Baadhi ya watu wanaokukatalia mahusiano ya kimapenzi wanakupenda

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
892
1,226
Habari wanaJf.

Nikiwa nabadilishana mawazo na mmoja ya wafanyakazi wenzangu, ikaibuka story ya kukaziwa na demu jamaa si akanipa story hizi nikaona sio dhambi nishare nanyi.

Jamaa alikutana na dada mmoja kwenye daladala akamchombeza mpaka ikafikia hatua mtoto wa kike akampa namba zake.

Baada ya pale mawasiliano baina yao yalipamba moto, mpaka ikafika kipindi wakaanzisha mahusiano ya kimapenzi.

Siku zilivyokuwa zinaenda walianza kukutana migahawani, jamaa alifanikiwa kumshawishi mdada akakubali angefika kwake Magomeni.

Siku bidada anafika Magomeni jamaa alikuwa amejiandaa kwa kila kitu anshawishi wafanye mapenzi.
Mdada alipofika story na vinywaji vikanoga mwishowe jamaa akaanza kuforce mchezo. Bidada alikataa katukatu na matusi kibao.

Jamaa alikasirika ila hakumwambia, baada ya ile siku yule dada kuondoka mwana akamkaushia akawa hajibu sms wala kupokea simu.

Baada ya kupita week moja jamaa alipokea text kutoka kwa yule dada akimwomba msamaha kwa kukataa kufanya nae mapenzi, lakini pia akimjulisha ni muathirika wa virusi vya UKIMWI ndio maana mara nyingi jamaa alivyokuwa anamforce akakataa.

Kuanzia siku hio nimejifunza papara zinaua aise, kuna wanawake wengine sio wagumu ila wana roho nzuri.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mbona mimi huwa nakumbuka kinga, wengine mnamatatizo gani???
Mbali na kuwa unajinginga ma maradhi hivi akisema yupo siku za hatar mkifanya utampa mimba unafaanzaje kutaka game na huku kinga hunaaa...?
 
Back
Top Bottom