Baadhi ya Wazanzibari wapinga Tanzania kudai eneo zaidi la mpaka wa bahari kuu

Realznzrian na Wana JF,
Wosia ni kitu muhimu sana, Tumkumbuke Mwalimu Nyerere ametuasa sana kuhusu huu Ufa wa Muungano, Sisi Watanganyika na Wao Wazanzibar, Nao Wazanzibar wakishajitenga hawatakaa salama, Wataanza tena nao Sisi Wapemba na wao ni Wazanzibar.
My Take: Hili jambo ni BUSARA na HEKIMA zitumike maana hii dhambi itatutafuna wote, Tuzibe huu UFA, kabla ya maafa
Nawakilisha



Mesej ambayo nimeletewa sasa hivi na
inaelekea inasambazwa inasema hivi:
TWENDENI kwa wingi kike kwa kiume
kesho Jumatatu na saa mbili asubuhi
tuwe tumeshakaa nje ya Ukumbi wa
Baraza la Wawakilishi, Chukwani ili kuonyesha Ulimwengu kuwa
Wazanzbari hatukubaliani na azma ya
Tanganyika na Shamhuna kuiondoa
nchi yetu Zanzibar kwenye ramani ya
dunia. Shime tufike kwa wingi na
utulivu. ” Sisi sote tuna uchungu kwa ndugu zetu walopotea kwa
kugombania nchi yetu….” Source: Ally Saleh Facebook
 
hivi we MS si ni mkeleketwa wa CUF wewe? Unakumbuka wawakilishi wa chama chako walisemaje kipindi Lisu anazungumzia kuhusu huu muungano? Au ndo yale ya ujanja mwingi mbele kiza.

Hebur tukurumbushere vire!
 
Kama inavyoonekana kwa wachangiaji wengi hapa; inaonekana Watanganyika hua wanaumia sana wakisikia Wazanzibari wanafanya harakati za kujitenga na wao na kutaka kua dola kamili! Hivi mimi hua najiuliza kwa nini watu hawa hua wanakua na mwangi wa woga na hofu kubwa kutanda nyoyoni mwao? Nini hasa kilichopo nyuma ya pazia hata wakawa hivi!
 
Baada ya gogoro la CUF/CCM kutulia kwa Maalim kupewa umakamu sasa wanatafuta wapi wafanye migogoro
Kwao kukaa bila gogoro hawajaridhika.

Mwl Nyerere was right, hata wakivunja Muungano lazima Pemb/Znz zivunjike make bila migogoro na kupigana hawaoni kama wanaishi.

Kazi kweli kuishi na watu kama hawa. Na wanasiasa hawana cha maana cha kuwambia zaidi ya kuanzisha zogo tu.

Hivi mtastarabika lini nyie

Hivyo definition ya Ustaarabu kwako ni ipi? Kuvaa, kusema, kuishi au kudai haki? Kama ya kudai haki si ustaarabu basi nyinyi si wastaarabu mara elfu. Kwani si mlisema mtaandamana nchi nzima? Kwani si mlisema nchi haitotawalika? kwani si mlisema damu itamwagika? Sasa hivyo nyie mtastaarabika lini na kuacha kudai haki iwapo unahisi kudai haki si ustaarabu?

Wacha ubwete wewe Zanzibar ni mwalimu wako kwa mengi na hili la ustaarabu tena wala usipime!
 
Wanaacha kwenda kufanya shughuli za kuijenga nchi yao 'zanzibar' wanapenda kuandamana. Huu muungano uvunjike tu wanalelewa kama watoto lakini hawakui wanabakia kuwa watoto. Mleta habari ni hivi muungano hata sisi hatuutaki

Hivyo pale watu walipodai uhuru walikuwa wanacheza kumwaya? Nahofia kuwa nikikuweka sehemu yako utaona ujinsia umeingia lakini wanaume wana aina ya shughuli mbali na wanawake hivyo tuwachie watoto wako tukue!
 
Realznzrian na Wana JF,
Wosia ni kitu muhimu sana, Tumkumbuke Mwalimu Nyerere ametuasa sana kuhusu huu Ufa wa Muungano, Sisi Watanganyika na Wao Wazanzibar, Nao Wazanzibar wakishajitenga hawatakaa salama, Wataanza tena nao Sisi Wapemba na wao ni Wazanzibar.
My Take: Hili jambo ni BUSARA na HEKIMA zitumike maana hii dhambi itatutafuna wote, Tuzibe huu UFA, kabla ya maafa
Nawakilisha

Na turejeshe Ujamaa basi ili wosia usipotee. Hili la Zanzibar sisi tunao wosia kutoka kwa Baba wa Taifa la Zanzibar Karume " Muungano ni kama koti likikubana unalivua". Basi kikoti hichi tulichshonewa tangu tulipoanza kutembea kinatiwa viraka tu badala ya kushona jipya kwa mujibu wa ukuaji wetu?
 
