Baadhi ya wapinzani aina ya Lema, Sugu, Lijualikali, Msigwa badilikeni, zama zimebadilika kwa sasa

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
Kiukweli awamu ya nne ya Jakaya Kikwete wapinzani mlidekezwa sana ikajengeka baadhi miongoni mwenu tabia ambazo si njema kwa maadili ya kitanzania. Dharau kwa mamlaka, kejeli, matusi, dhihaka na mengineo mengi yenye kuikera jamii ya wastaarbu.

Hili lilichagizwa na kupewa nguvu na baadhi ya vijana waliotumika katika maandamano ya kila mara yasio na tija kwa taifa.

Kipindi cha awamu ya nne ya Jakaya Kikwete baadhi ya wanasiasa wa upinzani walitumia uhuru huo vibaya. Waliposhikiliwa na vyombo vya dola, walitumia makundi ya vijana kuvamia vituo vya polisi kulazimisha waachiwe. Hii kwa waliokua hawajitambui iliwapa kiburi Sana.

Zama zimebadilika kabisa Serikali hii imejikita kurudisha nidhamu iliopote kwa wanasiasa na watumishi wa umma ikijikita kutumikia wananchi ambao upinzani kwa muda mrefu ulituhumu wamepuuzwa.

Kwa sasa vijana na makundi mbalimbali wameelewa dhamira ya dhati ya awamu ya tano katika kuwaondelea kero zilizopigiwa kelele kwa muda mrefu na upinzani.

Kujua hili, hapo nyuma angekamatwa Sugu vijana wa Mbeya wangeandamana aachiwe kwa vurugu nyingi lakini wamemchoka na kumpuuza. Kwa sasa yuko ngomeni na hali ya mji wa Mbeya ni tulivu.

Hali kadhalika kwa Lema, ile miezi minne hatukuona maandamano ya kutaka aachiwe, wamemchoka na kumpuuza. Vijana wako busy wanapambana na shughuli za kujitafutia kipato, wamechoka kutumika pasi na Faida yoyote.

Hili ni funzo kwa wanasiasa model ya watajwa hapo juu.

Wataishia kuilaumu Serikali wakati wao binafsi wanashindwa kutimiza wajibu wao, wanaishi kwa mazoea.

Kikwete aliposema mtamkumbuka mlipomwita dhaifu alimaanisha jambo, sasa mnaona jinsi alivyowadekeza.

Badilikeni, muda bado mnao wa kutosha kwenye uhai wenu, kwani mngali vijana
 
Kama hawajakuelewa na hapa basi hawataelewa tena ila umewaambia jambo la msingi sana katika maisha yao ya kisiasa..siasa sio kejeri kwa mamlaka ambazo hata Mungu anazitambua..sisi wengine hatuna vyama lakini tunatambua serikali iliyo madarakani. Na sisi tusio na vyama ndio wengi sasa iweje nyie kina sugu, lema, msigwa mjione ndio wakuzitusi na kukejeri mamlaka kila kukicha?? Badilikeni aisee
 
..mwanasiasa anaadhibiwa kwa kutumia SANDUKU LA KURA.

..kama siasa za kina Sugu, Lema, Msigwa,...zimepitwa na wakati hampaswi kutumia polisi na mahakama, washtakini kwa wapiga kura wao.
Kikwete aliposema mtamkumbuka mlipomwita dhaifu alimaanisha jambo, sasa mnaona jinsi alivyowadekeza.

Mwasiasa makini huheshimu mamlaka.
 
Wakati tunasubiri sanduku la kura hatuwezi vumilia utovu wa nidhamu kwa kisingizio cha kufanya siasa iliojaa vurugu na uchochezi kwa serikali na mamlaka zake kwa ujumla
 
Kikwete aliposema mtamkumbuka mlipomwita dhaifu alimaanisha jambo, sasa mnaona jinsi alivyowadekeza.

Mwasiasa makini huheshimu mamlaka.

..nyinyi mkubali tu kuwa siasa za ushindani hamziwezi au hamzipendi.

..hata wale wanasiasa ambao ni moderates wamekuwa wakinyanyaswa ktk awamu hii.

..mnachofanya ni kutumia dhamana mliyopewa vibaya kwa kuvitumia vyombo vya dola kisiasa.

..Vitendo mnavyovifanya ndiyo mfano halisi wa kutokuheshimu mamlaka, na kudharau imani mliyopewa na wananchi.
 
..mna-politicize vyombo vya dola huku mkisubiri uchaguzi.

..mbinu hiyo inaweza kuwasaidia kwa muda fulani, lakini baadaye kuna hatari kubwa mbele ya safari.
Mkuu tatizo hutaki kuifikirisha zawadi ya akili aliokujalia mungu. Mna wabunge zaidi ya mia, kwanini kila siku wanaokwaruzana na dola ni walewale?, ndo maana nikasema wabadilike zama zile zimepita, hakuna umaarufu kwa mwasiasa kuleta vurugu, umaarufu ataupata kwa kuisaidia mawazo na fikra jamii yake iweze jikwamua kiuchumi
 
..nyinyi mkubali tu kuwa siasa za ushindani hamziwezi au hamzipendi.

