Baadhi ya Watanzania Bwana, Mshahara Kiduchu, Matumizi Juu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baadhi ya Watanzania Bwana, Mshahara Kiduchu, Matumizi Juu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Superman, Dec 22, 2008.

 1. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Najiuliza sana sipati jibu, napiga picha bado sielewi . . . .

  Baadhi ya Watanzania kipatacho chao halali na kinachotambulika kuwa ni halali ni kidogo, ukilinganisha na style ya maisha yao . . . .

  Utawasikia

  - Mshahara hautoshi . . . . Anasomesha watoto Private Schools
  - Kipato kidogo . . . . Anajenga nyumba
  - Maisha magumu . . . Anavaa na kula vizuri
  - Tunapata shida sana na maisha . . . Ana gari . . .
  - Hali ni ngumu sana . . . . Utamkuta bar na kwenye starehe nyingine . . .

  Ndugu zangu nisaidieni ni wapi hasa wanapata kipato hiki cha ziada wakati vipato vyao vyao vyote vya halali vinajulikana . . . .


  I hope sio mafisadi . . . .
   
 2. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wanachukua mkopo SACCOS !!
   
 3. v

  varahala Member

  #3
  Dec 22, 2008
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 8
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata kanchi haka kanaweza kuiga watu wake ili kaendelee
   
 4. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jamani hivi wewe uko Tanzania au mahali pengine.Yaani mara hii umeshasahau rushwa na ufisadi,wewe vipi?
   
 5. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wangechukua mikopo SACCOS wangeishia lupango na kufilisiwa.Si unajua adabu ya Mikopo?
   
 6. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wangechukua mikopo SACCOS wangeishia lupango na kufilisiwa!Si unajua adabu ya mikopo.
   
 7. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Wakulu,

  Tuangalie sana . . . Isije ikawa kikulacho ki nguoni mwako . . . . Hebu kila moja na ajiulize kama mapato halali ayapatayo ndiyo hayo hayo yanamtosheleza katika matumizi yote ya mwezi.

  Kama si hivyo, ni wapi anapata mapato mengine?

  I wonder where the line of Ufisadi can be drawn . . . .
   
 8. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna wengine hawapendi kujionyesha kuwa wana pesa japo wana mishahara mizuri.Ndiyo hao utawakuta wanalalamika hali ngumu lakini weekend ikianza tu huwa hawakosekani sehemu za starehe.
  Halafu kuna swala la marupurupu,visemina,kongamano nk huko nako wakulu hawa inawezekana wanazichanga za kutosha tu.
  Sina uhakika kama hao wote unaowazungumzia unazijua na shughuli zao nyingine ukiacha hizo kazi za ofisini.Wengine huwa wana vi miradi vyao kama kufuga kuku,mayai,ice cream nk hizi zote huwa zinawaingizia kipato.
  Mwisho kabisa ni ujanjaujanja ukiwa na ufisadi ndani yake.Hapa watoto wa mjini wanakwambia 'kila mtu anakula ofisini kwake'!
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,550
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Kuna Watanzania wengi ambao pamoja na kipato chao kidogo wanajinyima sana ili kuwapatia watoto elimu ya uhakika maana wanaujua umuhimu wa kuwa na elimu ya maana hasa katika dunia ya leo. Pia wengine wanabiashara mbali mbali zikiwamo kuku wa nyama, mayai, ng'ombe wa maziwa, kushona n.k. Pia ni ukweli mtupu kwamba SACCO zinasaidia sana Watanzania ambao wamejiunga na vyama hivyo kwa kuchukua mikopo hata ya mpaka milioni au hata zaidi. Jamaa yangu aliongeza makato ya mshahara wake ili na kuyapeleka SACCO ili aweze kuchukua mkopo wa milioni 5 ambao ameshauchukua na kuanza kuurudisha.

  Bado wapo Watanzania wengi tu ambao wanaishi kwa njia za halali.
   
Loading...