Baadhi ya watanzania wanashangilia timu ya taifa kwenda kupambana ikiwa pungufu!

Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
17,142
26,132
Kocha kachagua wachezaji toka simba,yanga na vilabu vingine!Idadi ya wachezaji kutoka Yanga ni 6,Simba ni 2 na timu ya Le_prof ni 1 ila kutimiza idadi ya wachezaji 9 wanaotakiwa uwanjani,yaani hutakiwi kuzidisha hao japo ikipungua chini ya hapo ruksa!

Bahati mbaya vibali vya wachezaji wateule kutoka simba vimewekewa kizuizi na hivyo basi wachezaji hao wamekwama airport kwenda kucheza!

Na waliofanya figisu hiyo ni wana Yanga ili tu wawacheke Simba kuwa hawana mchezaji timu ya taifa!Wakati huo huo muda wa mechi umefika na timu yapaswa kuingia uwanjani,mechi haiwezi aihirishwa hivyo Taifa stars wanalazimika kuingia wakiwa pungufu!

Cha ajabu tunaenda kuipa support timu iliyopungufu ikikabiliana na timu nyingine ikiwa ina wachezaji kamili!

Hivi hapo Simba ndiyo imekomolewa au Taifa stars?

Kama ni Ruzuku,hakuna pesa inayoenda simba wala Yanga kisa tu wachezaji wao wameitwa Timu ya Taifa!

Wanapokuwa Timu ya Taifa,wanapambana kuipa nchi ushindi!

Kama ni Posho,wanapata wao wachezaji na si vilabu!

Sasa kwanin vilabu vifanyiane fitina ili wachezaji wengine wakwame airport ili wao wakacheze wenyewe?

Yaani kweli Yanga mko radhi kwenda timu ya taifa na kucheza pungufu kisa tu mna chuki na wachezaji wa simba?
 
Mbaya zaidi timu hiyo haitafanikiwa kupamba na mataifa mengine kwasababu haiwezi kuapishwa lazima member wawili kutoka CDM wawepo ndiyo team nzima ipate sifa ya kupambana na mataifa mengine.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mbaya zaidi timu hiyo haitafanikiwa kupamba na mataifa mengine kwasababu haiwezi kuapishwa lazima member wawili kutoka CDM wawepo ndiyo team nzima ipate sifa ya kupambana na mataifa mengine.
Kocha atalazimika kuchagua wachezaji vilaza ii tu wasifanyiwe zengwe
 
Mara ngapi timu ikiwa pungufu inashinda dhidi ya timu iliyokamilika?
Kuwa kamili si ticket ya ushindi mjomba.
Acha hiyo pungufu ikapambane
 
Nimekuelewa mfano huo kwa kweli hizo nisiasa za tz je wataenda pungufu bunge la east Africa?
 
Mwanachama wa CCM akifa mi huwa nafurahi sana..naandika Thank you Lord! Mana anatupunguzia matatizo
 
Kwa jinsi mlivyo mabingwa wa kupinga Kila jambo, hata nikikupa mfano utapinga tu.
Bora ninyamaze ili Wewe Uwe mshindi
 
Mbaya zaidi timu hiyo haitafanikiwa kupamba na mataifa mengine kwasababu haiwezi kuapishwa lazima member wawili kutoka CDM wawepo ndiyo team nzima ipate sifa ya kupambana na mataifa mengine.
Kama hii ni kweli basi rudisha majina yale yale bungeni mbwa kala mbwa
 
Back
Top Bottom