Baadhi ya watu mnaofanya Computer diagnosis kwenye magari mnawamislead wateja wenu na kuwaingiza gharama zisizo za lazima

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,327
9,321
Baadhi ya watu wamekuwa wakifanya OBD2 diagnosis kwenye magari. Ni kitu kizuri na kwa upande fulani kinaweza kurahisisha kutatua tatizo la gari husika hasa ukizingatia kwamba tatizo moja la gari linaweza kuwa na possible causes hata 10.

Tools zinazotumika kufanya diagnosis zipo za aina nyingi, Baadhi huonesha tu code na hivyo itamlazimu mtu aingie mtandaoni atafute hiyo code inahusiana na system gani, Zingine huenda mbali kidogo kwa kuonesha code na kuandika tatizo lipo kwenye system gani, zingine huonesha code na kutaja tatizo lilipo lakini pia huorodhesha sababu zinazoweza kupelekea hilo tatizo na zingine huwa zina mpaka live data hivyo kumuwezesha mtumiaji kuweza kuona live performance ya baadhi ya sensors na systems wakati engine inarun.

Sasa shida inakuja mtu anapojua kwamba fault ni kitu fulani. Mfano labda umepata code ambayo ni ya Mean Absolute Pressure(MAP) sensor. Wengi atakuambia nunua MAP sensor mpya kwa sababu tu ya code alizozipata kutoka kwenye obd2 scanner yake. Sometimes sensor inaweza kuwa ni nzima kabisa ila shida ikawa leakage kwenye vacuum line kutoka kwenye sensor hadi kwenye intake manfold, poor grounding kwenye sensor au poor or no voltage supply kutoka kwenye battery. Katika hizi case 3 nilizotaja ukimuambia mtu akanunue sensor mpya ni kumuingiza tu gharama ambazo siyo za lazima.

Mifano mingine ni hii:
1. MAF sensor, Kama mtu atapata code ya MAF sensor, Apart from sensor kuharibika, Pia shida inaweza kuwa ile hot element ya sensor imekuwa dirty(Inaweza kusafishwa), poor grounding au poor voltage supply kwenye sensor.

2. Idle Air Control Valve(IACV). Hii na yenyewe apart from kuharibika inaweza tu kuchafuka hiyo ikahitaji kusafishwa na kurudishiwa au ikawa ni poor electrical connection kati ya sensor na parts zingine za gari yako.

3. A/F ratio sensor/ Oxygen sensor. Hii kuharibika kwake huwa ni kukatika kwa heating element. Lakini kama Exhaust manfold gasket inaleak inaweza kupelekea less Oxygen molecules zifike kwenye sensor na hivyo basi lazima isome code ya O2 sensor lakini pia shida inaweza kuwa poor wiring harnesy ya sensor.

4. ECT sensor. Hii nayo sometimes inaweza tu kuwa imechafuka ila nzima kabisa. Hasa ukizingatia watu wengi huwa wanatumia maji badala ya recommended coolants. Kwa hiyo inakuwa ni swala la kusafisha na kuirudishia badala ya kununua mpya.

5. EGR valve. Hii nayo inaweza kuwa nzima kabisa ila shida ikawa tu ni deposit ya carbon au leakage kwenye baadhi ya hoses zake. Au poor electrical connection kwenye solenoid yake.

Matatizo mengi niliyoyataja hapo juu yanaweza kurekebishika bila kubadili component ya chombo cha mtu na hivyo kumuepusha na gharama ambazo si za lazima. Au kama kuna ulazima wa mtu kubadili component fulani katika gari yake hasa kwa hizi electrical components basi ni vizuri hicho kitu kikawa tested ili kuprove kwamba ni kizima au kibovu. Kila electrical component kwenye gari inaweza kuwa tested kuanzia spark plug, injectors, sensors, Valves, relays n.k.

Ni hayo tu...



Pia unaweza kusoma

Kuna umuhimu mkubwa sana kufanya check up ya mifumo ya umeme na electronics kwenye gari yako
 
Aisee mkuu kuna jamaa humu JF anaitwa chilubi nilishawahi kubishana nae humu khs hii mambo ya kutumia OBD2 ikisoma faulty tu fasta unaenda kununua kifaa sio sahihi kabisa akabisha nikampa point kana ulizomwambia,cheki hapo chini.
Cheki post no. 21&22 kwny hio thread.
Noah inazingua sana (linamiss na kuwaka taa ya check engine) naombeni msaada

Screenshot_2020-06-19-22-07-14-1.jpg
Screenshot_2020-06-19-22-07-19-1.jpg
 
Aisee mkuu kuna jamaa humu JF anaitwa chilubi nilishawahi kubishana nae humu khs hii mambo ya kutumia OBD2 ikisoma faulty tu fasta unaenda kununua kifaa sio sahihi kabisa akabisha nikampa point kana ulizomwambia,cheki hapo chini.
Cheki post no. 21&22 kwny hio thread.
Noah inazingua sana (linamiss na kuwaka taa ya check engine) naombeni msaada

View attachment 1483673View attachment 1483675
Sikumbuki kama nimesema kuwa eti ukiona faulty code uwende ukanunua tu spea fast, ila nilichosema ni hichi hapa;

Capture.PNG

Nafikiri ukifanya google search ya code uliopata, utapewa na maelezo. Naomba usome vizuri hapo.

Usichanganye na nliposema kwenye O2 sensor, na hapa niliomaanisha ni hio ya heater circuit malfunction na hata hio pia nimesema LABDA IWE HAMNA UMEME.
 
Sikumbuki kama nimesema kuwa eti ukiona faulty code uwende ukanunua tu spea fast, ila nilichosema ni hichi hapa;

View attachment 1483757
Nafikiri ukifanya google search ya code uliopata, utapewa na maelezo. Naomba usome vizuri hapo.

Usichanganye na nliposema kwenye O2 sensor, na hapa niliomaanisha ni hio ya heater circuit malfunction na hata hio pia nimesema LABDA IWE HAMNA UMEME.

Lakini mkuu hata hivo mafundi wengi bado sana kwenye hizi valves, sensors, n.k.
 
Thanx mkuu

Tatizo kubwa lililopo kwa mafundi na wamiliki wa magari ni kukimbilia kurekebisha sensor inayoreport error! Kutokana ba engine ya gari kuwa na parts nyingi, lengo la kuwa na mfumo wa "sensor" ni kumtaarifu mwenye gari hitilafu iliyopo, yaani sensor ni kama dira tu kukupa mwongozo mahali penye tatizo.

Then kupitia mwongozo huo mmiliki atafanya "in-depht diagnosis" sehemu yenye tatizo, inaweza ikawa ni replacement au repair ya kifaa kama mtaalamu alivyoeleza hapo juu.

Kukimbilia kubadili sensor bila kujiridhisha tatizo lililopo ni mis-use ya pesa
 
Thanx mkuu

Tatizo kubwa lililopo kwa mafundi na wamiliki wa magari ni kukimbilia kurekebisha sensor inayoreport error!
Kutokana ba engine ya gari kuwa na parts nyingi, lengo la kuwa na mfumo wa "sensor" ni kumtaarifu mwenye gari hitilafu iliyopo, yaani sensor ni kama dira tu kukupa mwongozo mahali penye tatizo.

well said mkuu.
 
Kwani wapi wanatoa elimu ya huo ufundi ili tupeleke ndugu wasikae kusubiria kusoma accounts afu wakawa jobless?
 
Mimi apart from degree yangu ambayo niliipata darasani plus kushinda garage kupata uzoefu. Nimeshinda sana youtube.

Matatizo mnayoongelea hapa yapo sana mtaani na watu tunaharibiwa sana vijiusafiri vyetu, binafsi nataka nifanye hiyo Computer diagnosis kwenye gari yangu lakini nasita sana kwani hata bei ya kazi hiyo haieleweki mfano ni mtaani kwangu kuna mvimba macho mmoja anayo hiyo computer eti anapima kwa 40,000/=

Pale Kimara kuna jamaa yeye kaniambia 100,000/= na atapima kila kitu na kurekebisha wakati Kariakoo nikaambiwa 200,000/= kupima tu mwisho nikamfuata mdosi mmoja huko Chang'ombe yeye akaniambia kitu kama 300,000 pamoja na matengenezo, wakati gari yangu Noah ikiwa na tatizo la kuchelewa kuingiza gia (Auto) na break system ina matatizo kiasi, Hebu naomba ushauri wenu ili nitoke kwenye ujinga huu wa kufanywa "Makuliwa"
 
Degree ya Automotive au

Je unaweza andika Channels ili watakaoweza wajifunze huko maana kazi hakuna ila magari yananunuliwa mengi ila mafundi hawajiongezi wako analogue

Okay mimi nilikuwa natumia random youtube channels. Ila kuna hizi mbili ambazo zinamilikiwa na mtu mmoja ndio nimezikariri. Moja inaitwa Chrisfix na nyingine inaitwa Ratchets and Wrenches.
 
Nisahihi kuifanyia gari tunning ya mafuta?? nimeshauliwa hvyo baada ya gari kuwasha taa ya check engine kila baada ya cku kadhaa,tatizo liligundulika kuwa ni mafuta niliyokuwa nimewek
 
Matatizo mnayoongelea hapa yapo sana mtaani na watu tunaharibiwa sana vijiusafiri vyetu, binafsi nataka nifanye hiyo Computer diagnosis kwenye gari yangu lakini nasita sana kwani hata bei ya kazi hiyo haieleweki mfano ni mtaani kwangu kuna mvimba macho mmoja anayo hiyo computer eti anapima kwa 40,000/= pale Kimara kuna jamaa yeye kaniambia 100,000/= na atapima kila kitu na kurekebisha wakati Kariakoo nikaambiwa 200,000/= kupima tu mwisho nikamfuata mdosi mmoja huko Chang'ombe yeye akaniambia kitu kama 300,000 pamoja na matengenezo, wakati gari yangu Noah ikiwa na tatizo la kuchelewa kuingiza gia (Auto) na break system ina matatizo kiasi, Hebu naomba ushauri wenu ili nitoke kwenye ujinga huu wa kufanywa "Makuliwa"

Mkuu mimi kwa bahati mbaya sana sina hiyo mashine ya OBD2 scan tool kwa sasa ila nafanya mpango wa kuagiza nje. Ila ninachoweza kupima kwa sasa ni sensor, valve, n.k. mojamoja kwenye gari, na ndio maana mara nyingi namshauri mtu aanzie kwenye hiyo mashine ya OBD2 ili akija kwangu na hizo code iwe rahisi kuconfirm hilo tatizo alilolipata kwe system husika kwa kupima hizo sensors valves n.k. then hapo naweza kumshauri cha kufanya.

Anyway kama utapata mtu mwenye mashine ambayo inaonesha Live data itakuwa ni vizuri zaidi mtu huyo akakupimia. Kuna baadhi ya matatizo huwa hayaoneshi warning light so kupitia live data inakuwa ni rahisi kujua.

Hayo matatizo yako angalia kwanza kama Transmission fluid ipo ya kutosha au kama umefika muda wa kubadilisha nenda kabadili. Then kama kutakuwa na shida ndio tuanzie kusolve tokea hapo.

Hapo kwenye brake mimi si mtaalamu sana. Ila hujaswma actual tatizo ni nini kwenye braking system.
 
Mkuu mimi kwa bahati mbaya sana sina hiyo mashine ya OBD2 scan tool kwa sasa ila nafanya mpango wa kuagiza nje. Ila ninachoweza kupima kwa sasa ni sensor, valve, n.k. mojamoja kwenye gari, na ndio maana mara nyingi namshauri mtu aanzie kwenye hiyo mashine ya OBD2 ili akija kwangu na hizo code iwe rahisi kuconfirm hilo tatizo alilolipata kwe system husika kwa kupima hizo sensors valves n.k. then hapo naweza kumshauri cha kufanya...

Story ni ndefu ila umenisaidia kitu kimoja ni kweli gari yangu ina matatizo kwenye transmission na break lakini hakuna taa inayowaka NB check DM
 
Back
Top Bottom