Ngekewa na Wana JF,
Kikubwa hapa ni kuziba huu UFA, maana kila mtu akivutia upande wake, ndiyo kila mtu anakuja na kauli zake


Na turejeshe Ujamaa basi ili wosia usipotee. Hili la Zanzibar sisi tunao wosia kutoka kwa Baba wa Taifa la Zanzibar Karume " Muungano ni kama koti likikubana unalivua". Basi kikoti hichi tulichshonewa tangu tulipoanza kutembea kinatiwa viraka tu badala ya kushona jipya kwa mujibu wa ukuaji wetu?
 
NAFIKIRI WAZANZIBARI WAKO SAWA.

SUALA LA MIPAKA NDANI YA TERRITORIES YA ZANZIBAR HALIHUSIANI NA MUUNGANO.

TATIZO WENGI WETU WATANGANYIKA HATUUFAHAMU HUU MUUNGANO.
KILICHOUNGANWA NI BAADHI TU YA MAMBO; KILA MTU ANA UTAIFA WAKE NA NCHI YAKE.
KAMA SI HIVYO INABIDI TUWASHTAKI TANGANYIKA LAW OF SOCIETY, AU TANGANYIKA MEDICAL ASSOCIATIONS (YAANI WAMEVUNJA KATIBA KUJIITA TANGANYIKA)

TATIZO LAKUTOFAHAMU NINI MUUNGANO NDIO LINAPELEKEA KUANZISHA VITU AMBAVYO VINAENDA KINYUME NA KATIBA (NA NDIO MAANA KERO ZA MUUNGANO ZINAONGEZEKA BADALA YA KUSOLVIWA)

UNITED REPUBLIC HAINA MANDATE YA KUOMBA HILO ENEO; MWENYE HAKI YA KUOMBA NI ZANZIBAR; UNLESS URT WANAWAOMBEA ZANZIBAR HILO ENEO (NA HASA LENGO LILILOSEMWA NI LA KIUCHUMI; AMBAPO SASAHIVI WAZANZIBARI WAMESHAPINGA MAFUTA YAO KUINGIZWA KWENYE MUUNGANO; UNAPOSEMA HILI ENEO NI LA MUUNGANO TENA MAFUTA SI YATABAKI KUWA YA MUUNGANO; HAPO SI TUNAKARIBISHA VITA BADALA YA UJIRANI NA UDUGU MWEMA!!!! MIMI KAMA MTANGANYIKA SIKO TAYARI KUPIGANA VITA NA WAZANZIBARI NDUGU ZETU KWA AJILI YA ENEO LAO).

KUWA NA WAZIRI WA MUUNGANO HAIMAANISHI SISI WATANGANYIKA KUTEKA NA KUINGILIA MAMBO YA ZANZIBAR.
HALAFU HATA WIZARA YENYEWE YA MUUNGANO IPO KINYUME CHA KATIBA (ZILIZOUNGANA NI NCHI; HII WIZARA TENA ITOKEE WAPI; HALAFU IPO CHINI YA JAMHURI YA MUUNGANO!!!!)

TUSIKURUPUKE KATIKA MAMBO YA WATU, TUSOME KWANZA TUJUE; TUSIWAONE WAZANZIBARI WAJINGA; TUNAHITAJI UJIRANI MWEMA NAO; TUKIWABANA SANA WATAVUA KOTI; HALAFU VISION ZETU ZOTE ZITAPOTEA.:hat:
 
Kwani Zanzibar ni nchi au? Nasikia ni kajisehemu ka bongo yaani kama Mwananyamala au kitangiri mwanza.
 
ZANZIBAR INAWEZEKANA SI NCHI KWA MUJIBU WA WANASIASA UCHWARA WA CCM HUKU KWETU WANAVYOTUDANGANYA.

ILA ZANZIBARA WANA KATIBA YAO YA NCHI; NA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO INAITAMBUA KATIBA YA ZANZIBAR.

NAFIKIRI SISI TANGANYIKA NDIO HATUNA NCHI; KWASABABU JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (HILI JINA LISOME VIZURI UPATE KUELEWA) NI MAMLAKA YA UTAWALA/AINA YA UTAWALA (NI TOFAUTI NA KUWA NA MONARCH SYSTEM, NK)

KWAHIYO JAMHURI MAANA YAKE NI MFUMO WA UTAWALA WA KISIASA; SIO MAANA YAKE NCHI. KWAHIVYO JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NI MAMLAKA YA UTAWALA AMBAYO INAONGOZA NCHI YA T......... (TANGANYIKA, NAOGOPA KUITAJA MAANA YAKE HAIPO IMEFUTWA NA NYERERE/BUNGE LA TANGANYIKA) NA NCHI YA ZANZIBAR AMBAYO IMEPRESERVE JINA LAKE.

KWA HIO CCM WATWAMBIE NCHI YETU IKO WAPI.

PASSPORT NI CITIZENSHIP TU; HAIMAANISHI KUWA NI NCHI; IRELAND/SCOTLAND WANATUMIA PASSPORT YA UK; JEE WAO SO NCHI;

CCM WAMEUZA NCHI YETU.:spy:
 
sheria za bahari za kimataifa ni kuwa kilomita 250 kutoka nchi kavu ni mali ya nchi husika. Kwa kuwa nchi inayotambuliwa na UN ni Tanzania hivyo Zanzibar inamezwa ktk hizo kilomita 250 na kutotambulika kabisa .
 
Ngekewa na Wana JF,
Swali ni kama UKUTA wenyewe bado Mzima ni UFA tu, bado utataka tujenge UKUTA mwingine ?? Je hizi gharama za kujenga UKUTA mpya nani atalipa ?? Au ndio Kodi zetu hizi ??? Vidole Vyote havilingani
My Take: Muungano ulikuja baada ya pande mbili kukaa pamoja na kukubaliana, Muungano haukuja hivi hivi tu, Bado tunahitaji kuziba UFA huendane na WAKATI.

Ni kujenga ukuta mwengine, ila tuamuwe ukuta huo tunataka uweje!
 
Kuna mahali nilisema mimi hawa ndugu zetu wa zanzibar this time tuwaachie na wao wakalie kiti cha urais wa muungano kupunguza ili joto watu wakawa wananizomea,and this is just the begining,wamepanga kufanya mambo mengi makubwa kujaribu kuzuiwa dhulma hii ya kutawala tunayowafanyia,nyerere alikua anajua kula na vipofu sasa sisi tokea nyerere afe ujuaji mwiiiiingi matokeo ndio haya,hata tungekua sisi halafu wazanzibari ndio wanatoa marais mfululizo tusingekubali huo ndio ukweli.Ili kutuliza hili tuwaache na wao wakae kwenye kiti cha urais na ikiwezekana na waziri mkuu nae safari hiyo inayokuja atoke kwao,yani zanzibar itoe rais na waziri mkuu sisi wabara tutoe makamu wa rais kwa maana ya mgombea mwenza,waziri mkuu wa kwanza na wa mwisho kutoka zanzibar alikua Salim Ahmed Salim tena kwa muda mfupi tu akimalizia muda ulioachwa na sokoine kama sikosei,sasa utaona ni muda kiasi umepita toka sokoine afe na leo! wako right kutumia njia yeyote kupigania haki zao ndani ya muungano,mimi naungana nao bwana!hatuwezi kuwaburuza kila siku namna hii!
 
zanzibar inawezekana si nchi kwa mujibu wa wanasiasa uchwara wa ccm huku kwetu wanavyotudanganya.

Ila zanzibara wana katiba yao ya nchi; na serikali ya jamhuri ya muungano inaitambua katiba ya zanzibar.

Nafikiri sisi tanganyika ndio hatuna nchi; kwasababu jamhuri ya muungano wa tanzania (hili jina lisome vizuri upate kuelewa) ni mamlaka ya utawala/aina ya utawala (ni tofauti na kuwa na monarch system, nk)

kwahiyo jamhuri maana yake ni mfumo wa utawala wa kisiasa; sio maana yake nchi. Kwahivyo jamhuri ya muungano wa tanzania ni mamlaka ya utawala ambayo inaongoza nchi ya t......... (tanganyika, naogopa kuitaja maana yake haipo imefutwa na nyerere/bunge la tanganyika) na nchi ya zanzibar ambayo imepreserve jina lake.

Kwa hio ccm watwambie nchi yetu iko wapi.

Passport ni citizenship tu; haimaanishi kuwa ni nchi; ireland/scotland wanatumia passport ya uk; jee wao so nchi;

ccm wameuza nchi yetu.:spy:

strong points!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom