Baadhi yetu kwa viongozi wetu wa CHADEMA, Mbowe sio kiongozi wa kutubadili

Avanti

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
1,209
1,195
Siandiki kwa ajili ya kumchukia Mbowe, hapana! Ni uhalisia wa mtazamo uliojengeka kwa baadhi yetu ambao yawezekana ni wachache sana na hivyo ninyi wengi mna mtazamo chanya kwa Mbowe.

Nakumbuka (mfano halisia), mwaka 2007 nilimwuliza mdogo wangu aliyekuwa akisoma UDSM ni kwa nini ghafla alitokea anamchukia sana JK ilhali mwaka 2005 wakati akigombea URais alikuwa akimpenda sana. Mdogo wangu akaniambia JK mara baada ya kupata URais alitembelea UDSM na kuwaambia hamna mwanachuo angefukuzwa (au kuachishwa masomo) kwa kuwa hakuwa na fedha za kulipa malipo yale ya awali ili mtu awe admitted kwa masomo.

Mmoja wa marafiki zake mdogo wangu ambaye hakuwa na uwezo wa kulipa fedha hizo na baadhi ya wenzao wakasimamishwa chuo. Wakafuatilia na ilifikia hadi wakafikisha ujumbe kwa JK lakini hawakusikilizwa na yule refiki yake mdogo wangu hakuendelea tena na masomo na nadhani pengine yeye na baadhi ya wenzake hawakusoma tena (ingawa sina uhakika). Kitendo hicho kilimsononesha sana mdogo wangu na akamwona JK sio mtu wa kusimamia ahadi zake zitekelezwe na tokea wakati huo mpaka leo anamchukia sana na JK hata afanye jambo gani mdogo wangu huniambia "Unamwona jamaa yako wa kucheka cheka tu".

Kama ilivyo kwa JK na mdogo wangu, kwangu mimi pia Mbowe alinifanyia hivyo hivyo. Nakumbuka ama mwaka 2003 au 2004, Mbowe akiwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mgodi wa Williamson Diamonds - Mwadui walikuja kutembelea mgodi huo na mimi nikiwa nafanya kazi hapo. Wakati huo sisi wafanyakazi tulikuwa na malalamiko kibao na tukiamini kuwa Mbowe kama mbunge wa kutoka chama cha upinzani angejulishwa kilio chetu basi angeweza kusaidia. Bwana we! Mbunge Mbowe na wajumbe wenzake wa Bodi, nakumbuka mmojawapo wa wajumbe hao alikuwepo bwana Phillip Makolo, mbunge wa Kishapu, tukajitahidi kupata nafasi tukawapa barua ya kilio chetu, kana kwamba haitoshi tukaandaa na mabango ambayo baadhi yetu tuliyanyoosha pale airport ya Mwadui kwa nguvu zote, jua kali (nakumbuka wakati huo bunge lilikuwa likiendelea nao walikodishiwa ndege kutoka Dom). Mbowe akapita karibu yetu kishikaji na akasema tumeona, tukafurahi bana!. We! kilichofuata, Kwa kuwa walitua mchana wakitokea bungeni Dodoma, wakubwa hao wakachukuliwa na magari ya wazungu, hao hadi kwenye ukumbi (jina la ukumbi limenitoka kidogo ila ni maeneo ya Boid ya chini, kwa wale wa Mwadui wanaujua ukumbi huo). Huko wakafanya kikao, kulikuwa na ratiba waonane na wafanyakazi, ghafla tukapotezewa, kesho yake tukashangaa mida ya saa sita hivi wakubwa haoooo wanarudishwa airport na magari ya wazungu, haooooo wakapaa hadi Dodoma na jioni yake Mbowe akachangia hoja bungeni (hapo ujue uzoefu wa Mbowe kupaa ulianza siku nyingi). Kwa maana hiyo Mbowe na mwenzake Makolo siku hizo mbili walilamba posho za ujumbe wa bodi WDL na za kuhudhuria bungeni.

Kibaya kilichotokea, baadhi ya wafanyakazi walioonekena kubeba mabango wakafuatiliwa sana, wengine wakahamishwa vitengo na wengine walitafutiwa visa na vibarua vikaota mbawa.

Mbowe mpaka leo hakuwahi kuongelea chochote khs unyanyaswaji wa wafanyakazi wa Mwadui. Kwa miaka hiyo hadi ikawa inavuma kuwa yeye na Makolo walikuwa wakihongwa almasi.

Kwa sababu hiyo kwa kweli mpaka leo hii, mimi Mbowe hawezi kunibadili kifikra nikamwona anaweza kusimamia haki za wanyonge. Naamini enzi hizo angekuwa Dr. Slaa au Zitto Kabwe basi, kilio chetu kingesikika.

Tabia hii ya Mbowe kutojali walalahoi imethibitishwa na hawa pia:


Mh. Mwigulu nchemba madelu, mbunge wa iramba magharibi katika mwongozo alioomba kwa spika wa bunge asubuhi hii amemlipua kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni FREEMAN MBOWE kwamba ametumia madaraka yake vibaya na kuharibu image na heshima ya bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania kwa kukatisha ziara ya kikazi ya mbunge wa viti maalumu chadema mkoa wa arusha joyce mukya ambaye alisafiri kwa kazi za kibunge kwenda Dominica Republic,lakini akiwa new york, MUKYA alipokea simu ya MBOWE kuwa akatize safari yake na kwenda Dubai aungane naye kwa "kazi maalumu' .

MWIGULU ameomba mwongozo kuwa uongozi wa bunge umchukulie hatua mh mbowe kama mtu binafsi badala ya hivi sasa ambapo taasisi nzima ya bunge inachorwa vibaya mbele za jamii ambapo Habari zilizopo kwenye top page za magazeti ya leo yamelichafua bunge zima kumbe mhusika mkuu ni mbowe ambaye ameelezwa kuwa alimwamuru joyce mukya arudi kutoka safarini badala yake aende dubai kwa kazi maalumu wakati tayari alishapokea posho ya bunge kwa safari ya kikazi.

Aidha mwigulu ameomba mwongozo wa kufanyika uchunguzi wa mahesabu kuhusu posho zilizotolewa na bunge/serikali halafu mhusika hakwenda kwenye safari iliyokusudiwa.badala yake mbunge ameenda kuvinjari na hawara

Tutasikia mengi mwaka huu

Na mwingine:

By FaizaFoxy
Mwigulu amesimama kuomba muongozo wa Mwenyekiti wa kikao cha bunge.

Anasema Mbowe aliandika barua bungeni kutaka safari ya Mbunge mmoja mwanamke (inasemekana ni hawara yake) aliyetumwa na bunge na kutumia fedha za safari za bunge alikuwa New York akielekea kwingine, Mbowe aliomba ofisi ya utawala wa bunge kwa barua, safari ya huyo Mbunge ibadilishwe na aende Dubai kula raha na Mbowe badala kutekeleza majukumu aliyopewa.

Huo ndio upinzani, na huyo ndio kiongozi wa upinzani bungeni.

Kimenuka!
 

TEMILUGODA

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
1,372
1,500
Masikini pole,

Ila nakushauri kuwa jitahidi utakapokuwa nje ya chadema usiwe mwanachama kwa kufuata jina la kiongozi bali fuata katiba ya chama,kadhalika kumbuka kwamba hakuna alie mkamilifu chini ya jua.

Kwa ujumla ukifuatilia sana kuhusu chadema, uongozi wa Mh Mbowe umekiweka chama katika mfumo wa dola hivyo ni vema mambo mengine uwaeleze makamanda wanaopita huko katika chadema msingi.

OTHERWISE PIGA KAZI YA CHAMA, HAKUNA KULALA...

PEOPLEEEEEES................
 

Mlayjr

JF-Expert Member
May 7, 2013
377
225
team zito kazini, hamchoki??? NINI HASA SHIDA NI WENYEKITI AU NJAA ZINAWASUMBUA ???? KWELI MNATUMIKA KAMA MA ROBOTI YA CHAMA CHA MAFISADI KWA UJIRA SHILINGI ELFU SABA NA MIA TANO ( nw imepanda kutokana na kuongezeka kwa gharama za kutoa fedha za makampuni mengi ya simu kuongezeka )
 

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,403
2,000
Huyu Avanti ana akili ya kitoto kabisa, I am not convinced amewahi kufanya kazi mgodini na ni mtu mzima. Tangu lini mjumbe wa board anaenda kuongelea mambo ya kampuni bungeni? Kwa nini msingepeleka hoja yenu kwa mbunge wa jimbo? Unajuaje kama labda Mbowe aliongea kikaoni lakini wajumbe wenzie walipingana na hoja, unajua vikao vya BoD vinavyoendeshwa lakini? Anyway ni utoto, ukikua utaacha. Kama bosi wenu muua Panya alivyo mpole saizi baada ya kuona support iko CCM Tu, ndani ya chama wamemtupa kwenye recycle bin
 

Avanti

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
1,209
1,195
Huyu Avanti ana akili ya kitoto kabisa, I am not convinced amewahi kufanya kazi mgodini na ni mtu mzima. Tangu lini mjumbe wa board anaenda kuongelea mambo ya kampuni bungeni? Kwa nini msingepeleka hoja yenu kwa mbunge wa jimbo? Unajuaje kama labda Mbowe aliongea kikaoni lakini wajumbe wenzie walipingana na hoja, unajua vikao vya BoD vinavyoendeshwa lakini? Anyway ni utoto, ukikua utaacha. Kama bosi wenu muua Panya alivyo mpole saizi baada ya kuona support iko CCM Tu, ndani ya chama wamemtupa kwenye recycle bin

Labda kidogoooo umejibu ila kisiasa mtu huwezi kuona unyanyaswaji wa walalahoi ukawa kimya. Kama unaongelea kisheria sawa mkuu!
 