..hata wale wanasiasa ambao ni moderates wamekuwa wakinyanyaswa ktk awamu hii.

..mnachofanya ni kutumia dhamana mliyopewa vibaya kwa kuvitumia vyombo vya dola kisiasa.

..Vitendo mnavyovifanya ndiyo mfano halisi wa kutokuheshimu mamlaka, na kudharau imani mliyopewa na wananchi.

Kwa hoja zako hizo ni dhahiri kwamba idadi kubwa ya upinzani kwao maneno na lugha chafu za kejeli, kebehi na matusi ndiyo siasa za ushindani.

Kama unataka kujua aina ya siasa za ushindani, hudhuria ushindani ndani ya CCM.
 
Hebu tuwekee kipengele ndani ya katiba kuhusiana na hapo kwenye rangi nyekundu. Watu wengine kwa kukurupuka na kuandika upuuzi! Duh!

Kama hawajakuelewa na hapa basi hawataelewa tena ila umewaambia jambo la msingi sana katika maisha yao ya kisiasa..siasa sio kejeri kwa mamlaka ambazo hata Mungu anazitambua..sisi wengine hatuna vyama lakini tunatambua serikali iliyo madarakani. Na sisi tusio na vyama ndio wengi sasa iweje nyie kina sugu, lema, msigwa mjione ndio wakuzitusi na kukejeri mamlaka kila kukicha?? Badilikeni aisee
 
Kwani kuna sharia lazima Wabunge wote wa upinzani wafananane? Jamii haiwezi kujikwamua kiuchumi kama kuna serikali dhalimu ya waongo wezi mafisadi ambao hawaheshimu katiba, Bunge, mahakama na sheria za nchi, uhuru wa habari na uhuru wa wananchi kujadiliana kuhusu mustakabali wa nchi yao.

Nchi yoyote haiwezi kuendelea kwa sera MUFILISI za kukurupuka. Achana na fikra potofu kwamba nchi itajikwamua kiuchumi kwa kukandamiza uhuru na haki nchini.

Mkuu tatizo hutaki kuifikirisha zawadi ya akili aliokujalia mungu. Mna wabunge zaidi ya mia, kwanini kila siku wanaokwaruzana na dola ni walewale?, ndo maana nikasema wabadilike zama zile zimepita, hakuna umaarufu kwa mwasiasa kuleta vurugu, umaarufu ataupata kwa kuisaidia mawazo na fikra jamii yake iweze jikwamua kiuchumi
 
Acha upuuzi ww.Hakuna Mungu Tanzania

Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu sana.
Taifa limegawanyika kabisa
 
Kama hawajakuelewa na hapa basi hawataelewa tena ila umewaambia jambo la msingi sana katika maisha yao ya kisiasa..siasa sio kejeri kwa mamlaka ambazo hata Mungu anazitambua..sisi wengine hatuna vyama lakini tunatambua serikali iliyo madarakani. Na sisi tusio na vyama ndio wengi sasa iweje nyie kina sugu, lema, msigwa mjione ndio wakuzitusi na kukejeri mamlaka kila kukicha?? Badilikeni aisee
Mbona mnamzungumzia sana Mungu kwenye mambo ya kipuuzi? Mamlaka gani hizi za kishetani au? Msitishe watu kabisa.
 
Katika awamu ya 5 upinzani ndio usiotakiwa,wapinzani hata kama watabadilika na kuwa zaidi ya malaika bado watakamatwa na wengine kupotea kama siyo kufanyiwa pyuupyuu.
 
Hebu tuwekee kipengele ndani ya katiba kuhusiana na hapo kwenye rangi nyekundu. Watu wengine kwa kukurupuka na kuandika upuuzi! Duh!
Unapodai uhuru na haki, na mimi nastahili uhuru na haki hiyo hiyo. Soma Ibara ya 29(5) ya Katiba ya JMT (1977).
 
Mkuu tatizo hutaki kuifikirisha zawadi ya akili aliokujalia mungu. Mna wabunge zaidi ya mia, kwanini kila siku wanaokwaruzana na dola ni walewale?, ndo maana nikasema wabadilike zama zile zimepita, hakuna umaarufu kwa mwasiasa kuleta vurugu, umaarufu ataupata kwa kuisaidia mawazo na fikra jamii yake iweze jikwamua kiuchumi

..hebu na wewe shirikisha bongo yako.

..mbona Kikwete na Jeshi la Polisi waliweza kustahimili siasa za wabunge hao wachache mnaokimbizana nao kila kukicha ktk awamu hii?

..my conclusion ni kwamba Magufuli hapendi siasa, hajui siasa, na hataki kujifunza siasa. Magufuli anapenda kutumia ubabe na ukatili dhidi ya yeyote aliyemzidi kwa hoja.

..Kilichobadilika siyo siasa. Kilichobadilika ni kwamba Tz tumechagua mtu mkatili na kumkabidhi vyombo vya dola.
 
Back
Top Bottom