Baadhi Ya Wasanii Wetu Hamna Customer Care Kwa Jamii,Yaani Mashabiki Wenu!!!!!!!!!!

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Wasanii [Celebrities] wetu wa Kitanzania wengi wao wamekuwa na mapozi ya ajabu sana wanapokutana na wanajamii mitaani.Tunategemea Msanii ni kioo sio kioo kwa tafsiri hiyo iliyozoeleka.Kwangu mimi msanii ni kioo ni kwa kuwa jamii inakutambua wewe huku mitaani kabla Msanii ajamtambua huyo muhusika aliyemtambua [Mwananchi] Msanii ni nani.

Kuna jamaa yangu tulikaa sehemu tunapata maji yale ya ilala pale basi jamaa yangu alikuwa anatoka pande za kusini akamuona msanii mmoja akabaki anamkodolea sana nikamuuliza vipi?Jamaa yangu akasema yule mdau pale mi namfahamu nikamuuuliza umemuona wapi?akanijibu ndio natafuta kujua yaani navuta picha nimemuona wapi?Nikamwambia poa Ok ukikumbuka utaniambia ummemwona wapi?Tukaandeleza baadae tunakaribia tuondoke eneo husika nikarudisha maongezi yetu nyuma kuwa vipi umemkumbuka yule jamaa umemuona wapi huyo jamaa akasema akumbuki lakini anamjua kwa sura na dhamila yake inatuma kweli anamfahamu jamaa.Kumwondolea akumbuki yake ikabidi ni mwambie huyo ni nani? alikuwa ni mmoja wa wasanii wetu hawa wa muziki wa kizazi kipya hapa bongo.

Ni kweli alikuwa anamfahamu lakin msanii yule hana ufahamu wowote hata kama kuna jamaa yangu anamfahamu yeye huyo Msanii wala uwepo wake hapa duniani ajui kama anapatikana hapa Tanzania mpaka pale watakapokuna uso kwa uso.

Ninachokutana nacho kwenye majiji yetu na hawa wasanii haswa wanapokuwa wanatembea kwenye mitaa yetu n kutembea na kuwatendea wanajamii ndivyo sivyo ya kuonyesha hajuani na yoyote yule pale.

Msanii anapaswa kuwa na sura ya ufahamu wa mtu yoyote anayetoa au kuonyesha sura ya bashasha kwake.Wengine umma unapokuwa na tabasamu kwao kwa kumuona uso kwa uso msanii wao wao ndio uongeza kukunja uso sura kwa kuwa tu wao ni maalufu.Hakika hawajui kuwa kufika kwao huko ni juhudi za raia mmoja mmoja hao hao anaokutana nao barabarani na kuwachunia ndio waliomfikisha hapo.

Mpaka leo uwa nasema wanamziki wa kizazi kipya na wacheza sinema za kitanzania ndio wanaongoza kwa manjonjo hayo [waswahili wanasema mashahuzi,nyodo na mengineyo kutaja].Hakika mpaka leo kimapato na kufahamika bado rekodi ya Lukas Mkenda [Mr Nice] aijavunjwa lakini njia aliyopita baadhi wangetumia kupita na kuvaa viatu hakika leo hii msingekuwa na na hiyo mikogo dhidi ya hao Watanzania mnaowapita mitaani wakionyesha kuwafaahamu mnawapita kama kama treni isiyo na break.

Ukiwa Msanii kila unayekutana nae njiani jua anakufahamu wewe,japo wewe umfahamu yeye,huo ndio ukio kwa kuwa kioo kiko pale kila ajae ujiona hapo.Wewe ubadiliki kuwa tofauti wewe ni yuleyule kama ni Pro Jay au Sugu [hawausiki kwenye Nyodo ndio maana nikawa huru kuwatumia] wanabaki kuwa wao,lakini akija Kibangu akimuona Pro atajikia kumfahamu,bado akija Mwanahawa nae vivyo hivyo atajisikaia kumfahamu hivyo hivyo,lakini wote hawo Pro au Sugu hawajui, huo ndio ukioo wenyewe.

What goes around it will always comiback again!!!!!Pro J anasema usimdharau mtu yoyote.Wasanii wetu amuoni Wasanii wa Michezo kama wacheza mpira wa miguu wao wakati wote furaha tele na bonge ya tabasamu kwa mashabiki na wapenzo wao.Ingawa kuna wacheza soka kizazi siku hizi wanaozunguka kwenye shangwe na baadhi ya wasanii wa music na sinema wanawambukiza ugonjwa huo wa kunata na kujisikia dhidi ya Wananchi.

Nyie endeleeni mtawakuta huku chini wanawasubilia kwa hamu tu.Uwe ni mcheza sinema,muimba mziki au chochote chenye kukupa umaarufu kujulikana kwenye jamii.

Naomba mnisaidie kuwataja mnaowajua wanaonata wakikutana na wananchi mitaani na kujifanya hawawajui wakati wanajua CUSTOMER CARE NI MUHIMU KWA HUDUMA YOYOTE.Au wao wanafikilia customer care ni kwenda Vodacom,Airtell au Tigo.

Nawasilisha
 
Mkuu post ni ndefu sana kidogo niishie katikati ila nimejitahidi kuisoma yote.mkuu naweza kusema post yote hiyo ililenga kuwaambia wasani wote waache kunata mbele za mashabiki wao,sijui kama nipo sawa.ninachoweza kusema nikuwa msanii wakati mwingine ili awe na washabiki wengi basi inafaa anate (aringe) japo inategemea na mazingira.mfano mimi slave ni msanii promota kaniambia leo napiga show hapo kwenu.eti kwa kuwa mimi ni kioo cha jamii basi kila ninae muona njiani nimsalimie na kujieleza kwamba mimi ndo yule msanii slave.kumbuka ktk kila onyesho mashabiki huwa kila mmoja huwa anaenda kuona show kwa malengo yake.wengine wanaenda kwa ajili ya kumuona slave live na si kucheza disco.swali kama huyu msanii kaonekana kabla ya show na wale waliyo kuwa wanania ya kumuona tu unazani wataenda club tena?hivo kunata kuwepo na kuto kunata kuwepo na itegemee na mazingira.
 
Pia hilo swala la customer care ni zuri ila lazima liwe sehemu moja hasa ingependeza cosota ndo wangebeba hilo jukumu kwa niaba ya wasanii wote.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
DSN nachukia sana kugongewa like kwakuwa like zingine ni za joke kwanini usifanye muendelezo wa mada yako?
 
Mh. Wewe naona kweli msanii. Hata likes hupendi.
mkuu nyumba kubwa unaweza ukawa mtu hata umechapia ki uandishi mtu anakupa likes so unajiuliza ni nini kilicho mfurahisha mpaka agonge like.kikubwa ni kuidadavua mada husika hasa mtoa mada ambae ndie mwenye kiti wa mada husika inafaa awe mstari wa mbele sio kugonga like tu.hii ni sawa na wale wabunge wanao sinzia bungeni wakistushwa usingizini na kuambiwa wanasemaje kuhusu hoja? Utasikia naunga mkono hoja mia kwa mia.
 
Back
Top Bottom