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
11,209
2,000
NI YUPI ATAKAYEFAA NA AMBAYE HATA NUNULIWA AU KUHADAIWA NA MASHEITWANi WENYE KILA HILA NA FWEZA?
 

mkandi

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
281
250
Avant anaweza akawa haelewi protocol ya namna Mbowe angelishughulikia suala hilo; lakini haonekani kama ni mtaalam wa siasa taka.
Si vyema kuongozwa na hisia na matukio pekee kumhukum; wakati mwingine matukio hutengeneza facts, huunganisha dots na kukumbusha.
Kwangu mie; Ushahidi wa KIMAZINGIRA unanifanya nitamani Zitto afukuzwe uanachama kuliko sababu zingine zote kama vile waraka; Lakini ushahidi wa kimazingira pia unaonesha Mbowe si aina ya wapiganaji kama Slaa. Kuweza kufanya siasa za upinzani na biashara Tz, nayo si haba.
Naamini wanaCDM wengi wanaamini hivyo; lakini wanaamini pia vidole havilingani.

tragedy of the commons
 

ifweero

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
7,961
1,225
Huyu Avanti ana akili ya kitoto kabisa, I am not convinced amewahi kufanya kazi mgodini na ni mtu mzima. Tangu lini mjumbe wa board anaenda kuongelea mambo ya kampuni bungeni? Kwa nini msingepeleka hoja yenu kwa mbunge wa jimbo? Unajuaje kama labda Mbowe aliongea kikaoni lakini wajumbe wenzie walipingana na hoja, unajua vikao vya BoD vinavyoendeshwa lakini? Anyway ni utoto, ukikua utaacha. Kama bosi wenu muua Panya alivyo mpole saizi baada ya kuona support iko CCM Tu, ndani ya chama wamemtupa kwenye recycle bin

Hizi porojo haziwezi kuepusha uzembe na uwezo mdogo wa mbowe kiuongozi. Mleta mada amehoji ht ile mbowe kusimama na kulisemea tatizo lao bungeni au ktk mikutano yake, hajaweza na wao waliamini kwa kuwa ni mbunge wa upinzani atawasemea, tena amewahadaa kwa kupita karibu na bango lao na kuwadanganya kuwa nimeona...soma kwa makini hoja zilizoibuliwa kwenye mkakati wa mabadiliko ndio urudi hapa.
 

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,133
1,225
Wewe ni Mmbeya tuu, kwa sababu, Mbowe , hajawahi kuwa mjumbe wa Bodi ya Williamson Diamond , hivyo huu uongo wako kaufremu upya.

Ila wewe inaonekana kuwa kiongozi mzuri kwako ni yule ambaye atapigania maslahi yako binafsi na sio ya jamii nzima, kama ndivyo kiongozi mzuri kwako ni mkeo ama mumeo , ndio mwenye kukupiga nia wewe binafsi.

mengine ,,wataandika wengine, ila hoja yako ni dhaifu sana.
 

swagazetu

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
4,089
2,000
kwa hili jitahid usifuate mtu fuata chama ukifuatu watu wanabadilika cha msingi ni sera za chama.
 

Avanti

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
1,209
1,195
Wewe ni Mmbeya tuu, kwa sababu, Mbowe , hajawahi kuwa mjumbe wa Bodi yaWilliamson Diamond , hivyo huu uongo wako kaufremu upya.

ila wewe inaonekana kuwa kiongozi mzuri kwako ni yule ambaye atapiga nia maslahi yako binafsi na sio ya jamii nzima, kama ndivyo kiongozi mzuri kwako ni mkeo ama mumeo , ndio mwenye kukupiga nia wewe binafsi.

mengine ,,wataandika wengine, ila hoja yako ni dhaifu sana.
Unamsemea? Aje Mbowe mwenyewe aseme thread hii ni umbeya!
 

Avanti

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
1,209
1,195
Du! nimeshangaa sana leo Mwigulu ametoa ushahidi stahiki khs huyu bwana - anafaa kuitwa Maslahi Binafsi.
 

Avanti

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
1,209
1,195
Moderator! Kama inawezekana hii thread iuanganishwe na ile ingine imhusuyo huyu mkuu ya "Mwigulu Alimpua Mbowe ...."
 
Sep 30, 2012
21
0
Huyu Avanti ana akili ya kitoto kabisa, I am not convinced amewahi kufanya kazi mgodini na ni mtu mzima. Tangu lini mjumbe wa board anaenda kuongelea mambo ya kampuni bungeni? Kwa nini msingepeleka hoja yenu kwa mbunge wa jimbo? Unajuaje kama labda Mbowe aliongea kikaoni lakini wajumbe wenzie walipingana na hoja, unajua vikao vya BoD vinavyoendeshwa lakini? Anyway ni utoto, ukikua utaacha. Kama bosi wenu muua Panya alivyo mpole saizi baada ya kuona support iko CCM Tu, ndani ya chama wamemtupa kwenye recycle bin

Hata usemeje kuna ukweli Mbowe ni mchumia tumboni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom