Baadhi ya watumishi wa Serikali si waadilifu hata kidogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baadhi ya watumishi wa Serikali si waadilifu hata kidogo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by apolycaripto, Aug 21, 2011.

 1. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 636
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Kwa kiasi kikubwa maisha ya mtumishi wa umma ya kila siku na mali anayomiliki haviendani na kipato chake.Nakumbuka usemi wa Waziri Mkuu mstaafu Mh. Cleophas David Msuya kuwa Watumishi wa serikali wanaongoza kwa kuwa na mali za kutisha.

  Hii ni kutokana na usemi wa mbuzi hula kutokana na urefu wa kamba yake.Haiwezekani kwa mshahara wa 375,000 ama laki tano,ukakuwezesha kukimu mahitaji ya mtumishi (chakula,malazi,mavazi,afya) hapo ukaweza kumiliki majumba ya thamani zaidi ya milioni 80 na si moja.

  Hapa haiitaji takukuru kuja na majibu ya kuiba ama kutokuiba kwani pesa haidanganyi labda useme umeokota almasi/dhahabu kwani hakuna bidhaa inayotoa faida kubwa kiasi chakuwa na ziada inayozidi mtaji Tanzania hii isipokuwa biashara haramu.

  Nyumba nyingi bora na za hadhi yake Dar es salaam na mikoani,sehemu kubwa ni mali za Watumishi wa umma.Hawa ndio tabaka linalolia kuwa mshahara hautoshi kila siku.Si nyumba pekee vilevile watumishi hawa wamewekeza katika miradi hasa ya usafiri ambayo kwao ni rahisi kuisimamia huku wakivuta muda ndani ya Ofisi zao.

  Leo,hatushangazwi kuona daladala,bajaji,taksi nyingi mtaani lakini pamoja na wingi wake bado kwa sehemu kubwa wamiliki wake ni wale wa kipato cha chini (trafiki,afisa kilimo,mhasibu,mkurugenzi halmashauri,mganga mkuu,afisa wa maji n.k).

  Shule za gharama ya juu maarufu kwa jina la ''academy''.Watumishi wa serikali ambao wanaonekana wa kipato cha chini,wanaongoza kwa kusomesha watoto wao huko na ada y mtoto huyo ni pato lake kwa mwaka(mshahara).

  Ebu tujiulize watu hawa wanatoa wapi fedha huku mishahara tunayowapa haitoshelezi kwa matumizi ya mwezi tu.Tazama hesabu hii kisha unipe jibu.Mtumishi wa Serikali mwenye cheo cha Mhasibu ama Afisa kilimo ngazi ya halmashauri(kipato cha 600,000) ambapo pato lake kwa mwaka ni 7,200,00 ongeza na safari wastani wa siku tano kila mwezi (5x12x80,000) ni sawa na 4,800,000 kwa mwaka.Hivyo ukichukua jumla ya kipato chake ni takribani 12,000,000.Mtu huyu anamaisha mazuri,nyumba si chini ya 2,watoto wanasoma shule bora na mambo mengine yanakwenda huku katika ajira anamiaka chini ya 5.

  Kuna bwana mmoja alipata kazi ukubwani katika shirika moja la umma kama meneja fedha na Utawala.Ndani ya miaka sita alikuwa na nyumba tatu za kuishi,hostel mbili za wanafunzi wa chuo kuishi,orofa moja iliyokuwa katika hatua za awali za kumalizika,gari taksi 2,pick up za kubeba mizigo 2 na maduka mawili ya vipodozi na dawa.

  Mtu huyu historia yake inafahamika,hakuwa na chochote kipindi anapata ajira na mwanzo aliishi kwa shida kiasi cha kupanga chumba kimoja katikati ya mji japo alikuwa na tegemezi wengi.Baada ya Wananchi kumpigia kelele kwa yeye kuwadharau kutokana na jeuri ya fedha aliyokuwa nayo,hapo takukuru na usalama wakaingilia kati kumchunguza.

  Thamani ya nyumba yake tu aliyokuwa akiishi ni milioni 220.Mtu huyu baada ya kuulizwa nini chanzo cha mapato yake alidai ni ajira yake.Ofisi husika iliagizwa kuwasilisha mapato yake yote baada ya kodi toka amepata ajira,ilikuwa aibu kwani hazikuzidi milioni 44.

  Leo nimesikitishwa na habari kuwa mtu huyu ameshinda kesi.Nakiri kweli huu ndio utawala bora ''unaozingatia sheria''.

  Rushwa (kupiga deal) ni sehemu ya kawaida sana kwa mtumishi wa serikali hasa aliyekatika mianya ya pesa,ama mwenye kutoa maamuzi ya nini kifanyike.Tazama huko mbezi beach,kunduchi,bunju,mbezi kimara hayo majumba utakuta watumishi wa serikali wanafukuzana na wafanyabishara.Hatupingi mikopo,lakini dalili za mtu aliyekopa na aliyeiba huwa ni tofauti.

  Najiuliza nchi itakuwaje kama uthibiti wa fedha za serikali hautoruhusu centi kupotea ama kwenda isipofahamika.Bila shaka vyama vya wafanyakazi vitafanya kazi ya ziada kudai ongezeko la mishahara na maslahi mengineyo iwapo hali hii itajitokeza.Hapa ndipo watanzania watashuhudia nchi ikichomeka kwani njaa itaonekana tofauti na saa hizi wengine wapo kivulini (mrija unapitisha maziwa ya kutosha kutoka bomba kuu) na wengine juani(hawana kamba ya kupima urefu wa kula).

  Wasalaam
   
 2. Researcher

  Researcher Senior Member

  #2
  Aug 21, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  I actually thought there will be no response to this one....I was so damn right.

  Tupo kwenye jamii iliyojaa wezi na wanya'anganyi wa aina nyingi, tofauti ikiwa ni nani anatumia njia gani na ni zipi zinazopigwa vita zaidi na jamii husika. Jamii ya ni yupi amebainika na kuanikwa kwenye vyombo vya dola, bungeni, gazetini au mtandaoni (na huyo alimuanika anafaidilka vipi kwa kufanya hivyo). Bila kusahau pia kwamba huyo muhusika ana nguvu kiasi gani ya kujinasua na hatimaye kujirejeshea hadhi yake afterwards...

  One thing is for sure mkuu, WE ARE BOTH HERE!. In this particular time and space.not fifty years ago not fifty years to come no! now (2011). Not in Switzerland or China no!, in Tanzania. And I have guts to tell you IN THIS CORRUPT society..

  Ni kweli kila jambo kwa dhamira na wakati wake na kwa upande wako leo ni fursa ya watumishi wa umma, naomba nikuunge mkono ktk hilo..Kama sehemu ya jamii hii naweka bayana kwamba sipati manufaa yoyote katika kuwabariki wezi wa aina yoyote hata wakiwa watumishi wa umma..

  Ila napenda wakati tunatafakari tatizo lao tusisahau kwamba sio watumishi wa umma wanatulazimisha kujenga nyumba za kuishi kama magereza kulinda mali zetu, wala si wao pekee wanaokwepa kodi na kutoa rushwa..... Im sorry kama natoka nje ya mada.Si watumishi wa umma waliojaza Nyumba za sadaka dar es salaam na kuacha wengi wanaohitaji kumjua Mungu huko vijijini...Sidhani kama nina haja ya kuoroshesha maovu yanayohusiana na wizi katika jamii yetu...anyone can do the maths kwamba kila kundi la wanajamii linaguswa kwa namna moja au nyingine..

  At least tunaweza kuona kwamba kuna tatizo la msingi litokanalo na utu wetu na mitazamo yetu, lakini pia kuna tatizo kubwa la mfumo tulioujenga..Mfumo ambao unayaruhusu kuwalea na kuwabariki wezi na wanyang'anyi kiasi cha kuwapa uwezo wa kutuzuia hata kuwaita wezi ili hali tuna ushahidi wa wizi wao..mfumo huo huo ambao unatusukuma kuwaita wezi wale wachache wanaobainika na kuwaacha wengi JUST GETTING AWAY WITH IT.

  CHAGUO NI LETU
  Aidha tuendelee kumlaumu mtumishi au mwanajamii mmoja mmoja anayekumbwa na ajali ya kubainika, au kuwanyooshea vidole watu watatu kama chanzo cha matatizo ya wenzao milioni arobaini au tuukubali ukweli na tuwe tayari kuukubali ukweli na kuliangalia upya tatizo.

  Ni kwa namna gani tunaweza kujenga hofu, na kutoa motisha AGAINST wizi na unyang'anyi wa namna au kiwango chochote...

  Swali la msingi ni je tuanzie wapi?

  Wengine wanasema kupitia siasa ila sina hakika....nitaendelea na huu mjadala somehow somewhere, kwa leo naishia hapa.
   
Loading...