Kidzogolae
Senior Member
- Apr 20, 2008
- 133
- 2
Jambo forum pamoja na watz wengine wenye uwelewa, tunayo kazi kubwa ya kuwaelimisha watz wenzetu walio vipofu. si kosa lao, kikubwa najua ni umasikini na kunyimwa elimu, ndo maana hawajui yanayoendelea duniani na tz kwa ujumla. mfano, Lowasa alikula kodi zao, lakini walipomwona kule Monduli waliungana nae, wakamshangilia na kuona kama watz tuliomfichua ni wabaya. pili, kule kwa mzee chenge, au kenge kwa jina lingine wanalomwita watu mtaani. siliafiki jina hili. alipoende kule kwenye jimbo lake, wamemshangilia na kumpa sifa zote, na wanaona kama vile sisi tuliomfichua ni watu wabaya. Naombeni, hivi tufanye nini ili watz wote wajue kinachoendelea duniani? mbona wengi wetu huko vijijini ni vipofu kabisa, ndo maana hadi leo tunaogopa mabadiliko, hata kubadili chama, watu wanafikiri ccm ndo kila kitu, ukibadilisha ccm ni kuleta vita. ndo maana ccm wana wini sana vijijini kwasababu vijijini watu wana uelewa mdogo sana. Mungu saidia watz wenzangu hawa, wajue kuwa hela zinazoibiwa na hawa mafisadi ni za kwao, ni kodi zao. hivyo wao wenyewe ndo wanaibiwa. asante. nimeandika haraka, nitasahihisa vizuri baadae. nafanya kazi hapa, naomba niendelee.