kirahisi.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
38,384
2,000
Wizi wa kura na mauji sio kitu kizuri. Na hamtaweza kubadili hili mpaka muamue kutenda haki kwa kutokupora haki ya kuchaguliwa. Hili unalifahamu japo unajifanya hulijui.

Kwa taarifa yako maendeleo tuliyo nayo hayafiki hata robo ya wazungu huko kusini mwa Afrika, lakini weusi wa nchi hiyo hawakujali hayo maendeleo ya taifa, bali walidai haki yao ya kuwa huru na kuwachagua wawatakao.
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
4,663
2,000
Damu ya binadamu inanguvu kubwa. Hamtakuwa na amani hadi mtubu kwa wizi, dhuluma, mauaji na kutoa mkono wa amani. Tanzania ni yetu sote. Ya Z'bar yanaleta walau matumaini Bara tunafeli wapi.
 

Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
7,091
2,000
Mngeyawaza hayo wakati mnatesa,kubambikizia kesi na kuua wapinzani!

Mnataka tusiwe na hisia, shwain!
 

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
624
1,000
Bora kuanguka watu wanategemea lizame kabsaa ibaki Zanzibar tu. Ole wako ujidai kuogelea kuifuata Zanzibar shee watu watakusubiri kwa bakora urudi utukako.
 

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,468
2,000
Kama ilivyo Kwa mtu na mtu kuoneana wivu ndivyo ilivyo Kwa Vyama na wanachama wa vyama mbalimbali kuoneana wivu wa Kwa nini tusingekuwa Sisi?

Wivu wa Kwa nini huyu anajenga na kufanikiwa Sana kwenye maswala mbalimbali,Kwa nini isingelikuwa Sisi?

Wao wanaomwonea wivu kiongozi aliyepo, wanaamini kabisa kwamba, hayo mafanikio yanayofanywa na serikali yake ndio yanayompa nafasi ya kuendelea kukubalika zaidi Kwa watu.

Wapinzani wanachokifanya ni kugeuka kuwa upande wa shetani kuombea mabaya na kuponda kila kizuri kinachofanywa kukigeuza kuwa ni kibaya na hakifai.

Nataka niwathibitishie, hata Mungu hatakubali, kwani Hata kama Raisi ni mbaya sana, lakini Kwa sadaka atoayo Kwa Watanzania ni Bora mara 10000 kushinda mtazamo wa ubaya wanaoueleza wapinzani wake na atazidi kufanikiwa.

Acha wao wauvae ushetani kuombea vifo vitokee Kwa Watanzania wenzao na binadamu kama wao na wanaowaombea wage au washindwe ni binadamu kama walivyo wao, huo kama sio ushetani utaita nini?

Mungu hawezi kusikiliza Ujinga wa upinzani wa Aina hiyo!

Mungu ibariki Tanzania
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,089
2,000
Sidhani kama kuna Mtanzania anaeweza kuiombea mabaya nchi yake, ni hali tu ya kujishtukia kwa watawala na nyie wafuasi wao.
 

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
4,329
2,000
Watu wanavyoimba kunaihitajika umoja wa kitaifa mnawaona wehu! na bado.

Bado nini tatizo maafa hayaendi kwa hao wanaochukiwa tukikosa hela unadhani maumivu anayapata Rais au sisi raia? Ajali za treni tunapata sisi na ndugu zetu sio Rais chuki ipelekwe kwenye kudai katiba sio maumivu ya wenzetu.
 

dolevaby

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
11,630
2,000
Hivi karibuni kumekuwa na watu wenye fikra hasi kuelekea maendeleo ya kitaifa

1. Ajali ya treni Bahi. Kuna watanzania wenzetu wanaikuza habari na kukataa kuwa ni vifo vitatu tu, wanasema namba imefichwa. Wanatamani maafa yangekuwa makubwa sana sababu tu serikali imepeleka nguvu nyingi kwenye miundo mbinu ya reli.

2. Mwanzoni hospitali nzuri ya kisasa ya Mloganzila nayo ilitangazwa kama hospitali hatari ukipelekwa huponi. Kipindi ambacho ilibidi watanzania tujivunie kwa kuwa na hospitali nzuri.

3. Uvunjaji rekodi wa mapato ya TRA, kama taifa ilibidi tushangilie mafanikio na kuongeza juhudi kwani mapato yakiwa makubwa taifa litaweza kwenda mbele kwa kasi lakini kuna watanzania wenzetu hili nalo hawalifurahii

Umewaza itakuwaje reli ya sgr ikisombwa na mafuriko? Au kwa bahati mbaya ndege yetu moja ikapata ajali? Je, tutasikitika kama taifa ama wapo watakaoshangilia?

Baadhi yetu wanatamani taifa lianguke, likumbwe na magonjwa na maafa ili tu serikali ilaumiwe. Kama taifa tufanye nini tutoke hapa maana hali inavyozidi kuna hati hati ya adui wa taifa kupata support na kuweza kuyumbisha taifa kirahisi.
Umewahi kujiuliza kwanini watu wanatamani hivyo?

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 

redio

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
2,317
2,000
Watu wa ainaiyo hawata isha, wengine walisha wahi kuwaona wazazi wao madikteta kisa walikua wakisimamia misimamo yao, ata JK alitukanwa Sana kisa alikua akitabasamu ata wakimtukana.

Ata Rais atayekuja baada ya JPM ata tukanwa na kudhihakiwa. Kama mitume na mana bii walitukanwa wakadhihakiwa Waka uwawa itakuja kuwa JPM !!.

Gadafi alifanya Kila aliloweza kusaidia watu wake lakin mabeberu waliwatumia wananchi wake wamwondoe madarakani na ku muua, Kwasasa Libya Wana enjoy show ya Mabeberu.
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,021
2,000
Mm namba moja. Simpendi huyo "mponya" korona wenu. Mshamba na limbukeni huyu basi tu.!!
 

Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
2,335
2,000
Wizi wa kura na mauji sio kitu kizuri. Na hamtaweza kubadili hili mpaka muamue kutenda haki kwa kutokupora haki ya kuchaguliwa. Hili unalifahamu japo unajifanya hulijui.

Kwa taarifa yako maendeleo tuliyo nayo hayafiki hata robo ya wazungu huko kusini mwa Afrika, lakini weusi wa nchi hiyo hawakujali hayo maendeleo ya taifa, bali walidai haki yao ya kuwa huru na kuwachagua wawatakao.
Kwani ulizuiwa kumchagua umtakaye?
 

Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
2,335
2,000
Damu ya binadamu inanguvu kubwa.Hamtakuwa na amani hadi mtubu kwa wizi ,dhuluma,mauaji na kutoa mkono wa amani.Tanzania ni yetu sote. Ya Zbar yanaleta walau matumaini Bara tunafeli wapi.
dua la kuku
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom